Tetesi: Kuna nchi jirani ambayo magari yake yanapita free bandarini bila kukatwa kodi

Tetesi: Kuna nchi jirani ambayo magari yake yanapita free bandarini bila kukatwa kodi

Wengi tunajua tunavyoumia pale tunapoagiza magari hususani kupitia bandari ya dare es sallam ilivyo ghali na kodi kubwa

Lakini inasemekana kuna nchi jirani ambao kwao ni neema tu kwani wakati sisi tukitozwa bei kubwa wakati gari zetu tulizonunua zikipita bandarini wao wanapitishiwa sawa na bure

Mfano inasemekana gari za rwanda enzi za kikwete zikipita bandarini basi kila gari ilikua inatozwa usd 500 lakini kwa sasa inasemekana wanatozwa usd 150 kwa magari makubwa kama malori na mascania huku magari mengine madogo madogo yakipita bure bandarini

Kama ni kweli ili jambo basi ni jambo baya mno na kutia hasira kuwa nchi yetu imegeuzwa jamvi la wageni kila mtu anafaidi. Kwanini mtanzania aagize gari akatwe makodi huku raia wa nchi jirani anunue gari kama ile ile asikatwe kodi?

Kama haya ni ya kweli bhas ujue tuna kiongozi wa ajabu kuwahi kutokea toka dunia imeumbwa
Kumbe tetesi, ndio hasara ya kukaa vijiweni na kulishana matangazo pori

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtoa mada ni zuzu wa kutupwa toka lini kodi ya mtu wa nchi nyingine akatozwa na Tanzania halafu akitaka kuingiza nchini kwake atatozwa nini ndo maana hata ukitoka south Africa na gari yako ukifika hapa kwetu mpakani utatozwa pia. bandari inahuduma zake za bandari na kodi yake kwa nchi husika na TRA nao wanakodi zao. Mbona malawi na Zambia hamuwalalamikii nao wanatozwa pungufu kuliko sisi punguzeni kusikiliza hadithi za vijiweni fanya utafiti kwanza. nina wasiwasi kwa ulalamishi huu watanzania wengi shule hazitusaidii, tusifuate mkumbo kwa kila kitu mengine tuwe tunayachuja
 
Wengi tunajua tunavyoumia pale tunapoagiza magari hususani kupitia bandari ya dare es sallam ilivyo ghali na kodi kubwa

Lakini inasemekana kuna nchi jirani ambao kwao ni neema tu kwani wakati sisi tukitozwa bei kubwa wakati gari zetu tulizonunua zikipita bandarini wao wanapitishiwa sawa na bure

Mfano inasemekana gari za rwanda enzi za kikwete zikipita bandarini basi kila gari ilikua inatozwa usd 500 lakini kwa sasa inasemekana wanatozwa usd 150 kwa magari makubwa kama malori na mascania huku magari mengine madogo madogo yakipita bure bandarini

Kama ni kweli ili jambo basi ni jambo baya mno na kutia hasira kuwa nchi yetu imegeuzwa jamvi la wageni kila mtu anafaidi. Kwanini mtanzania aagize gari akatwe makodi huku raia wa nchi jirani anunue gari kama ile ile asikatwe kodi?

Kama haya ni ya kweli bhas ujue tuna kiongozi wa ajabu kuwahi kutokea toka dunia imeumbwa
Post zakijinga
 
naona kuna nyumbu wananyumbukia tu bila kujiongeza kuwa mtoa mada kawapotosha , hii inaonesha kuwa ni kweli kuna watz mbumbumbu wengi
 
Kodi ipi unamaanisha??
Kwa taarifa yako hata kwetu Gari za Nchi jirani HAZILIPI KODI, zinapita kama "In Transit-IT) tu. Maana yake huko kwenye nchi zinakoenda zitaenda kutozwa kodi. Sasa zikitozwa na hapa kwetu inakua Double Taxation.

The East African Community Customs Management Act (EACMA) inazungumzia hili.
Walishadanganywa na yule bibi mwenye njaa kule Marekani, wakaona ni point ya kuleta JF. Pole yao.
 
Hakuna kitu kama hicho wakipitisha magari yao wanakatwa excise duty kama kawaida ila Import duty na VAT ndio watakatwa bandarn kwao zikifika, other port charges wanachajiwa kama kawaida usidanganywe.
Pia likisafirishwa kwa kutembea kwa malorry ndio wanakatwa hyo $150 kwa magari madogo hutegemea na cc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha tu mkuu huyu rais wetu ni wa kung'Oa tu ni ajent wa rwanda
Mkuu, jifunze kutafakari kabla ya kusema kitu, unajua maana ya neno "treason" na sheria za nchi zinasemaje kuhusu hili?
 
Back
Top Bottom