Kuna sehemu yenye joto zaidi ya Ifakara Tanzania?

Kuna sehemu yenye joto zaidi ya Ifakara Tanzania?

Kuna utajiri wa hatari kupitia kilimo cha umwagiliaji,kuna mito miwili inakutana,mto ruaha na mto lukosi,ukienda na mtaji wako wa milioni tano ukalima nyanya unatoboa
Niliwahi fanya mishe flani pale around 2017, ila kiukweli kwa sasa ukipita unaona kabisa mji unakua kwa kiwango cha kuona kabisa hapa watu wanachacharika sana..pana ela pale mahali.
 
Joto la Ifakara si la mchemchezo. Ila kuna sehemu inaitwa RUAHA MBUYUNI (Kilolo) nadhani ni mwisho wa yote kwa joto hata Tanzania.
Lakini mbona wana mto pale wa maji .Sema eneo lile kama lipo blocked upepo haupiti sawa sawa!
 
Tanga Napo Moto unawaka hatari,usiku unaweza pasuka kichwa kwa joto kali
 
Hapa nipo Mvuha Morogoro vijijini muda huu. Jana ilifika 42
Screenshot_2021-11-16-12-20-30-30.jpg
 
Mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi ndio unaogoza kwa joto kwasasa hata Dar inangoja.....!
Mm Niko Moshi mjini hapa nikweli joto lipo ila siyo Kali kama la Dar haya mambo mnakuza tuu, nimekuja Toka juzi naona afazali ya huku Dar ni jehanamu
 
Kuna Sehemu inaitwa MAJI YA CHAI, hii ipo Arusha . Joto lake ni hatari yaani maji yanatiririka kwenye mto huku yanachemka. Unachota maji mtoni unaweka majani na sukari unapata chai. Ndio pakaitwa Maji ya chai yaani ni shida.
 
Back
Top Bottom