Salaam!
Umekuwa ni utamaduni wa watu wa kasikazini hususani Wachaga kwenda mapumzikoni kila mwisho wa mwaka
Nimejaribu kufikiria ni kwanini makabila mengine hayana utamaduni huu mzuri kama wachaga?jibu sahihi bado sijapata ila nimejaribu kuhisi labda ni kwa sababu Wachaga wengi wamesoma?
Au mkoa wa Kilimanjaro upo mbali sana kiasi cha wachaga kushindwa kwenda mara kwa mara?
Lakini nimegundua hata Morogoro na Tanga sio mbali lakini Waluguru na Wasambaa hua hawaendi makwao mwisho wa mwaka so umbali na ukaribu kwangu ni vigezo vilivyokosa nguvu.
Nini siri ya Wachaga na utamaduni huu mzuri wa kwenda mapumzikoni mwisho wa mwaka?
Kwa nini makabila mengine wamekuwa wazito kutekeleza swala hili?
Mjadala upo wazi!