Kuna Range Rover Evoque kutoka China huku

Gari za kichina nzuri sana Sema tuna zi underate ila kwa utabiri zitaendea sana miaka ijayo hapa bongo nimepishana na suv za kichina kama tano
 
Kusema kweli kweneye quality, naogopa gari zao especially hizi zenye specifications kubwa hafu bei unakuta chini ya $20k.

Nawaza sisi watu wa used after ,5 years ukinunua si itakua ineshachakaa sana.
Chinese kwenye suala la ubora hawana muda, wazungu huwa wanazingatia hata details ndogo sana ambapo unaweza kuona hazina umuhimu ila wanazingatia sana.

Mchina anaangalia vya umuhimu tu, vitu ambavyo ni too basic.

Kiukweli mchina hapana, hasa kwa sisi huku Africa wapenda vya bure ndio atatumaliza.
 
Shida soko la africa wanaonunua gari mpya ni wachache sana , wengi ni used na gari mpya ambayo haijatumika kwa bei yake hata ikiwa ni ist wabongo wengi hawatanunua
Mkuu hakuna asiyependa gari zuri ni swala la kipato tuu. Wewe angalia humu JF kutwa wananzengo wana discuss Raum na magari kama hayo. Yote ni used na bei zako ndo hizo. Kifupi, magari mengi yanayokuja kwetu ni dumping tuu, kwa sababu hawana pa kuyatupa. Hata hiyo Raum kuinunua lazima uwe mwanaume kweli kweli. Likely hata kwa pesa ya kustaafu. Ndo maana bongo anayeongoza kununua magari mapya na mazuri ni Nani? You guessed right! Sasa jiulize kwa style hiyo tutafika kweli?

Ndo maana nasema watunga sera wetu wanafeli pakubwa. Uchumi wowote lazima upambane kutengeneza middle class. Bongo middle class yetu ni wanasiasa. Ndo maana hata mwenye PhD yake..ndoto ni ubunge. Ndo maana ukiwapa vyeo wanataka hata wapenzi wao wapate pension za serikali…..

Our problems are deeper than we think.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…