Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

1: Hivi kuna kabila lengine linaloongoza kwa kwenda vijijini kwao mwezi desemba kama wachagga?

2: Ni kwanini kila mwaka mwezi huu desemba, unakuta wachagga wanapeleka magodoro nyumbani(vijijini), yale mwanzo walopeleka huwa yanakuwa yameenda wapi?

3: Ushajiuliza kwanini wachagga wengi na familia zao wanaenda vijinini desemba hii tu?

4: Kama wangekuwa waajiriwa, waajiri gani wangetoa likizo kwa wachagga wote iangukie desemba peke yake?

5: Kwahiyo wachagga wengi(asilimia kubwa) ni wajasiriamali. Hivyo, likizo zao na familia, huwa ni mwezi desemba?

6: Kuna ukweli gani juu ya suala hili la wachagga kusema, ukizaliwa tu mchagga, una elimu ya form4 ya kimaisha. Ukisoma hadi la saba una elimu ya form6 kimaisha. Ukifika form6 una elimu ya shahada ya chuo kikuu kimaisha. Ukiwa na shahada ya elimu, elimu ya maisha una PhD.

Wanasema huitaji kusoma sana, jifunze kutengeneza pesa sana. Ni kweli hili?

Nisaidieni majibu tafadhali.
Wana nyumba za kufikia na hawana uchawi kama makabila mengine kule ni mashindano wengine mukienda kijijini kwenu na gari ndio kwisha tata so acha watanue ili wawe chachu za maendeleo. Na wewe jenga kwenu uone!!!!!!!!!!
 
tuna group yetu fb tupo watu 780 kwanza tunaenda kutoa fungu letu la kumi kwa kituo cha watoto yatima kipo pale vilage tutakesha nao tar 24 then mishemishe zingine just imagine itakavikuwa poa
Weeee Smiley, hamtaki member mpya?
Hiyo imetulia kweli.
 
itadipendi na wewe ni wa ukoo gani sisi ni ukoo wa yuleeeeeeeeee mangi hatupendi uzushi. Ngoja niwasiliane na mod wa iyo kitu nitakupim lizzy
Hahahahha,kwahiyo Smiley mtakataa maombi yangu kisa mi ukoo wangu hauvumi?Come now. . .japo hatuvumi Tuna madaktari wengi pale Kibong'oto hosp so kuweni wazuri tu kabla hamjakosa huduma ikitokea mkatakiwa kwenda pale.
 
hahahahha,kwahiyo smiley mtakataa maombi yangu kisa mi ukoo wangu hauvumi?come now. . .japo hatuvumi tuna madaktari wengi pale kibong'oto hosp so kuweni wazuri tu kabla hamjakosa huduma ikitokea mkatakiwa kwenda pale.
hata sisi tunao yaani kila mahali tupo wee hadi mirembe tuna species
 
raha yake usisubiri kuhadithiwa karibu uchagani upate mbege na machalari
 
Kaka k ni nani mdau? Ulimaanisha mimi?
Mimi ni mchagga bila kuchanganya kabila. Wazazi wote wachagga.

Aiseee mbona unatuaibisha chalii wangu! yani wachagga huwa hatupigi mayowe kiasi hich ati, sisi tunafanya wanayaona wenyewe! wachagga hatujisifu sifu tunafanya vitu watu ndiyo wanatusie chalii wangu. Usirudie tena wasije wakakuita ISEMBO
 
Dah!!!hii sijui ilinipiataje?
Hapa nishamalizana na mkolon kanipa kazi za mwezi mzima nizimalize kabla ya tar 22 ili 23/12 mwendo mdundo,
Kituo cha kwanza kiborilon mwisho wa shuhuli mail sita,
Wacha kbs,najiandaa kufunja kibubu tar 20 nikifka huko ni matumisi tu kwa kwenda mbe.......mbele kweliii!!!
Euwiiiiii,yesu na maria,kutakuwa na rahaje!!!
 
dah..we acha tu, ni raha kwenda lakini kuanzia january ukiangalia account unaweza kulia!!

teh teh teh teh..! kwa yooote hongereni ila kwa hili poleeeni..! ila nasikia kwa wale wanao kaa tanga hua hawaendi bwana nasikia mijimama ya tanga ni balaaaa buwana weeewe hhhehehehehehhheheeeeeee uuuuuwiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom