Kuna shida gani kwenye matikiti maji ya wakati huu?

Hili n tatizo aisee,mm nahisi kemikali zimezidi lazima hatua zichukuliwe
 

Matikiti ya zamani yalikuwa makavu kama spochi na sukari ya kutosha ila ya sasa kama unakula Tango lililowekwa sukari na chumvi.
 
Yatakuaje na utamu wakati yamefyonza maji mengi kuliko kiwango, kilichotokea kwenye matikiti ndicho kilichotokea kwenye miwa kukosa utamu.
 
Hakuna matunda siku hizi

Ova
Kweli kabisa,siku hizi hasa mjini hatuli matunda yenye virutubisho kamili.
Juzi nilipita maeneo ya Buguruni kuna jamaa wameweka makontena yenye coolers na heaters kwa ajili ya kuivisha ndizi mapem...yaani hata ndizi ikiwa changa inaiva kwa siku mbili.
 
mambo yanabadilika hata wewe enzi hizo haukuwa ivi kama iv leo
 
GMO hizo kwa hali iliopo sasa swala la cancer na figo yatakuwa matatizo ya muda mrefu sana kufikia mwaka 2050
 
Ni matokeo ya kilimo cha kibiashara., mbegu zinazotoa faida mara nyingi huwa zina mapungufu ya ubora.,
Tafuta documentary inaitwa food inc, inaelezea vizuri industrial farming, utaelewa kwa nin matikiti mazuri utaweza kuyaona tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…