Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kuna mwaka nilikua nimefulia sina hata sumni nikafanya kosa la mwaka nimeongea na mwanangu mmoja akaniita sehemu njaa inagonga vibaya badala ya kunipa hela ananinunulia bia tu .Mwisho tukaanza nyagi nikawaka vibaya sana akanidrop gheto ye huyooo kwake.Kimbembe nimestuka usiku mnene ile njaa ikawa imejidabo .Simu haina kifurushi,ndani hamna kitu kuna gesi tu.Nguvu sina .Kwa mara ya kwa nza nilikua supu ya marando.Kwa wasiojua marando ni majani yale ya viazi vitamu .Na niliyala asubuhi ,mchana na jioni .Kwa bahati nzuri bi.mkubwa jioni akanipigia ndio pona yangu .Vinginevyo nilikua nafia ndani.
Unforgettable experience
 
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
Huna majirani
 
Kuna kipindi nilifulia hadi nikawa nakosa chakula cha kuwalisha mbwa wangu Afu niko Man alone. So chakula nilichokua nakula ilabidi niwe nawabakishia kidogo wasife njaa. To be honest nilikua naongea na mbwa wangu nawaomba msamaha. Mungu atusaidie sana aisee.
 
Ungewatumia hao mbwa mkawinda mpate kula hata visungura
 
Unaweza kufulia mpaka ukatapeli. Nakumbuka kuna siku tumewahi kuazima magunia ya kuhifadhia mahindi kwa jirani yetu tukaenda kuyauza ili wiki isonge. Ila tulivopiga mishe tukanunua tukamrudishia. Mpaka leo hajui tuliazima ili tukauze. Alifikiri tumepata mazao ya kutosha mpaka magunia hayatoshi.
[emoji85][emoji85]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Roho ya umasikini inakuandama mkuu. Kwa imani yako ipinge. Maana yake ni kwamba unakuwa na amani sana ukiona wenye shida mpo wengi kuliko mmoja akiondoka kwenye umasikini. Ama badala ya kuongeza bidii unajikuta unarelax kwakuwa mpo masikini wengi.

Nb: Sijaandika kwa ubaya
Na hii inasababisha kuwa umefulia kila siku.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Ilikuwaje mkaachana na huyu mama watoto na anakupenda kiasi hiki. Maana mwanamke mpaka akupe hela yake, jua anakupenda.
Ni ubinaadam tu...haihusiani na kumpenda mtu.

Au labda tuseme upendo wa Agape...maana kama naweza kumkopesha mtu mwingine kwanini nisimkopeshe yeye?
 
Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.

Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
Yale yale,hapo ukute mume hana kitu wakati ex kaomba kapewa laki 2,sijawahi kuwaamini sana hawa watu...
 
Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au Serikali. Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!

Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara.
Yanatokea hayo, unamkopa mtu ambae aadae hakusaidii na anakusema tu kwa watu.Muhimu kuvumilia unapokwama
 
Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.

Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
Ukioa / Kuolewa na mke/mme mwenye watoto ufahamu umeanza mechi ukiwa Bao moja/ Mbili nyuma. Usiwe mtu wa kufatilia Sanaa, hutaishi nao kwa amani. Huwa hawaachani moja kwa moja.
 
Mkuu naongelea ile shida ya mwisho kabisa kiasi umekosa msaada. Yaweza kuwa unaongea kwa kujiami kwakuwa haijawahi kukuta.

Mimi jamaa yangu alipata ishu akawa yuko safi alijaza geto safi. Ila mambo yalikuja kubuma akawa anaomba hadi buku. Alichofanya aliuza tv, friji, kabati akajikita na biashara hadi saizi jamaa ni story nyingine. Na vitu vyake ndo vilimuokoa kuishi
Umemjibu vizuri.

Mimi kuna siku niliyakanyaga nilizingua inshu na nikafulia ile mbaya saaaana na nina deni sio la kitoto kama laki 3 hivi.

Nilikuwa na simu yangu nimenunua laki 6,nikaipiga bei kwa laki 3 na simu haina hata miezi mi2.nikauza nikasolve shida nikawa natumia simu yangu ya zamani sana.

Kikubwa hakuna raha ya kukaa na friji ndani wakati una njaa mambo hayaendi.

Hakuna raha ya kulala kitandani wakati una njaa kali mambo hayaendi.

Hakuna raha ya kuangalia azam tv na njaa tumboni.

Kwa mtu ambae hajspitia kipindi kigumu snaweza kudhani kwamba kuuza vitu vya ndani kunaondoa amani na kufanya mambo yawe mazito.

Ila kwa mtu aliyepitia msoto anafulia na mambo yakawa magumu basi wala haoni thamani ya tv ndani,wala haoni thamani ya ftiji ndani
 
Back
Top Bottom