Kuna sehemu yenye joto zaidi ya Ifakara Tanzania?

Moshi mjini napo mpaka maeneo ya Himo na holili kuna joto zaidi ya Dar.
Holili kumekua na joto siku hizi? Nakumbuka miaka ya 1990s tulifika eneo la Mkuu Rombo kumfuta jamaa yetu aliyelazwa Huruma Hospital. Nadhani hapo na Holili ni masafa mafupi tu

Sasa tulilala hostel za Huruma. Baridi lake halikua la kitoto. Mchana huwezi kukaa bila jacket au sweeter zito na usiku huwezi kulala bila blanket
 
Ruaha mbuyuni na Iringa mjini kuna umbali wastani km120 , ila ni climate mbili tofauti kabisa .
 
Hapo Ifakara ni kama chungu kiko jikoni na maji yanachemka kisha mfuniko wameweka mawe joto la mvuke lisitoke.
Ifakara joto na mbuuuu!

Ifakara kuna joto, hapo ni bwawani kisha jua linapapiga halafu kingo za bwawa zinazuia upepo kuingia ndani.

Everyday is Saturday................................😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…