Kuna namna mtu akipata pesa anakuwa na kiburi cha uzima cha hyper pro max

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Majuzi dogo moja gari namba E ya harrier alikuja duka fulani kununua bidhaa.

Sasa alipopaki pembezoni mwa duka ng'ambo ya pili ya bara bara kuna lori kubwa la mzigo, kumaanisha alitengeneza double parking ambayo ilipelekea bara bara kuwa finyu.

Sasa jamaa mmoja wa bajaji ya mizigo akatokea kwa nyuma akipiga honi ili jamaa wa harrier asogee mbele kidogo ili apenye apite ila jamaa wa harrier hata akutikisika. Yani honi zilipigwa hadi jamaa wa bajaji akaja kumlamlamikia .

Cha ajabu jamaa wa bajaji alivyorudi alitegemea atapishwa ila hauwezi amini jamaa aliendelea kuchomeshwa mahindi kama dakika 8-10 hivi huku yule jamaa wa harrier akiwa ame relax amekaa kwenye gari akifanyia huduma ya kuletewa bidhaa.

Sawa watu hawana vitu kama vyako, ila pale eti vitu ndivyo vinavyo determine umwamba wako, yani kisa gari kali mpya namba E unakuta mtu anahisi wewe ni "untouchable", ila reality ni ushamba na sio kila mtu atatetereka na kagari kako, wanatunza tu receipts zako.
 
ana hela ya rangi huyo hajakutana na watu wenye roho mbaya inapigwa msumari mwanzo mwisho mstari mmoja mtakatifu.... ukiwa na gari kali jitahidi uwe mstaarabu sana maana swala la hasara mara nyingi linakua upande wako
 
Issue sio hilo gari wala namba, madereva wa kibongo akili zetu zimefyatuka.. Kuna mwamba pale Tazara, barabara mbele imefunga ila kisa taa zimemruhusu akaenda kuweka semi lake kwenye ile junction akaifunga nafasi yote, upande wa pili taa zinawaka kijani, nyekundu zinarudi tena kijani ila njia imefungwa na semi.

Halafu kuna ndugu zetu wa daladala, anaweza kusimama njiani maksudi ili wenzie wa nyuma wasimpite.. anawalostisha hadi msiokuwemo. Pia wana mchezo kama huyo dereva harrier, mbele kuna nafasi ila anasimama hapo mbele yako na kushusha/ kupakia abiria.

Kuna wale njia yao imefunga, wanafunga na magari yanayokuja na njia inafunga mazima pande zote, hamna inayokuja wala inayokwenda.
 
Majuzi dogo moja gari namba E ya harrier alikuja duka fulani kununua bidhaa.

Sasa alipopaki pembezoni mwa duka ng'ambo ya pili ya bara bara kuna lori kubwa la mzigo, kumaanisha alitengeneza double parking ambayo ilipelekea bara bara kuwa finyu.

Sasa jamaa mmoja wa bajaji ya mizigo akatokea kwa nyuma akipiga honi ili jamaa wa harrier asogee mbele kidogo ili apenye apite ila jamaa wa harrier hata akutikisika. Yani honi zilipigwa hadi jamaa wa bajaji akaja kumlamlamikia .

Cha ajabu jamaa wa bajaji alivyorudi alitegemea atapishwa ila hauwezi amini jamaa aliendelea kuchomeshwa mahindi kama dakika 8-10 hivi huku yule jamaa wa harrier akiwa ame relax amekaa kwenye gari akifanyia huduma ya kuletewa bidhaa.

Sawa watu hawana vitu kama vyako, ila pale eti vitu ndivyo vinavyo determine umwamba wako, yani kisa gari kali mpya namba E unakuta mtu anahisi wewe ni "untouchable", ila reality ni ushamba na sio kila mtu atatetereka na kagari kako, wanatunza tu receipts zako.
Wakati mwingine waweza mchukia mtu tu kwasababu amekuzidi. Kumbe ungechukua + isingekuwa issue maisha yange endelea. Nahii nishida ya wabongo
 
Majuzi dogo moja gari namba E ya harrier alikuja duka fulani kununua bidhaa.

Sasa alipopaki pembezoni mwa duka ng'ambo ya pili ya bara bara kuna lori kubwa la mzigo, kumaanisha alitengeneza double parking ambayo ilipelekea bara bara kuwa finyu.

Sasa jamaa mmoja wa bajaji ya mizigo akatokea kwa nyuma akipiga honi ili jamaa wa harrier asogee mbele kidogo ili apenye apite ila jamaa wa harrier hata akutikisika. Yani honi zilipigwa hadi jamaa wa bajaji akaja kumlamlamikia .

Cha ajabu jamaa wa bajaji alivyorudi alitegemea atapishwa ila hauwezi amini jamaa aliendelea kuchomeshwa mahindi kama dakika 8-10 hivi huku yule jamaa wa harrier akiwa ame relax amekaa kwenye gari akifanyia huduma ya kuletewa bidhaa.

Sawa watu hawana vitu kama vyako, ila pale eti vitu ndivyo vinavyo determine umwamba wako, yani kisa gari kali mpya namba E unakuta mtu anahisi wewe ni "untouchable", ila reality ni ushamba na sio kila mtu atatetereka na kagari kako, wanatunza tu receipts zako.
Ukibahatisha kuishi Bukoba afu ww mgeni,Hivi vituko utaona kawaida
 
Back
Top Bottom