Kuna siri gani kwenda Pre-Season nje ya nchi kwa timu masikini?

Kuna siri gani kwenda Pre-Season nje ya nchi kwa timu masikini?

Pre season zote dunia ni psychological issues hakuna team duniani hasa team zinabaki kwenye nchi yake fuatilia team zote kubwa ulaya sasa hivi ziko wapi kiufupi pre season ni kuweka sawa psychology ya mchezaji ambayo ina nafasi kubwa kwenye performance ya mchezaji.
 
Sitaki kuamini hizi timu ni maskini.
Kama ni kweli basi ni suala la viongozi wabovu wasio na maono tulionao.
Mfano ukiangalia uhitaji wa kadi za uanachama kwa timu kama Simba ni mkubwa sana.Lakini hakuna kiongozi anayependa timu iwe na wanachama wengi ndio maana kuna ugumu wa kupata kadi na utaratibu haueleweki
Viongozi Simba hawataki wanachama wengi bali wanataka mashabiki wengi oyaoya. Niliwauliza kwanini, wakajibu eti kwakuwa Kuna hisa hivyo kama wanachama wakiwa wengi dividend itapungua, yaani faida kwa wanahisa itapungua. Kwa maana nyingine wanataka wanachama wabaki haohao milele kwaajili ya uroho wa pesa. Wanamtegemea mo afanye kila kitu. Ndio maana mo anawazingua kila mara, ni nyani wala mabibo.
 
Pre season zote dunia ni psychological issues hakuna team duniani hasa team zinabaki kwenye nchi yake fuatilia team zote kubwa ulaya sasa hivi ziko wapi kiufupi pre season ni kuweka sawa psychology ya mchezaji ambayo ina nafasi kubwa kwenye performance ya mchezaji.
Pre season unakwenda kutafuta vitu vingi kwa wakati mmoja. Lakini kikubwa zaidi ni kutafuta muunganiko wa wachezaji kuwa timu moja. Huo muunganiko utaupataje kama wachezaji wengine hawako kambini? Lakini je, hali ya hewa ya Kambi ni sawa na hali ya hewa ya mashindano unayoyaendea? lakini je viwanja vya preseason ni sawa na vile vya nangwanda? Je, unao wachezaji wageni wanaohitaji adaptation ya hali ya mambo kwenye nchi??
 
Kaka hakuna logic ya timu zetu "maskini" kuweka kambi nchi za nje, kuhusu
1. hali ya hewa: Tanzania ina aina zote za hali ya hewa za dunia hii (DSM, Bagamoyo, Makambako, Mufindi, Arusha, Karatu, Shinyanga, Kagera, Mbeya, Handeni,nk). Hata hivyo hali ya hewa ya preseason lazima ifanane na ile ya mashindano (ligi)

2. Viwanja vizuri: Preseason lazima ifanyike kweye viwanja vinavyofananafanana na viwanja vitakavyotumika kwenye mashindano (ligi husika). Unaenda ulaya kwenye viwanja vizuri halafu mechi utacheza manungu na majaliwa stadium wapi na wapi.

3. Swala la mazoezi ni swala endelevu kwenye msimu wote. Huwezi kwenda kufanya mazoezi kwenye vifaa ambavyo hutakuwanavyo wakati wa mashindano msimu mzima, sio kweli. Yaani ufanye mazoezi kule Uswis kwa wiki 3 tu yatakayodumu kwa mchezaji kwa msimu mzima kule tanzania, hii sio kweli.
4. Kuwa na fedha: Hii nayo sio kweli, timu zetu zinashindwa kusajili wachezaji wazuri sokoni kwasababu hazina fedha na kuwanunua na kuwalipa mishahara.

TRA, Uhamiaji na wadau wengine:
1. Kagueni kwelikweli mifuko na mabegi ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wakati wa kwenda na kurudi preseason nje ya nchi.
2. Tikiseni mipira yooote wanayoenda na kurudi nayo safarini, msione haya kuipasua randomly michache kati ya hiyo.

3. timu na wachezaji wafuate taratibu zote sa kusafiri nje ya nchi.
Nakazia hapa

Mamlaka husika zifanyie kazi hii kitu
 
Utajiri wa dewj na gulamali families ukiuchunguza saaaaaana vizuri wana sababu za kuwa wafadhili wa club hizi. Sehemu kubwa ya mtaji huenda ulitokana na timu hizi. Kwenye mabegi, kwenye mpira, kwenye makontena ya zawadi na vifaa vya timu huenda Kuna mambo mambo!!!
 
