Kuna rafiki yangu ana changamoto ya kazi msaaidieni ana hali mbaya kiuchumi

Hilo ni janga la taifa tupo wengi hatuna kazi,, na sasa hivi hatuchagui kazi
 
Umejaa ubongo wa kitanzania kwa asilimia zote. Unajua nilichangia kwa njia gani? Mbona unafanya conclusion bila kuuliza? Na hata kama niko ng'ambo, unajuaje kama shughuli nayofanya ningepata nafasi nije? Hili siyo suala la anayetaka, ni suala la kufa na kupona. Hakuna anayelazimisha ila hali ndiyo itakulazimisha. Vinginevyo wacha kulialia. Join ''politely'' basi upate matokeo.
 
Sure, nimejaa ubongo wa kitanzania. Mimi mtanzania.
Mashujaa wa kupigania haki au Uhuru kamili wa kweli anangeacha chochote afanyacho ili arudi kupambana. Hapo tungeita umejitoa kwa hali na mali.
Sasa usitake wenzio wajitoe kiasi usichoweza kujitoa au nduguyo.
Na wao walikuwa na shughuli iliyo wabana.
Lissu alirudi toka Belgium kushiriki kupambana na sasa yupo jela. Yeye na wale waliovunjwa viungo wana haki ya kuwasimanga kwa kejeli walioshindwa kutokea kwenye mapambano.
 
kwa hyo unataka wamshikie bakora samia awape kazi?
 
Nyumbu @ its base! "Justice is never given; it is exacted." — A. Philip Randolph
 
Nahitaji Bint au Kijana wa kutembeza Juice Makole Saba Saba Malipo ni 7,000/= uliza Glass kuanzia 20
Mawasiliano
0678340383

Wahudumu wa Pub Mshahara 100,000/= kula na Kulala juu ya Ofisi
0747668411
 
Nyumbu @ its base! "Justice is never given; it is exacted." — A. Philip Randolph
Next time wakihitajika watu kujitokeza kwenye harakati kama zile za kutetea justice uhudhurie.
Hatutaki pesa na maneno, Lissu angeweza kuchangia pesa tu na kujificha ughaibuni. Uje tudai haki wote kwa pamoja.
 
Achukue fomu VETA nitamlipia ada
Issue sio kwenda VETA anahitaji kazi ajikwamue kiuchumi anakaa kwa rafiki yangu wa kike nae ni mwanachuo ni kwamba ukimlipia Ada kula je yeye hapa anahitaji kazi ili maisha yake yaende mbele
 
Muulize ANAJUA kupika bagia, maandazi, kachori.
Mimi nataka mtu wa kupika tu asubuhi nampa 5000.
Kuuza ni juu yangu yeye akipika aondoke zake nyumbani hata akimaliza kupika saa mbili asubuhi.
Ok sawa nitamuuliza
 
Next time wakihitajika watu kujitokeza kwenye harakati kama zile za kutetea justice uhudhurie.
Hatutaki pesa na maneno, Lissu angeweza kuchangia pesa tu na kujificha ughaibuni. Uje tudai haki wote kwa pamoja.
Siku zote nipo front. Sijawahi kuogopa kudai haki. Najua ubongo wako wa ki-nyumbu unakudanganya kuwa kila mtu ni mwoga kama wewe.
 
Siku zote nipo front. Sijawahi kuogopa kudai haki. Najua ubongo wako wa ki-nyumbu unakudanganya kuwa kila mtu ni mwoga kama wewe.
Nishakuwa front najua jinsi ya kuosha uso na maji kupunguza maumivu ya mabomu ya machozi.
Usinikadirie mkuu.
Ushauri usipende kushambulia watu kwa maneno makali na kejeli.
Mfano kuita watu nyumbu. Huwezi jua mwingine atakurudishia maneno makali pengine atatukana wazazi wako, Sasa utapata faida gani?
Ukinitusi au nidhihaki siyo guarantee nitafuata mawazo yako.
 
Da... unadhani mimi naogopa matusi kwangu au kwa wazazi? Kama matusi yaua mimi nisengekuwapo yakhe! Mkuu nyumbu siyo tusi ila sisi watanzania wengi ni nyumbu. Na wala sidhani kama nalazimisha mtu kukubali nachosema. Nchi ni yetu sote ati, na ikiharibika ni kwa wote. Wengine tunajua madhara ya wanachofanya CCM iwapo wananchi watafikia critical point ndiyo maana tunapiga kelele kwa sababu madhara yake yatatupata sisi sote na kina Samia na watoto watatoroka. Hivi mnaona jinsi kulivyo na unemployment rate kubwa ya vijana na serikali ndiyo kwanza inatoa majibu ya kejeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…