Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kweli hapo mtu unatakiwa ujifikirie kama kuna umuhimu wa kuleta viumbe wengine dunia hii.. Lakini kama hali inaruhusu hata wasizidi wawili...ili waweze kusaidiana mbele kwa mbele sio unaleta mmoja halafu ghafla wote mnavuta....sipati picha....mpaka nawaza hivi ni kwa nini naishi!!!
Roho ya umasikini inakuandama mkuu. Kwa imani yako ipinge. Maana yake ni kwamba unakuwa na amani sana ukiona wenye shida mpo wengi kuliko mmoja akiondoka kwenye umasikini. Ama badala ya kuongeza bidii unajikuta unarelax kwakuwa mpo masikini wengi.Asee sijui kwanini Ila mada zakuishiwa huwa zinanitia moyo kuwa kumbe sipo peke yangu.
Mkuu Nyamanoro mbona karibu tu? Mimi nikiwa nasoma, nilitembea mwaka mzima kwa mguu, nenda rudi kutoka Ilemela (kule wanapopaita kanisani) hadi Lake shule ya msingi. Hiyo ni adhabu nilipewa kwa colabo la mama mzazi na bibi yangu.Dah! Mkuu acha tu maisha yasikie tu!
2017 kuna siku niliwahi kuishiwa yaani unajua kuishiwa acheni tu jamani, hasa kwa sisi ambao tunapambana noma sana.
Wazo lilokuja kichwani ni cha kwako ndo kinakusaidia, nikachukua simu yangu nikaitafutia soko kwenye maduka simu kila ninapoingia wananiambia una risit wengine wananipa kiwango ambacho hata shida yangu haiwezi kuisha dah siku hiyo ilikuwa noma sana.
Siku hiyo sikuuza simu asubuhi nikatembea toka Nyamanoro hadi mjini (Mwanza) kazini shida iko pale pale.
Nikawaza nimpige mzinga mama naye maisha kijijini noma nikapiga chini wazo la mama nikakomaa kama siku tatu mpaka nawaza hivi ni kwa nini naishi!!!
Nimekusoma vilivyo mkuu🤣🤣🤣Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au serikali.
Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!
Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara!
Ulipata wengeMimi nilishawahi kumkopa baba mwenye nyumba na wakati huo alikuwa ananidai kodi
Mwenye kuelewa ataelewaKwa kweli hapo mtu unatakiwa ujifikirie kama kuna umuhumi wa kuleta viumbe wengine dunia hii..Lakini kama hali inaruhusu hata wasizidi wawili...ili waweze kusaidiana mbele kwa mbele sio unaleta mmoja halafu ghafla wote mnavuta....sipati picha....
Fikiria maisha magumu unaenda kutoa msongo kwa papuchi ya wife na unamalizia humo
unategemea matokeo yake ni nini..
tuliwahi kupitia masha magumu sana kifamilia bado wadogo, mpaka nikawa nawaza kwanini baba alituzaa wengi hivi...
Kwa kweli kama sina uwezo sitaleta viumbe vingine kuja kuteseka duniani...
Wakati huo mmeo amemlala BURE utajua haujuiNdo maana mnadhulumu wadada wa kazi mwisho wanawapiga viberiti ndani, unamwambia unamtunzia mshahara wake siku akitaka kuondoka kwakua kwako vyuma vimekaza unaanza kumpigia hesabu ya vyombo vilivyovunjika ili umtapeli hela yake
Ilikuwaje mkaachana na huyu mama watoto na anakupenda kiasi hiki. Maana mwanamke mpaka akupe hela yake, jua anakupenda.Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.
Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
Ukiendekeza kuuza hivyo vitu! Utabaki kununua mabarafu kwa jilani, lazima ujue vibanda umiza, kulala chini kwako liwe jambo la kawaida!kuna vitu ni muhimu sana.
AKIBA
Kingine jitahidi uwe na vitu vya thamani kama TV,MUSIC SYSTEM, FRIJI, KITANDA, GODORO, N.K niamini hv vitu vinaokoa sana ukifulia maana hata ukiuza ukika sawa vina nunulika
Kama hujawahi kuishiwa huwezi kuelewa pesa ni nini, hata jero utaiheshimu tu, sitasahau siku nilivoishiwa, ni katoa gari niende kutafuta chochote kwa marafiki, nafika mwenge kwenye mataa gari ikaishiwa mafuta kati kati ya barabara hata shilling mia sina, kwenye simu hata ya kubeep sina wale vijana wa kunisukuma kuniweka pembeni ya barabara kabla trafiki hawajaja wakaniomba elf 5 sina........duh Mungu ndo alioniokoa siku hiyo.Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au Serikali. Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!
Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara.
Mkuu naongelea ile shida ya mwisho kabisa kiasi umekosa msaada. Yaweza kuwa unaongea kwa kujiami kwakuwa haijawahi kukuta.Ukiendekeza kuuza hivyo vitu! Utabaki kununua mabarafu kwa jilani, lazima ujue vibanda umiza, kulala chini kwako liwe jambo la kawaida!