Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

"... Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!..."

HAKIKA INAUMA MNO, TENA MNO! NATAMANI KUJUA WATOTO WALIPO, NIKAWACHUKUE WAWE WANANGU WA KUWALEA.
Basi baaasi usilie ndugu acha kulia maana umepiga ukunga hadi simu yangu imevibrate.
 
Kwa mujibu wako ukizaliwa binadamu una pepo.
 
Wanapaswa kumlilia Mungu aisee
Sasa MUNGU awasaidie nini tena kama wameshindwa kutumia akili aliyopatia kujitengenezea maarifa ya kujijenga vema na kuwa na maisha mazuri na sio kuwa wabangaizaji. MUNGU hakuwataka wawe hapo ni matokeo ya namna wao walikuwa wanapanga ratiba zao za kila siku.
 
PEPO LA KUSOMA AF KUKOSA KUAJIRIWA

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Hilo sio pepo ni upumbavu wa serikali ya kijani na raia wasiokuwa na maamuzi na serikali yao. Wewe unaona ni mapepo sababu unatazama hili tatizo la kukosa ajira kwenye individual level.

Ungelitazama katika level ya taifa ungeelewa kuwa haimake sense idadi ya wahitimu wasomi kuongezeka kila mwaka huku nafasi za kazi na taasisi zikiwa zile zile na watu hawastaafu wanang'ang'ania kubakia serikalini.

This means kuna mfumo ambao unakinzana na mahitaji ya uhalisia. Sasa hapo mapepo yanafanyaje huo upepo wao.
 
Pepo wanaozungumzwa kwenye biblia, au wale mapepo waliotolewa na yesu kwenye injili ni malaika wabaya, ni kundi la malaika walioasi na kufukuzwa mbinguni pamoja na shetani.

na wala hayo tunayoita mapepo (mashetani waasi) hawapo kwenye makundi kiivyo kwamba pepo la ngono, pepo la umasikini, pepo la maradhi, pepo la ulevi, pepo la kubeti nk. Ni wapo makundi mawili tu malaika waasi waliofukuzwa mbinguni pamoja na shetani na malaika wema waliobakia mbinguni kwa kumtii Mungu.

Muwe makini mnapotumia biblia kama reference kwani naona mapepo ulivoyacategorize hapa na jinsi unavoyaelezea ni kwa mujibu wa imani ya kiisilamu na sio biblia.
 
Hiki kifungu umekielewa lakini?
[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Kwa sababu ya ukweli kwamba Injili zinasimulia hadithi tofauti juu ya kutoa pepo kutendwa na Yesu, imani imeenea kuwa pepo siku zote ni nguvu hasi au za kishetani, au ni shetani mwenyewe. Walakini, haya hayapaswi kuchanganywa na mfano wa shetani.
 
Idadi wa watu wengi hatumuelewi vizuri Mungu na dini basi tuu. Binadamu tulipewa na Mungu akili na utahi akamaliza haya mambo mengine yote ni matokeo ya matendo yetu wenyewe wala Mungu hausiki kabisa. Watu wanaharibu misitu na vyanzo vya maji afu mwisho tunapigwa na ukame na njaa. eti tunaenda kesha kanisani kumuomba Mungu alete mvua, au tunanyoshea vidole eti tuache dhambi kisa hakuna mvua serious tunashindwa kufundishana na kuwekea sheria kali za kudhibiti mazingira afu tunakuja kumpigia kelele Mungu eti hakuna mvua.

Huo ni mfano tu, ila asilimia kubwa hayo ndio maisha na fikra zilizopo kwenye familia zetu. Tunaona dhahiri kabisa tu kinatakiwa kufanyika hiki na hiki hata kwa jasho na damu ili kuepusha matokeo mabaya, ila tunakaza mafuvu tunaenda kukesha makanisani, kwa waganga, manabii na mitume.
 
Wewe unawakilisha kizazi kilicholishwa kasumba kuwa there is no second chance.

Full kulaani
Full kulaumu
Maisha ni tairi lilanozunguka. Tatizo ni wapi tairi linapita
 
Nimekuelewa mkuu.

Nilichotaka kusema ni hizo nguvu hasi, sio kwamba zipo kwenye makundi mfano kundi la ngono, kundi la ulevi, kundi la uvivu, kundi la umasikini nk. Ila ni kundi moja tu la malaika waasi basi na ambao walishavunjwa vujwa na kumalizwa nguvu na Yesu mwenyewe, hivyo hawana tena ubavu wala nguvu zozote juu ya binadamu kama kabla ya Yesu kuwashinda. Hivyo tukiendelea kuwatupia lawama hawa malaika waasi kwamba ndio wanaoendesha hizo nguvu hasi kwa kuwaona kama wao ndio chanzo cha kila dhambi na matatizo yote yanayomkabili binadamu ma familia zetu basi Yesu hakuna alichokifanya na ni kama hakuwahi kuja kabisa duniani maana shetani na malaika zake bado wanatamba.
 
Wewe unawakilisha kizazi kilicholishwa kasumba kuwa there is no second chance.

Full kulaani
Full kulaumu
Maisha ni tairi lilanozunguka. Tatizo ni wapi tairi linapita
Second chance ipo sio kwa kukesha kanisani na kumuomba Mungu, second chance ipo kwa kutafuta na kufumbua vyanzo vya matatizo yanayotuandama na kupambana navyo kwa kuyarekebisha hata kwa jasho na damu. Nje ya hapo Mungu hana msaada wowote maana sio kazi yake, alisha kuoatia akili na utashi akamaliza. Yanayobakia yote yatakuwa ni matokeo ya matendo ya binadamu mwenyewe either wewe mwenyewe au mwingine. Na ndio mana hata wasio-muelewa Yesu mpaka leo wanawaza Yesu alikuja duniani kumaliza matatizo yote ya mwanadamu na kumfanya aishi bila shida wala tatizo lolote.
 
Je wewe ndo unayeweka masharti ya second chance au ni aliyetuumba ndo huweka masharti?

Usiwe na inda wala ila ndani ya moyo unapokuwa unaangalia haya mambo. Usiwalaumu wahanga bali muombe Mungu yasikukute
 
Nimekubali. Ukishaona historia ya mtu kiroho NI hovyo,kuachaacha wanawake,Mara alizalisha akatelekeza,kimbiaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…