Kuna siri gani kwenda Pre-Season nje ya nchi kwa timu masikini?

Ingekuwa ndo Yanga anakwenda Uturuki kufanya pre season ungeandika yote haya ??
 
Ingekuwa ndo yanga anakwenda uturuki kufanya pre season ungeandika yote haya ??
Ningeandika pia, maana najua yanga haina hata uwanja wa kupigia pushup wachezaji, lakini pia ina wachezaji wapya wa kigeni ambao ingekuwa fursa yao kuja nchini mapema na kuzoea hali ya hewa, vyakula na viwanja kabla ya ligi kuanza.
 
Timu ilikwenda Dubai na Robertihno, je matokeo yake baada ya kurudi tz mnayajua? mnayakumbuka?
 
Hizi timu mbili Ni dili kwa magabachori Ni mwendo Wa utakatishaji fedha haramu ukienda undercover kuna madudu we usione juu tuu
 
Unaonaje kama hiyo pesa ndogo unayosema ingewekezwa kwenye ununuzi wa matofali ya kujenga uwanja wa club au hostel za wachezaji au ununuzi wa vifaa vya kisasa kwenye gym za timu? wasiwasi ndo akili.
Unawapangia wewe ni nani? Siyo hata mshabiki wa timu, achilia mbali kuwa mwanachama ila unataka wafanya mambo kulingana na matakwa yako. Hii ni ajabu sana.
 
Kweli mkuu na waturuki wanapenda Bangi si mchezooo.
 
nyie mnasafirisha ngada za mhindi tu hamna lolote...
 
Unawapangia wewe ni nani? Siyo hata mshabiki wa timu, achilia mbali kuwa mwanachama ila unataka wafanya mambo kulingana na matakwa yako. Hii ni ajabu sana.
kwahiyo ni timu ya mazombie? tunaandika haya kwakuwa huenda dawa za kulenya kwa vijana wetu zinapitia mlango huu, na madini yetu na pembe za faru wetu vikaondokea mlango huuhuu. Wasiwasi ndio akili bro, nothing more nothing less.
 
Kweli mkuu na waturuki wanapenda Bangi si mchezooo.
Waturuki wako karibu na Afghanistan, Pakistan, nk ziliko ngada. Wasiwasi ndio akili. Kwanini timu haziendi nchi kama Israel na nyingine ambazo ngada hazipatikani kwa urahisi? Kwanini ni uturuki, dubai, tunisia, morocco, brazil, Colombia, nk?
 
Hizi ni dili za watu kujipatia marupu rupu ya ziada koo haliwezi kukwepeka, watasema hawana hela ya kumsajili mchezaji wa milion 500 lakini wanaenda pre season ya milion 700.

Kumbe kuna 10% zao kwenye pre season ni tofauti na usajili ambapo hawana 10%
 
Hii safari ya simba ime wauma sana, hususani baada ya kutangaziwa kuwa kikundi chao cha masela kitabakia kigamboni
Msimu uliuopita Yanga alinangwa hivi hivi kwa kubakia Kigamboni wakati Simba akienda nchi zaidi ya mbili katika pre season lakini mwisho wa siku aliyebakia Kigamboni ndiye aliyebakia hadi fainali mashindano ya CAFCC, bingwa wa NBC premier league, na bingwa wa Azam Federation cup. Endeleeni kujivunia pre season tu
 
Mwisho wa siku wanasajili akina Akpan, sawadogo, okwa, dejan kwa bei ndogo kabisa na kumpa Ahmed Ally awapake mafuta wauzike kwa mashabiki.
 
kwahiyo ni timu ya mazombie? tunaandika haya kwakuwa huenda dawa za kulenya kwa vijana wetu zinapitia mlango huu, na madini yetu na pembe za faru wetu vikaondokea mlango huuhuu. Wasiwasi ndio akili bro, nothing more nothing less.
Kwa hiyo umekaa hapo unahofu Shomari Kapombe anatorosha pembe za ndovu na hayo yote unaamini yanasubiri wakati wa pre-season tu ila msimu mzima timu zinaposafiri ikiwemo Yanga hauna wasiwasi? Wewe hauna wasiwasi, bali una upungufu wa maarifa ukichanganya na wivu.
 
Sina hakika na mwendelezo wa hili baada ya kipindi Hali hii iliposhamiri kushitukiwa na serikali. Enzi za Abbas Gulamali na Azim Dewji hii Hali ilikuwa juu Sana. Timu iliweza kusafiri na mipira 30 ya mazoezi wakirudi Wanarudi na mipira mipya 30. Mambo yalikuwa mengi kipindi hicho cha Giza Ila sijui kama mpaka Leo bado wanaendelea.
Nikija Kwa hoja ya mleta Uzi kuhusu timu kwenda nje huku ikishindwa kusajili Wachezaji wazuri Kwa hela kubwa, nadhani hili amelijibu mwenyewe. Safari za pre-season zinadhaminiwa na Mtu Kwa malengo na faida yake ya kibiashara. Kwa hiyo anayemlipa Mpiga Ngoma ndiye anayechagua wimbo.
 
Yaweza kuwa kweli
 
Ningeandika pia, maana najua yanga haina hata uwanja wa kupigia pushup wachezaji, lakini pia ina wachezaji wapya wa kigeni ambao ingekuwa fursa yao kuja nchini mapema na kuzoea hali ya hewa, vyakula na viwanja kabla ya ligi kuanza.
Basi kaa kimya ya simba hayakuhusu dili na utopolo walioabakia kigamboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…