Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kumbe wife wako soon anarudi kutoka kwao? Sasa shida iko wapi si atakuja na mazagazaga kibao, maharage, karanga njegere, ndizi unga wa ulezi, mahindi, maziwa, parachichi etc? Au umeoa kwenye familiya ambayo hivyo nilivyovitaja nao wanavinunua kwa mangi?
Si unajua familia zetu hizi sister za hali ya chini, hivyo vitu kupatikana ni kwa tabu kidogo. Ila nimempanga ajitaidi aje hata na mahindi ili tukisaga unga angalau utusogeze hata mahali fulani kipindi naendelea kuumiza kichwa
 
Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au Serikali. Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!

Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara.
Nenda msikitini au kanisani muombe Mungu hayo yataisha
 
Daah nakumbuka msoto niliwahi kupitia kipindi hiko nilivyomaliza form 4, nikakutana na sister yangu mtoto wa mama mkubwa slay queen kipindi hicho ameukwaa u misss Morogoro, maktaba DSM pale navuka zebra yupo kwenye harrier yake mbele na tumeonana kabisa akaangalia pembeni, hapo mfukoni nina 200, nikagonga kioo nimpe hata salamu, akauchuna haangalii kabisa, mara taa zikawaka akainua, aisee iliniuma sana ila Mungu alivyo mwema baada ya kuvuka taa tuu hatua mbili tatu nikakutana na mjomba wangu akaniambia twende hivi, tukaishia mgahawa flani nikapata heavy breakfast na laki moja cash, cha ajabu huyu mjomba ni bahili kinoma kwa ndugu zake wengine.

Nilijifunza kuacha kuhukumu kabla hujamjua mtu, mimi na uncle wangu ni du damu kwa muda huu na huyu sister sijawahi kuacha kumsaidia akija na shida zake, na anakuja mara kwa mara, nilisamehe lakini sijawahi kusahau hii scenario... ipo siku nitamkumbusha
daah sister mkavu huyooo
 
haya maisha naelewa sana hasa Nkikuta kijana mwenzangu ananiambia kakosa hata nauli kama ninayo huw anampa mara 2 ya aliyoniomba kama mwanaume unaweza kupigika mpaka ukaona wadada wanaojiuza hawakosei 😀 😀 😀 😀 tukaze huku tukiomba wanaangu
 
Kwa kweli hapo mtu unatakiwa ujifikirie kama kuna umuhumi wa kuleta viumbe wengine dunia hii.. Lakini kama hali inaruhusu hata wasizidi wawili...ili waweze kusaidiana mbele kwa mbele sio unaleta mmoja halafu ghafla wote mnavuta....sipati picha....

Fikiria maisha magumu unaenda kutoa msongo kwa papuchi ya wife na unamalizia humo
unategemea matokeo yake ni nini..

Tuliwahi kupitia masha magumu sana kifamilia bado wadogo, mpaka nikawa nawaza kwanini baba alituzaa wengi hivi...

Kwa kweli kama sina uwezo sitaleta viumbe vingine kuja kuteseka duniani...
Kati ya agenda ambayo mama yangu haipendi ni kusikia unataka kuzaa watoto wachache, naishia kucheka na kusema haya...
 
Dah wakuu! Hii situation ya kuishiwa ni mbaya sana na ndo ninayoipitia sasa. Yaani hapa ninavyoandika hii comment mfukoni nimebaki na buku 3 tu! Then ndani stock ya chakula imekata, umeme imebaki unit 1.63 alafu sijala chochote toka asbh na harakati zangu zimeyumba kwa kipindi hiki sio mchezo, mbaya zaidi wife kuanzia kesho siku yoyote anarudi home maana alienda kwao kusalimia mara moja.

Yaani hapa nilipo nimechill gheto nawaza vitu vingi hadi kichwa kinauma. Nilichoamua hapa nimeenda kuchukua unga nusu nitoe kitu badae mishale ya jioni then unga utakaobaki wa kesho, nitachukua na fungu la dagaa, najua kwenye buku 3 itabaki kama 1300 hv hii nitaamka nayo kesho na akili mpya.

Ila ndugu zangu kuishiwa kubaya sana, hapa nimezima kila kitu kinachotumia umeme ili tu usije kukata maana muda wote naichungulia hiyo unit ili inifikishe kesho nijue nafanyaje kusurvive na siku mpya.

NB: Najua hii changamoto ninayopitia mm kuna mtu pia mahali anaipitia at the same time, hivyo cha muhimu ni kujua na kuamini kila jambo linatokea kwa kusudi maalumu na litakwisha tu.
Pole sana mkuu.
 
haya maisha naelewa sana hasa Nkikuta kijana mwenzangu ananiambia kakosa hata nauli kama ninayo huw anampa mara 2 ya aliyoniomba kama mwanaume unaweza kupigika mpaka ukaona wadada wanaojiuza hawakosei 😀 😀 😀 😀 tukaze huku tukiomba wanaangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.

Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
Vipi ulimrudishia pesa yake au aliendelea kunyandua kama malipo yake?
 
Back
Top Bottom