Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk
Hivyo
vitu hapo juu karibu vyote
vinaanza katika
ngazi za familia,koo,taifa na bara. Mimi nimejaribu
kufikiri kama ifuatavyo hasa ngazi ya
bara moja na bara
lingine:
a) Umasikini: Afrika inaongoza kwa umasikini mkubwa.
b)Migogoro na mifarakano: Afrika inaongoza.
c)Mikopo na madeni: Afrika inaongoza.
d)Wizi,utapeli,udanganyifu (ufisadi): Afrika tumo
e)Mikosi mbalimbali :Afrika tumo
Swali :Tumelaaniwa??????
Jibu: Hapana, ila tumeacha
kufikiri kwa kutumia
fikra tunduizi na tunatumia
fikra mfu. Kwa kifupi tunatumia majibu
rahisi kwenye maswali
magumu.
Mfano mzuri ni hapo juu, ukitumia
fikra tunduizi kujibu maswali ya hapo juu utagundua kuwa yote ambayo umeyataja yana
sababu na chanzo chake na vilevile yana
majibu na suluhisho yake.
Bara la ulaya baada ya kupitia katika zama za giza hatimaye walipata
mwamko(Renaissance) kwani waliamua kuacha watu wa dini, waganga na washirikina wawaamulie na kuwatatulia
matatizo yao.
Badala yake waliamua kutafuta
kiini cha tatizo husika na
majibu yake kwa
kina kupitia
fikra tunduizi. Mara baada ya huu
mwamko, kilichotokea ni historia mpaka leo!!!!!!!!!!!!
Encyclopedia Britannica
https://www.britannica.com › ... › Philosophical Issues
28 Mar 2023 —
Renaissance, (French: “Rebirth”)
period in
European civilization immediately following the Middle Ages and conventionally held to have been ...
Nb 1: Tuache kujibu majibu rahisi kwenye maswali magumu:
Mfano 1: Kwanini wewe ni masikini????
Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya umasikini kwenye ukoo wenu.
Mfano 2: Kwa nini wewe hujaolewa???
Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya ndoa kwenye ukoo wenu au familia yenu.
Nb 2: Kila tatizo lina chanzo chake na suluhisho lake.
Nb 3: Kufikiri kwa kutumia fikra tunduizi ni njia sahihi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali.
Nb 4: Kazi kuu ya kichwa ni kufikri licha ya kuwa na kazi nyingine ya kubebea masikio!!!!!!!!!!
Ni mtazamo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!