Kama kusafiri tu kwenye mechi za Caf mnapanda ndege za abiria na mnakwenda kimafungu ndo mtaweza kwenda pre season nje ya nchi mkae wiki tatu?
Simba huwa wanaoanda Private jet kwenye mechi za Cuf?
 
Eti timu zetu!,, zipi hizo ?.. lini utopolo mlikwenda nje ya nchi mkafanya pre season ukiachana na ile mliyolipiwa na waarabu,, kila mwaka excuse ile ile eti mda hautoshi, mlikuwa hamjui kuwa kuna pre season kabla ya msimu mpya kuanza ?..

Ifike wakati utopolo muelewe kuwa simba sio level yenu, kwa Tanzania ni Azam na Simba tu zenye misuli ya kifedha na uwezo wa kufanya watakalo,, hatuwezi kuwa sawa na timu inayotegemea kuuza magodoro iweze kujiendesha.. nadhani kwa sasa mmeelewa tuliposema bajeti yetu ya msimu ujao ni B23 tulikua tuna maanisha.

IKIUMA CHOMOA
We mjinga sikiliza timu za Ulaya huwa wanaweka kambi lets say Man U Anaenda China au Marekani ni kwa sababu ya Biashara na si vinginevyo wanaenda kutaga timu kupata mashabiki wapya ili wapige pesa kwenye jezi. Sasa Simba kunabBiashara anafanya Uturuki? Tunaiga hadi ujinga
 
Ngada je?
 
Nakazia hapa

Mamlaka husika zifanyie kazi hii kitu
Tumepigwa sana, unashangaa vijana wetu wamelewa TU, unga umepitia wapi kuingizwa nchini haijulikani, kumbee uliingizwa wa kutosha wakati wa preseason!!!!? Whistle browsers hawauawi
 
Tanzania hakuna timu tajiri, timu nyingi kama sio zote hazina misuli ya fedha za kusajili wachezaji wazuri sana na mabenchi ya ufundi class ya juu. Timu nyingi zinashindwa kuwalipa makocha na wachezaji signing fees zao na mishahara kwa wakati, wachezaji hawana bima na hazina viwanja vyao wenyewe. Kwa ujumla timu zetu zinaendeshwa kwa kubangaiza huku na kule; kwa maneno ya kimpira timu zetu ni feeder clubs kwa timu za kanda nyingine Afrika kutokana na umaskini wao.

Kwanini ni rahisi mno timu zetu kwenda kuweka kambi nje ya nchi lakini ni vigumu kusajili wachezaji wazuri, kulipa mishahara mikubwa ya wachezaji na benchi la ufundi au kujenga uwanja? Majibu ni mengi sana, mojawapo ya majibu hayo ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati timu kwenda pre-season za nje ya nchi na sababu za mtu kukubali kuidhamini timu. Sina ushahidi kamili, lakini pre-season hizi za hivi zina uhusiano mkubwa na biashara za magendo (smuggling), madawa ya kulevya au ukwepaji ushuru kwa kutumia jina la timu, wachezaji na benchi la ufundi. Akili ya kawaida tu haiwezi kuamini kwamba timu zetu zina fedha nyingi za kwenda kuweka kambi nje nchi lakini hazina fedha za kusajili wachezaji wazuri wa kuleta mataji.

Jeshi la uhamiaji na wadau wengine hebu tegeni mitego ya kunasa matunda ya pre-season za nje ya nchi kwa timu mbovu kabisa uwanjani na zinazolalamika kuwa hazina pesa za kulipa wachezaji, makocha, kusajili na kujenga viwanja vyao. Mnaweza kugundua chocholo za uovu kwenye hizi safari.
Hapa ndio navishangaaga HV vilabu vyetu kusafiri kwenda uturuki mbna hatuwasiki mamelod

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pre season unakwenda kutafuta vitu vingi kwa wakati mmoja. Lakini kikubwa zaidi ni kutafuta muunganiko wa wachezaji kuwa timu moja. Huo muunganiko utaupataje kama wachezaji wengine hawako kambini? Lakini je, hali ya hewa ya Kambi ni sawa na hali ya hewa ya mashindano unayoyaendea? lakini je viwanja vya preseason ni sawa na vile vya nangwanda? Je, unao wachezaji wageni wanaohitaji adaptation ya hali ya mambo kwenye nchi??
Kwani shida iko wapi mkuu yaani kwasababu yanga wapo avic town kwa hyo kila mtu abaki avic town kisa alibahatisha final.
 
