Kuna Siri gani katika hili mbona wanaume wanakuwa sana kuliko wanawake.

Tuliza akili kwa kufanya utafiti mdogo jadidifu kulingana na umri anaofariki nao mtu na si mahusiano ya mke na mume au baba, mama au babu na bibi.

Ulitakiwa utueleze idadi ya wanaume na idadi ya wanawake waliozaliwa siku moja, ni jinsia gani iliyotangulia kufa wengi kabla ya wengine.

Uelewe maisha yapo kimfumo wa "first in, first out", anayetangulia kuzaliwa ndiye anayetangulia kudanja, usiyahesabu ya ajali.

Sasa kwa mantiki hii wanaume wengi huoa wenza wenye umri mdogo, sasa hapo unategemea nani aanze kuvuta?

Pia "life expectancy" ya wanawake ni ndefu kuliko ya wanaume, sazingine kutokana na mazingira ya kimaisha ya kila siku.

Mambo ni mengi ya kuangalia hapo ili kuweza kupata jibu yakinifu, vinginevyo utabakia na dhana isiyo na ukweli.
Ni kweli karibu duniani kote wanawake huishi maisha marefu kuliko wanaume japo kwenye baadhi ya nchi tofauti ni ndogo. Kuna sababu za kibayolojia na za kimazingira/kitamaduni. Actually hata kwa wanyama wengi mbali na binadamu hali ni ile ile: madume hufa mapema [emoji51].

Huku kwetu nadhani sababu zifuatazo zinachangia:

1. Wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuendekeza tabia hatarishi mfano uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupindukia; na hata madawa ya kulevya.

2. Wanaume pia wana tabia ya kubweteka. Wao ni kula tu na kubweteka na hata kwenda kunywa pombe huku wanawake wakifanya kazi zote. Hii inawasaidia sana wanawake kimwili na hata kisaikolojia.

3. Kibayolojia mafuta ya mwilini ya mwanaume huwa yamejipenyeza mpaka kwenye viungo muhimu kama moyo, ini n.k. Hali hii ni hatarishi kwa viungo hivyo muhimu. Kwa wanawake hata akiwa mnene mafuta mengi yanabakia kwenye ngozi, hips, mapaja na matakoni bila kuathiri viungo vyake muhimu.

4. Wanaume pia ndiyo hufanya kazi hatari na zenye kuhatarisha maisha kuliko wanawake.

5. Wanaume pia wana tabia ya kutojali afya zao. Yaani mpaka akaende hospitali ni kweli anaumwa na mara nyingi ugonjwa unakuwa umeshatamalaki. Ni ngumu sana kwa mwanaume kwenda kufanya check up ya kawaida tu kuona viungo vyake muhimu vinavyofanya kazi. Vifo vingi vingeweza kuepukwa kama wanaume wangejua BP yao, sukari pamoja na kiwango cha lehemu (cholesterol). Viwango vya juu vya BP na lehemu ndiyo visababishi vikuu vya mishtuko ya moyo (heart attacks) na kiharusi (stroke). Vyote vinaweza kudhibitiwa kwa dawa au kubadili mfumo wa maisha kabla havijaleta madhara.

6. Mwanaume pia ana majukumu mengi sana na wengi huwa na stresi kwa muda mrefu. Pia hawana tabia ya kushea mambo yao mazito na watu wengine. Matokeo yake wengi wanakuwa na kiwango kikubwa ya Cortisol. Hii ndiyo homoni inayohusika na stress na japo ina kazi nyingi nzuri mwilini, ikitolewa kwa wingi na kukaa kwenye damu kwa muda mrefu ina madhara makubwa ikiwemo kudumaza immune system, kuharibu mfumo wa umeng'enyaji chakula na kufanya mishipa ya damu kukakamaa.

7....

Screenshot_20220416-085144_Chrome.jpg
Screenshot_20220416-085513_Chrome.jpg
 
Wadau naomba mwenye elimu katika hili mbona wanaume wengi wanawahi kufariki kuliko kina mama yaaani ata hospital utakuta bibi au mama kampeleka hospital babu au baba lakini mara chache sanaaa kumkuta babu au baba kampeleka bibi au mama.na mara nyingi babu na baba ndio wanatangulia kuondoka dunia hii sijui imekaaje....
Au ndio maana neno mjane lipo kwa mwanamke tu hakuna mjane mwanaume?????
Hadi leo hii huna jibu? Aisee kama wewe ni me jiandae kuzikwa mapema.
 
Na hapa Me huwa tunapoteza sana Kinga ya mwili baada ya kufika kileleni sababu kuna baadhi ya wadudu ambao ni Kinga ya miili hufa na kupunguza ulinzi wa afya kadri siku zinavyosonga.
Na usipo to....ba una hatari ya kupata tezi dume/prostate cancer na kuchanganyikiwa juu.
 
