Kaka hakuna logic ya timu zetu "maskini" kuweka kambi nchi za nje, kuhusu
1. hali ya hewa: Tanzania ina aina zote za hali ya hewa za dunia hii (DSM, Bagamoyo, Makambako, Mufindi, Arusha, Karatu, Shinyanga, Kagera, Mbeya, Handeni,nk). Hata hivyo hali ya hewa ya preseason lazima ifanane na ile ya mashindano (ligi)
2. Viwanja vizuri: Preseason lazima ifanyike kweye viwanja vinavyofananafanana na viwanja vitakavyotumika kwenye mashindano (ligi husika). Unaenda ulaya kwenye viwanja vizuri halafu mechi utacheza manungu na majaliwa stadium wapi na wapi.
3. Swala la mazoezi ni swala endelevu kwenye msimu wote. Huwezi kwenda kufanya mazoezi kwenye vifaa ambavyo hutakuwanavyo wakati wa mashindano msimu mzima, sio kweli. Yaani ufanye mazoezi kule Uswis kwa wiki 3 tu yatakayodumu kwa mchezaji kwa msimu mzima kule tanzania, hii sio kweli.
4. Kuwa na fedha: Hii nayo sio kweli, timu zetu zinashindwa kusajili wachezaji wazuri sokoni kwasababu hazina fedha na kuwanunua na kuwalipa mishahara.
TRA, Uhamiaji na wadau wengine:
1. Kagueni kwelikweli mifuko na mabegi ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wakati wa kwenda na kurudi preseason nje ya nchi.
2. Tikiseni mipira yooote wanayoenda na kurudi nayo safarini, msione haya kuipasua randomly michache kati ya hiyo.
3. timu na wachezaji wafuate taratibu zote sa kusafiri nje ya nchi.