Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Ndiyomaana huwa namwomba sana Mungu kuniepusha na majanga ya kuendekeza vimada kila kona ya nchi maana mengine ndiyo hayo mapepo yenyewe
Dunia ina mambo mengi mazito mkuu, wakati mwingine ni kama mkosi au nuksi yaani unaingia tu kwa mara ya kwanza unakutana na balaa. Lakini nilichojifunza, kabla ya kufanya jambo lolote baya huwa Kuna sauti ya ndani inaonya wazi wazi ila kwa ukaidi na tamaa zetu tunajikuta tumeshaingia kwenye mtego
 
Ni makosa makubwa pia kuamini kuwa ulipoachana nae physically ndo umemaliza.

Fuatilia vizuri ndoto unazoota, Bado Huwa anakujia na mnatenda tendo,

Kuna vinasaba amekuachia vitakavyoenda kuathiri Hadi uzao unakuja BAADAYE.

Ongeza bidii kuhakikisha umekata hizo connection zote zote za KUZIMU, maana watu hao ni vinganganizi sana. Maombi serious ukifanya utafanikiwa.

Ikishindwa, watafute watumishi wa Mungu wa Kweli wakusaidie, Usitende Kwa manabii wa uongo, utapotea zaidi.
 
[emoji1545][emoji817] umeongea kiroho zaidi.. I wish haya masomo ya utambuzi wa kiroho yangekuwa yanafundishwa kwenye taasisi zetu za elimu
Kabisa mkuu,sijui kwa nini elimu ya utambuzi imefichwa mnoo kias kwamba access yake ni ngumu mnoo.

Nasikitika mnoo,imefikia hatua mtu ananzishiwa dawa za schizophrenia kwa kukosa tu mtu wa kunotice kwamba vile anavyo feel ni source of awakening to the highest Consciousness.

Maana dalili za spiritual awakening zinafanana kabisa na yule anaye anza kuumwa kichaa.
 
Sauti hiyo inaitwa WILL au dhamira. Mungu ameiweka ndani ya Kila mtu.

Ukikutana na mtu ukajikuta unakosa Amani naye na hujui sababu, muepuke.
 
Huhitaji kwenda kwa wachungaji mkuu,kuna procedure za kurelease karmic energy ambazo umezibeba kwa kufanya Yoga au Meditation ingawa ni very painful process.

Jifunze maana ya yoga na meditation.
Mshana Jr
 
Hiyo sauti ya ndani ndio sauti ya Mungu na ndio jicho la kiroho huona zaidi ya kuona. Ila ujuaji wa kibinadamu ndio hutupofusha na kututia nta masikioni
 
Kuna picha tulizowahi kupiga pamoja, nilipooa niliendelea kuzihifadhi. Mke wangu akaniambia siyo vizuri kuzihifadhi hizi picha huwa zinaambatana na roho. Basi kwa Imani yangu nikaomba na kuvunja mahusiano yangu na wanawake niliokuwa nao hapo kabla, Kisha nikazichana na kuzitupa hizo picha zote. Mambo ya ajabu ni kwamba hata mke wangu alikuwa akipata ndoto kadhaa kuhusu mwanamke huyu, huyu tu wala si hao wengine niliokuwa nao kabla ya mwanamke huyu na kbla ya kuoa huyu mke wangu. Ndoto za kukutana naye kimwli ni nyingi tu nilikuwa nikiota mpaka nilipochukua hatu ya kumwomba Mungu. Ndiyo maana nawaogopa wanawake na kukaa nao mbali sababu najua kwa sehemu matokeo ya baadaye. Haijalishi ni mzuri au ana mvuto kiasi gani, najua Kuna kilichopo cha ziada nyuma yake.
 
Kama ni hivo basi Yesu inabidi aje Tena. Maana yake pamoja na hadi kusurubiwa msalabani lakini bado shetani anatamba tu.

Sipendi watu wanaohusisha changamoto na Imani. Nyumbani wananiambiaga Nina Pepo la ubishi, na Mimi nawaambia Kwa hiyo nyinyi mna malaika wa kukubalikubali Kila kitu bila logic
 
Mfanya biashara ya ngono anaanzaje kuzaa kirahisi namna hii asimjue mhusika? Labda kama mhusika alimkimbia
Kama ananunuliwa na wateja kadhaa kila siku atajuaje?
Cheki mfano hapa..
 
Ungejielimisha jinsi gani ndoto inatokea kisayansi, ungeanza mwenyewe kujiona ulikuwa mjinga
 

Bro mshana umezungumza kitu cha maana sana. Family background is everything, inaweza kupa picha halisi mtu unae ishi nae mbeleni atakuwaje
 
Uko nondo sana, hongera sana kwa kutupatia madini haya Chifu.
 
Kila jambo ni vema kulipima, hasa mambo nyeti yanayohusu Imani. Changamoto unayoweza kuipata katika kutafuta usahihi ni namna unavyotenga utulivu wa kuisikia sauti ya kweli (sauti ya ndani) kwa sababu wakati mwingine unaweza kujikuta unavutana na mtu aliyeendelea sana kiakili na kiufahamu kuliko wewe, hivyo akawa na hoja zinazoonekana zina nguvu zaidi kuliko hoja zako, ingawaje hoja zake haziwezi kupingana na ukweli unaosikia ndani yako
 
Ni kweli Ke wa kununua wanaweza kumtupia Mtu pepo la ugumba hata kama alitumia kondomu?
 
Watu wengi sana wanapitia haya wasijue sababu ni nini
 
Katika hiyo familia mmoja anaweza kuwa mshirikina na kuwaletea Pepo la kuwamaliza ili yeye mambo yake yaende. Kuna mtu anaishi mjini na starehe zake ila wazazi na ndungu zake wanateseka kijijini. Akienda chap, anawapa wazaze wake pesa kidogo kwa kutumia mkono wa kushoto. Hilo ni pepo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…