kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tanzania hakuna timu tajiri, timu nyingi kama sio zote hazina misuli ya fedha za kusajili wachezaji wazuri sana na mabenchi ya ufundi class ya juu. Timu nyingi zinashindwa kuwalipa makocha na wachezaji signing fees zao na mishahara kwa wakati, wachezaji hawana bima na hazina viwanja vyao wenyewe. Kwa ujumla timu zetu zinaendeshwa kwa kubangaiza huku na kule; kwa maneno ya kimpira timu zetu ni feeder clubs kwa timu za kanda nyingine Afrika kutokana na umaskini wao.
Kwanini ni rahisi mno timu zetu kwenda kuweka kambi nje ya nchi lakini ni vigumu kusajili wachezaji wazuri, kulipa mishahara mikubwa ya wachezaji na benchi la ufundi au kujenga uwanja? Majibu ni mengi sana, mojawapo ya majibu hayo ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati timu kwenda pre-season za nje ya nchi na sababu za mtu kukubali kuidhamini timu.
Sina ushahidi kamili, lakini pre-season hizi za hivi zina uhusiano mkubwa na biashara za magendo (smuggling), madawa ya kulevya au ukwepaji ushuru kwa kutumia jina la timu, wachezaji na benchi la ufundi. Akili ya kawaida tu haiwezi kuamini kwamba timu zetu zina fedha nyingi za kwenda kuweka kambi nje nchi lakini hazina fedha za kusajili wachezaji wazuri wa kuleta mataji.
Jeshi la uhamiaji na wadau wengine hebu tegeni mitego ya kunasa matunda ya pre-season za nje ya nchi kwa timu mbovu kabisa uwanjani na zinazolalamika kuwa hazina pesa za kulipa wachezaji, makocha, kusajili na kujenga viwanja vyao. Mnaweza kugundua chocholo za uovu kwenye hizi safari.