Ni kweli karibu duniani kote wanawake huishi maisha marefu kuliko wanaume japo kwenye baadhi ya nchi tofauti ni ndogo. Kuna sababu za kibayolojia na za kimazingira/kitamaduni. Actually hata kwa wanyama wengi mbali na binadamu hali ni ile ile: madume hufa mapema [emoji51].

Huku kwetu nadhani sababu zifuatazo zinachangia:

1. Wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuendekeza tabia hatarishi mfano uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupindukia; na hata madawa ya kulevya.

2. Wanaume pia wana tabia ya kubweteka. Wao ni kula tu na kubweteka na hata kwenda kunywa pombe huku wanawake wakifanya kazi zote. Hii inawasaidia sana wanawake kimwili na hata kisaikolojia.

3. Kibayolojia mafuta ya mwilini ya mwanaume huwa yamejipenyeza mpaka kwenye viungo muhimu kama moyo, ini n.k. Hali hii ni hatarishi kwa viungo hivyo muhimu. Kwa wanawake hata akiwa mnene mafuta mengi yanabakia kwenye ngozi, hips, mapaja na matakoni bila kuathiri viungo vyake muhimu.

4. Wanaume pia ndiyo hufanya kazi hatari na zenye kuhatarisha maisha kuliko wanawake.

5. Wanaume pia wana tabia ya kutojali afya zao. Yaani mpaka akaende hospitali ni kweli anaumwa na mara nyingi ugonjwa unakuwa umeshatamalaki. Ni ngumu sana kwa mwanaume kwenda kufanya check up ya kawaida tu kuona viungo vyake muhimu vinavyofanya kazi. Vifo vingi vingeweza kuepukwa kama wanaume wangejua BP yao, sukari pamoja na kiwango cha lehemu (cholesterol). Viwango vya juu vya BP na lehemu ndiyo visababishi vikuu vya mishtuko ya moyo (heart attacks) na kiharusi (stroke). Vyote vinaweza kudhibitiwa kwa dawa au kubadili mfumo wa maisha kabla havijaleta madhara.

6. Mwanaume pia ana majukumu mengi sana na wengi huwa na stresi kwa muda mrefu. Pia hawana tabia ya kushea mambo yao mazito na watu wengine. Matokeo yake wengi wanakuwa na kiwango kikubwa ya Cortisol. Hii ndiyo homoni inayohusika na stress na japo ina kazi nyingi nzuri mwilini, ikitolewa kwa wingi na kukaa kwenye damu kwa muda mrefu ina madhara makubwa ikiwemo kudumaza immune system, kuharibu mfumo wa umeng'enyaji chakula na kufanya mishipa ya damu kukakamaa.

7....

View attachment 2189712View attachment 2189713
Pia nature inataka hivyo, imagine msituni madume wawe wengi kuliko majike Kwa jinsi Huwa yanapigana ni noma Sana..
 
Tuna mambo mengi sana, yanayosababishwa na hao wanawake...
 
Haya maswali ya uhai na kifo, ngoja tumuulize Maulana ndiye mwenye majibu sahihi
 
Swala la Kiroho zaidi. Vita kubwa ipo katika uzao wa kiume. Maana mwanaume ndio mbegu, ndio kizazi. Bila mwanaume hakuna mbegu, hakuna kizazi.

Ili kuharibu uzao/kizazi lazima uharibu wanaume. Maapizo vitabu vya dini Wali laani na kuua wanaume wote au watoto wote wa kiume.. Kwa nini? Ni kudhoofisha au kuangamiza kizazi...

Sasa hivi wanaume wanapigwa vita za kidigitali, Sio Kwa bunduki na upanga Tena.. Ni hatari kuwa na role models na public personality kwenye TV au Radios ambao Kuna utata wa jinsi na mahusiano Yao. Tunaendelea kupata kizazi dhaifu na lege lege.. Mwishowe wata perish kabisa maana uzazi utakoma maana mbegu/wanaume watakuwa hawapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naomba mwenye elimu katika hili mbona wanaume wengi wanawahi kufariki kuliko kina mama yaaani ata hospital utakuta bibi au mama kampeleka hospital babu au baba lakini mara chache sanaaa kumkuta babu au baba kampeleka bibi au mama.na mara nyingi babu na baba ndio wanatangulia kuondoka dunia hii sijui imekaaje....
Au ndio maana neno mjane lipo kwa mwanamke tu hakuna mjane mwanaume?????
Tuna mengi sana moyoni ambayo yanatuua taratibu
 
Wadau naomba mwenye elimu katika hili mbona wanaume wengi wanawahi kufariki kuliko kina mama yaaani ata hospital utakuta bibi au mama kampeleka hospital babu au baba lakini mara chache sanaaa kumkuta babu au baba kampeleka bibi au mama.na mara nyingi babu na baba ndio wanatangulia kuondoka dunia hii sijui imekaaje....
Au ndio maana neno mjane lipo kwa mwanamke tu hakuna mjane mwanaume?????
Kilichonileta kwenye uzi huu ni makosa yako ya kuandika tittle
 
Back
Top Bottom