Kwani shida iko wapi mkuu yaani kwasababu yanga wapo avic town kwa hyo kila mtu abaki avic town kisa alibahatisha final.
Hakuna association kati ya kambi ya preseason ilipo na mafanikio kwenye mashindano. Tumevamia mtumbwi wa vibwengo TU sisi kwenda ng'ambo preseason. Sisi ni kwaajili ya ngada lakini wenzetu ni kwaajili ya marketing na business. Wao preseason inawezakuwa ni sehemu ya udhamini.
 
Pre season zote dunia ni psychological issues hakuna team duniani hasa team zinabaki kwenye nchi yake fuatilia team zote kubwa ulaya sasa hivi ziko wapi kiufupi pre season ni kuweka sawa psychology ya mchezaji ambayo ina nafasi kubwa kwenye performance ya mchezaji.
Ona mwenyewe!! kocha yuko Brazil, wachezaji nusu Uturuki na nusu Dar es salaam, Tz. Hiyo ni pre-season ya wapi? vuluvulu fc. Kuna jambo muhimu hapo ambalo ni zaidi ya preseason, vyombo husika fanyeni kazi yenu kikamilifu, maana hakuna pre-season ya hivi duniani. Kocha Mkuu hayuko kambini, wachezaji muhimu kama Chama. Sakho, Baleke, Onana, Ngoma na wengine hawako kwenye kambi ya preseason sasa preseason wanafanya nini? Huo muunganiko wa timu utafanywa na nani kwa wachezaji gani?
 
Una hoja ila ushabiki umetuharibu akili, ukitoa hoja kinzani na simba basi wewe yanga, ukitoa tofauti na yanga basi wewe simba.
 
Umejenga hoja nzuri sana mkuu, Uandishi wako pia ni mzuri.

Natamani tungekuwa na WATU wa aina yako kwa wingi hapa jukwaani ukiondoa wale WAJINGA wanaojaza Seva za Jamii forum.

Nikienda kwenye hoja Moja kwa Moja
Timu zinahusishaa na ubebaji WA magendo kama vile madawa ya KULEVYA, Heroin Cocain Bangi nk.

Mara nyingi Timu zimekuwa hasikaguliwi uwanja WA Ndege wameamua kutumia huo mwanya kubebe PODA.

Wanasingizia
1. Hali ya HEWA nzuri..
2. Uwepo wa viwanja vizuri vya Mazoezi.
3. Kuwepo kwa Facilities zote za mazoezi.
4.kuwa na Fedha kwa VILABU nk

ZILAANIWE TIMU ZOTE ZENYE TABIA ZA KISHENZI KAMA HIZI.

MAMLAKA AMKENI.
Wale wanaobaki avic town ,hawana mchongo huo?
 
Tanzania hakuna timu tajiri, timu nyingi kama sio zote hazina misuli ya fedha za kusajili wachezaji wazuri sana na mabenchi ya ufundi class ya juu. Timu nyingi zinashindwa kuwalipa makocha na wachezaji signing fees zao na mishahara kwa wakati, wachezaji hawana bima na hazina viwanja vyao wenyewe. Kwa ujumla timu zetu zinaendeshwa kwa kubangaiza huku na kule; kwa maneno ya kimpira timu zetu ni feeder clubs kwa timu za kanda nyingine Afrika kutokana na umaskini wao.

Kwanini ni rahisi mno timu zetu kwenda kuweka kambi nje ya nchi lakini ni vigumu kusajili wachezaji wazuri, kulipa mishahara mikubwa ya wachezaji na benchi la ufundi au kujenga uwanja? Majibu ni mengi sana, mojawapo ya majibu hayo ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati timu kwenda pre-season za nje ya nchi na sababu za mtu kukubali kuidhamini timu.

Sina ushahidi kamili, lakini pre-season hizi za hivi zina uhusiano mkubwa na biashara za magendo (smuggling), madawa ya kulevya au ukwepaji ushuru kwa kutumia jina la timu, wachezaji na benchi la ufundi. Akili ya kawaida tu haiwezi kuamini kwamba timu zetu zina fedha nyingi za kwenda kuweka kambi nje nchi lakini hazina fedha za kusajili wachezaji wazuri wa kuleta mataji.

Jeshi la uhamiaji na wadau wengine hebu tegeni mitego ya kunasa matunda ya pre-season za nje ya nchi kwa timu mbovu kabisa uwanjani na zinazolalamika kuwa hazina pesa za kulipa wachezaji, makocha, kusajili na kujenga viwanja vyao. Mnaweza kugundua chocholo za uovu kwenye hizi safari.
Umeeleweka vzr sana,tuliwahi kuhoji hili sehemu flani
 
Back
Top Bottom