Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au Serikali. Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!

Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara.
 
Kuna kipindi maisha yanakuwa magumu hadi unaanza kuwaza labda mishe za baada ya kufa zitakuwa na uafadhali, ila ndio hakuna namna no retreat no surrender.

"...Death has got to be easy, because life is hard..."

-50 Cent
 
Unakopaje kwa dada wa kazi hana uwezo wowote haa kukupa 50K, 100k.
 
Dah! Mkuu acha tu maisha yasikie tu!

2017 kuna siku niliwahi kuishiwa yaani unajua kuishiwa acheni tu jamani, hasa kwa sisi ambao tunapambana noma sana.

Wazo lilokuja kichwani ni cha kwako ndo kinakusaidia, nikachukua simu yangu nikaitafutia soko kwenye maduka simu kila ninapoingia wananiambia una risit wengine wananipa kiwango ambacho hata shida yangu haiwezi kuisha dah siku hiyo ilikuwa noma sana.

Siku hiyo sikuuza simu asubuhi nikatembea toka Nyamanoro hadi mjini (Mwanza) kazini shida iko pale pale.

Nikawaza nimpige mzinga mama naye maisha kijijini noma nikapiga chini wazo la mama nikakomaa kama siku tatu mpaka nawaza hivi ni kwa nini naishi!!!
 
Wewe jamaa kuna mtu kakutuma ulete huo ujumbe kwangu, shenzi
 
Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.

Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
 
Aise yaani fanya haraka sana umuoe huyo mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…