Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwasababu wengi tunakua likizo.
Point nzima ya kwenda likizo ni familia nzima kuwa pamoja na disemba(tofauti na miezi mingine) wengi tunakua kwemye nafasi yakuacha shughuli zetu na kwenda kukutana na wenzetu.
Kama hiyo sio sababu inayokupeleka wewe then sioni ajabu kwamba huelewi kwanini kwetu inaleta maana.
Mwamba ngozi!!!!!!jamani hujapandisha machame, utakutana na mashamba njian yaliyolimwa mahindi kwamstari utafikiri hakuna watu. maliza km kama 8 hivi utaanza kukutana na maghorofa katikati ya kahawa na migomba. hadi ufike machame cottage utakuwa umekwisha sahau kama uko kijijini.
tizama makanisa yanayojenga kijijini hata huku mjini hakufui dafu, anza kanisa la NSHARA, UDURU, NKWARUNGO, NENDA NKUU KISERENI, LYAMUNGO utashangaa sana manake utajiuliza maswali mengi na sio ya miaka ya karibuni la hasha mengine yalijengwa 80's lkn kwa ramani kali na ya kisasa.
kule kwao vijijini ni km town! Kunapendeza, kuna nyumba za nguvu, greenish ya kufa mtu nikienda ukweni kuanzia njia panda ya himo marangu mtoni unapishana na vitu vya kufa mtu! Wenzetu wako mbele sana, katikati ya migomba unakutana na kigorofa mzee dah.
Kusifu wachaga hakunitoi kwenye tamaduni yangu hata siku moja..yani niwe mnafiki wakati watu wanafanya mambo mazuri! Kapimwe iq..