Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Unforgettable experience
 
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
Huna majirani
 
Kuna kipindi nilifulia hadi nikawa nakosa chakula cha kuwalisha mbwa wangu Afu niko Man alone. So chakula nilichokua nakula ilabidi niwe nawabakishia kidogo wasife njaa. To be honest nilikua naongea na mbwa wangu nawaomba msamaha. Mungu atusaidie sana aisee.
 
Ungewatumia hao mbwa mkawinda mpate kula hata visungura
 
Unaweza kufulia mpaka ukatapeli. Nakumbuka kuna siku tumewahi kuazima magunia ya kuhifadhia mahindi kwa jirani yetu tukaenda kuyauza ili wiki isonge. Ila tulivopiga mishe tukanunua tukamrudishia. Mpaka leo hajui tuliazima ili tukauze. Alifikiri tumepata mazao ya kutosha mpaka magunia hayatoshi.
[emoji85][emoji85]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Na hii inasababisha kuwa umefulia kila siku.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Ilikuwaje mkaachana na huyu mama watoto na anakupenda kiasi hiki. Maana mwanamke mpaka akupe hela yake, jua anakupenda.
Ni ubinaadam tu...haihusiani na kumpenda mtu.

Au labda tuseme upendo wa Agape...maana kama naweza kumkopesha mtu mwingine kwanini nisimkopeshe yeye?
 
Yale yale,hapo ukute mume hana kitu wakati ex kaomba kapewa laki 2,sijawahi kuwaamini sana hawa watu...
 
Yanatokea hayo, unamkopa mtu ambae aadae hakusaidii na anakusema tu kwa watu.Muhimu kuvumilia unapokwama
 
Ukioa / Kuolewa na mke/mme mwenye watoto ufahamu umeanza mechi ukiwa Bao moja/ Mbili nyuma. Usiwe mtu wa kufatilia Sanaa, hutaishi nao kwa amani. Huwa hawaachani moja kwa moja.
 
Umemjibu vizuri.

Mimi kuna siku niliyakanyaga nilizingua inshu na nikafulia ile mbaya saaaana na nina deni sio la kitoto kama laki 3 hivi.

Nilikuwa na simu yangu nimenunua laki 6,nikaipiga bei kwa laki 3 na simu haina hata miezi mi2.nikauza nikasolve shida nikawa natumia simu yangu ya zamani sana.

Kikubwa hakuna raha ya kukaa na friji ndani wakati una njaa mambo hayaendi.

Hakuna raha ya kulala kitandani wakati una njaa kali mambo hayaendi.

Hakuna raha ya kuangalia azam tv na njaa tumboni.

Kwa mtu ambae hajspitia kipindi kigumu snaweza kudhani kwamba kuuza vitu vya ndani kunaondoa amani na kufanya mambo yawe mazito.

Ila kwa mtu aliyepitia msoto anafulia na mambo yakawa magumu basi wala haoni thamani ya tv ndani,wala haoni thamani ya ftiji ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…