Kuna mwanasimba aliyemuelewa huyu Sadio Kanoute?

Huyu Kanoute hamfikii Kotei kwa kasi hata kidogo. Kasi muhimu wakati wote wa kupandisha na kushusha timu.
 
Yeah! ukweli ni kwamba kwa Simba yetu hii yatasemwa mengi.Kila mtu atafanya analysis kulingana na uelewa wake, lakini jambo linabaki kwamba kama watu wanataka Simba ibaki kucheza birian football lazima ipate creative midfielder ambaye atacheza nyuma ya(na) viungo washambuliaji pamoja na strikers.

Kwa squad letu sasa nadhani, we need to trust Ajibu for this role.Niliwahi kumsikia kiongozi mmoja wa Simba akisema Bwallya atakuwa mbadala wa Chama na wengi wanataka iwe hivyo,lakini hapa jambo letu sio mtu wa kuwa kama Chama, maana Simba haina uhitaji wa Chama, but we need a player to link a team.Mchezaji ambaye atakuwa akitoa pasi makini kwa mshambuliaji au washambuliaji.Kama hili si sahihi basi tunahitaji squad letu liwe linaanza na viungo washambuliaji ambao ni hatari.Na hawa tunao tayari,mfano Banda,D Nyoni,Morrison,Mhilu,Kibu etc.Sifa ya hawa viumbe wanaweza kutembea na mpira bila kupokonywa mahali popote uwanjani, kwahiyo inakuwa rahisi kutengeza gaps nyingi ambazo zinaweza kutoa nafasi timu kuscore bila kuwa na uhitaji wa kutengeza pasi mpenyezo.

Leo hii coach anachagua Dilunga kuanza,Dilunga hawezi kuwin linapokuja one vs one.Siku zote ana style yake ile ya kizamani sana inapokuja one vs one,anachofanya ni kupiga mpiga mbele then tushindane kasi,sasa hayo mambo gani?Unajua timu haina mtu wa kupiga pasi mpenyezo nzuri then unaanzisha kiungo of Dilunga type kama attacking midfielder hapo unakuwa unataka miujiza itendeke au ucheze mpira.

Kuhitimisha ni kwamba bado tuna squad bora,tatizo limekuwa macoach wetu wanavyopanga wachezaji basi tu
 
Sasa kamba namba sita ni slow utafika vipi kwa namba nane kwa haraka??? Namba nane na sita zote zinabidi ziwe kasi kupanda na kushuka.
Mkiwa mnashambuliwa mnakuwa hampo kwenye shepu nzur yeye kaz yake n kuhold kwanza namba sita wote wako slow mkuuu hawako shapu Kama viungo wengine unamuona matic ata kotei alikuwa slow
 
Kwa hali ya timu kwa Sasa ni vigumu kutambua viwango halisi vya wachezaji wetu.....

Lakini katika soka ubora wa holding midfielder unahalalishwa na ubora watu wa forwards na strikers.....

Hata kama holding midfielder atakuwa na ubora kiasi gani pale Kati lakini kama Kyle mbele inaharibika kutokana na ubora duni wa Safu ya ushambuliaji lazima ataonekana anapwaya.....

Ubora wa Lwanga ulikuwa unaletwa uwezo mkubwa wa Luis na Chama....kwa Hali ya Sasa ya Simba hata Lwanga ataonekana hafai.....

Mimi namuona ni mchezaji mzuri na mwenye kujitoa kwenye eneo lake.....na jambo zuri anajua kuyachungulia mashimo.....nadhani akipata strikers na winger wazuri tutaona ubora wake......
 
Huyu Kanoute hamfikii Kotei kwa kasi hata kidogo. Kasi muhimu wakati wote wa kupandisha na kushusha timu.
Yap inawezekana, lakini unaona siku hizi Simba inavyocheza?Kuna wakati wachezaji wanasinzia kabisa uwanjani. Leo hii unaweza kusema Kanoute hana kasi lakini angalia watu anaocheza nao.Sasa hivi naomba kama unaweza rejea mechi za Simba za msimu huu angalia Simba wanavyokuwa na mpira style wanayotumia kufungua uwanja.Mchezaji anapata mpira then wenzake baada wafunguke, mtu anabaki kaganda kwenye nafasi yake kama kawekewa gundi pale.Kama kanoute asingekuwa na kasi mnayosema mechi ya jana asingekuwa na uwezo wa kwenda kufanya shots na bado kurudi kukaba.
 
Hii kazi ya kukaba na kupoza mashambulizi nimemwangalia hata kwenye CHAN yeye hakua akicheza kama kiungo mkabaji.
 
Hili swala la ubora kuletwa na washambuliaji hebu fafanua maana hata haieleweki

Mfano tu ubora wa yule kiungo wa coast Jana ulikua unaletwa na forward yupi?

Ubora wa mukoko msimu ulopita uliletwa na forward yupi pale Yanga?

Mchezaji bora kwenye uwanja huwa anaonekana tu kwa kutimiza majukum yake .
 
asa yanga tumeingiaje apo jamaniiii
 
Kifupi jamaa aliachwa Al Ahly Benghazi . Sasa kama angekua Bora asingeachwa kule kwa ligi kama ya Libya.
 
Kifupi jamaa ni slowly sana na alishwandwa kupata namba alipoenda Libya na aliachwa Al Ahly Benghazi . Sasa kama angekua Bora asingeachwa kule kwa ligi kama ya Libya.
 
Mkiwa mnashambuliwa mnakuwa hampo kwenye shepu nzur yeye kaz yake n kuhold kwanza namba sita wote wako slow mkuuu hawako shapu Kama viungo wengine unamuona matic ata kotei alikuwa slow
Matic naye ni slow ndio maana mourinho hakumpendelea na huwezi kulinganisha kasi yake na huyu Ngongoti Kanoute.
 
Timu ni kila mwanatimu kutimiza wajibu wake uzembe au kutotimiza wajibu kwa baadhi ya wanatimu kunaharibu timu nzima kwa ujumla wake
 
Kanoute ni mmoja tu. Yule wa Simba Day basi.
 
Waiangalie Juventus na Barca kama mfano.
 
Kanoute hamfikii Juma Nyangi wa mtibwa wala hana alichomzidi ndemla
 
Kanoute hafiki hata robo ya uwezo wa baraka gamba majogoro
 
Hata huyo Inonga wasingekuwa naye, maana waliomscout ni Yanga. Simba alikuja akabeba juu kwa juu. Hivyo, inatakiwa Simba ipate Mtaalam wa Scouting ya Wachezaji wenye viwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…