Daah nakumbuka msoto niliwahi kupitia kipindi hiko nilivyomaliza form 4, nikakutana na sister yangu mtoto wa mama mkubwa slay queen kipindi hicho ameukwaa u misss Morogoro, maktaba DSM pale navuka zebra yupo kwenye harrier yake mbele na tumeonana kabisa akaangalia pembeni, hapo mfukoni nina 200, nikagonga kioo nimpe hata salamu, akauchuna haangalii kabisa, mara taa zikawaka akainua, aisee iliniuma sana ila Mungu alivyo mwema baada ya kuvuka taa tuu hatua mbili tatu nikakutana na mjomba wangu akaniambia twende hivi, tukaishia mgahawa flani nikapata heavy breakfast na laki moja cash, cha ajabu huyu mjomba ni bahili kinoma kwa ndugu zake wengine.
Nilijifunza kuacha kuhukumu kabla hujamjua mtu, mimi na uncle wangu ni du damu kwa muda huu na huyu sister sijawahi kuacha kumsaidia akija na shida zake, na anakuja mara kwa mara, nilisamehe lakini sijawahi kusahau hii scenario... ipo siku nitamkumbusha