Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kama mwanzo wa mwaka huu nilikuwa na relationship kwa kweli Mwaka unaniendea vby sana hata sijui nijisafishaje.

Ninamjua niliyetoka nae, na kwa kweli sijui ndio yeye mwenye nuksi hii.


QUOTE]Ukiweza tumia chumvi tafadhali kuogea.. Usijaribu kwenda kwa waganga kusafishwa nyota ama kwa manabii na mitume kuuziwa maji na vitu vya upako
 
Asante Mkuu tunaogea au

Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya kwanza
 
Sijui ni pepo gani hili [emoji23]
Mimi ndio maana imani yangu naijenga kupitia kujisomea biblia mimi mwenyewe, kujifunza kusali mwenyewe na si kumuamini sana kiongozi wa dini, ndio maana kukengeuka kwa kiongozi wa dini hakuto nifanya nipate sababu ya kutokwenda kanisani, sababu imani yangu nimeijenga zaidi ktk kumjua Mungu na kumtafuta yy.
 
Mimi ndio maana imani yangu naijenga kupitia kujisomea biblia mimi mwenyewe, kujifunza kusali mwenyewe na si kumuamini sana kiongozi wa dini, ndio maana kukengeuka kwa kiongozi wa dini hakuto nifanya nipate sababu ya kutokwenda kanisani, sababu imani yangu nimeijenga zaidi ktk kumjua Mungu na kumtafuta yy.
Uko sahihi sana!
 
Huwa nawaambia watu kinachoweza kukuangusha mwanaume /mwanamke unapokwenda kuoa /kuolewa ni aina ya familia anayotoka mwanamke/mwanaume wako.

Kama ni watu wa hovyo tegemea ule upuuzi wao utakuja hadi sebuleni kwako. Unless uamue kuwa kauzu na mkeo au mumeo akusapoti muwe kitu kimoja kukataa upuuzi usije katika familia yako unayotengeneza.

Familia huwa ndizo zinaharibu Ndoa na mahusiano sababu ya kuingiliwa na muingiliano wa tamaduni ambazo hazimatch.

Imagine wewe labda unatokea kwenye familia decent, baba mzazi akija anakutembeleeni kisha halali hapo unapoishi sababu ya udogo wa nyumba au mwingine ni maadili yake tu hawezi lala kwenye mji wa watoto sababu ni mwiko. Halafu ukaoe au kuolewa familia za kiswahili ambazo baba na mama mkwe na watoto wao wanaweza kuja sehemu unaishi tena ya chumba na sebule wakajiachia comfortable kabisa. Mkwe analala chumbani au sebuleni. [emoji23][emoji23][emoji23]

So kuna mambo ni ya kuchunguza kwanza tamaduni. Unaweza kutana na binti mzuri sana au kijana mtanashati sana ila familia anayotoka ni hovyo bin vuluvulu.


Acha kabisaaa..... umesema uhalisia wa maisha ya mtaani kabisaaa.

Majuto ni mjukuu.....

Laiti maono yangekuja mapema, isingekuwa hivi ilivyo leo....
 
Pepo la hasira
Pepo la umbea
Pepo la wivu mbaya kila likionacho lataka kuharibu
Pepo la unafiki
Pepo....
 
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk


Hivyo vitu hapo juu karibu vyote vinaanza katika ngazi za familia,koo,taifa na bara. Mimi nimejaribu kufikiri kama ifuatavyo hasa ngazi ya bara moja na bara lingine:

a) Umasikini:
Afrika inaongoza kwa umasikini mkubwa.

b)Migogoro na mifarakano: Afrika inaongoza.

c)Mikopo na madeni: Afrika inaongoza.

d)Wizi,utapeli,udanganyifu (ufisadi): Afrika tumo

e)Mikosi mbalimbali :Afrika tumo

Swali :Tumelaaniwa??????

Jibu: Hapana
, ila tumeacha kufikiri kwa kutumia fikra tunduizi na tunatumia fikra mfu. Kwa kifupi tunatumia majibu rahisi kwenye maswali magumu.

Mfano mzuri ni hapo juu, ukitumia fikra tunduizi kujibu maswali ya hapo juu utagundua kuwa yote ambayo umeyataja yana sababu na chanzo chake na vilevile yana majibu na suluhisho yake.

Bara la ulaya baada ya kupitia katika zama za giza hatimaye walipata mwamko(Renaissance) kwani waliamua kuacha watu wa dini, waganga na washirikina wawaamulie na kuwatatulia matatizo yao.

Badala yake waliamua kutafuta kiini cha tatizo husika na majibu yake kwa kina kupitia fikra tunduizi. Mara baada ya huu mwamko, kilichotokea ni historia mpaka leo!!!!!!!!!!!!


Renaissance | Definition, Meaning, History, Artists, Art, & ...


Encyclopedia Britannica
https://www.britannica.com › ... › Philosophical Issues



28 Mar 2023 — Renaissance, (French: “Rebirth”) period in European civilization immediately following the Middle Ages and conventionally held to have been ...

Nb 1: Tuache kujibu majibu rahisi kwenye maswali magumu:

Mfano 1: Kwanini wewe ni masikini????


Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya umasikini kwenye ukoo wenu.

Mfano 2: Kwa nini wewe hujaolewa???

Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya ndoa kwenye ukoo wenu au familia yenu.

Nb 2: Kila tatizo lina chanzo chake na suluhisho lake.

Nb 3: Kufikiri kwa kutumia fikra tunduizi ni njia sahihi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali.

Nb 4: Kazi kuu ya kichwa ni kufikri licha ya kuwa na kazi nyingine ya kubebea masikio!!!!!!!!!!

Ni mtazamo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kula 5 mkuu. Wewe ni Great Thinker.
 
Matatizo yanayoikumba Nchi yetu pia Kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na maagano ktk NDOA ilofungwa na viongozi wetu pande mbili.

Kuna vipengele vigumu mno ktk hati ya NDOA hiyo vinavyowafunga vizazi na vizazi katika vifungo vya Umaskini na ukondoo.

Sina HAKIKA kama waanzilishi walichagua MKE sahihi.
 
Matatizo yanayoikumba Nchi yetu pia Kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na maagano ktk NDOA ilofungwa na viongozi wetu pande mbili.

Kuna vipengele vigumu mno ktk hati ya NDOA hiyo vinavyowafunga vizazi na vizazi katika vifungo vya Umaskini na ukondoo.

Sina HAKIKA kama waanzilishi walichagua MKE sahihi.
Na ishu za kulinda ndoa kupitia ushirikina
Kulinda cheo kupitia ulozi nk
 
Back
Top Bottom