Kuna siri gani kwenda Pre-Season nje ya nchi kwa timu masikini?

Pre season zote dunia ni psychological issues hakuna team duniani hasa team zinabaki kwenye nchi yake fuatilia team zote kubwa ulaya sasa hivi ziko wapi kiufupi pre season ni kuweka sawa psychology ya mchezaji ambayo ina nafasi kubwa kwenye performance ya mchezaji.
 
Viongozi Simba hawataki wanachama wengi bali wanataka mashabiki wengi oyaoya. Niliwauliza kwanini, wakajibu eti kwakuwa Kuna hisa hivyo kama wanachama wakiwa wengi dividend itapungua, yaani faida kwa wanahisa itapungua. Kwa maana nyingine wanataka wanachama wabaki haohao milele kwaajili ya uroho wa pesa. Wanamtegemea mo afanye kila kitu. Ndio maana mo anawazingua kila mara, ni nyani wala mabibo.
 
Pre season unakwenda kutafuta vitu vingi kwa wakati mmoja. Lakini kikubwa zaidi ni kutafuta muunganiko wa wachezaji kuwa timu moja. Huo muunganiko utaupataje kama wachezaji wengine hawako kambini? Lakini je, hali ya hewa ya Kambi ni sawa na hali ya hewa ya mashindano unayoyaendea? lakini je viwanja vya preseason ni sawa na vile vya nangwanda? Je, unao wachezaji wageni wanaohitaji adaptation ya hali ya mambo kwenye nchi??
 
Nakazia hapa

Mamlaka husika zifanyie kazi hii kitu
 
Utajiri wa dewj na gulamali families ukiuchunguza saaaaaana vizuri wana sababu za kuwa wafadhili wa club hizi. Sehemu kubwa ya mtaji huenda ulitokana na timu hizi. Kwenye mabegi, kwenye mpira, kwenye makontena ya zawadi na vifaa vya timu huenda Kuna mambo mambo!!!
 
Kama kusafiri tu kwenye mechi za Caf mnapanda ndege za abiria na mnakwenda kimafungu ndo mtaweza kwenda pre season nje ya nchi mkae wiki tatu?
Simba huwa wanaoanda Private jet kwenye mechi za Cuf?
 
We mjinga sikiliza timu za Ulaya huwa wanaweka kambi lets say Man U Anaenda China au Marekani ni kwa sababu ya Biashara na si vinginevyo wanaenda kutaga timu kupata mashabiki wapya ili wapige pesa kwenye jezi. Sasa Simba kunabBiashara anafanya Uturuki? Tunaiga hadi ujinga
 
Ngada je?
 
Nakazia hapa

Mamlaka husika zifanyie kazi hii kitu
Tumepigwa sana, unashangaa vijana wetu wamelewa TU, unga umepitia wapi kuingizwa nchini haijulikani, kumbee uliingizwa wa kutosha wakati wa preseason!!!!? Whistle browsers hawauawi
 
Hapa ndio navishangaaga HV vilabu vyetu kusafiri kwenda uturuki mbna hatuwasiki mamelod

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwani shida iko wapi mkuu yaani kwasababu yanga wapo avic town kwa hyo kila mtu abaki avic town kisa alibahatisha final.
 
Kwani shida iko wapi mkuu yaani kwasababu yanga wapo avic town kwa hyo kila mtu abaki avic town kisa alibahatisha final.
Hakuna association kati ya kambi ya preseason ilipo na mafanikio kwenye mashindano. Tumevamia mtumbwi wa vibwengo TU sisi kwenda ng'ambo preseason. Sisi ni kwaajili ya ngada lakini wenzetu ni kwaajili ya marketing na business. Wao preseason inawezakuwa ni sehemu ya udhamini.
 
Ona mwenyewe!! kocha yuko Brazil, wachezaji nusu Uturuki na nusu Dar es salaam, Tz. Hiyo ni pre-season ya wapi? vuluvulu fc. Kuna jambo muhimu hapo ambalo ni zaidi ya preseason, vyombo husika fanyeni kazi yenu kikamilifu, maana hakuna pre-season ya hivi duniani. Kocha Mkuu hayuko kambini, wachezaji muhimu kama Chama. Sakho, Baleke, Onana, Ngoma na wengine hawako kwenye kambi ya preseason sasa preseason wanafanya nini? Huo muunganiko wa timu utafanywa na nani kwa wachezaji gani?
 
Una hoja ila ushabiki umetuharibu akili, ukitoa hoja kinzani na simba basi wewe yanga, ukitoa tofauti na yanga basi wewe simba.
 
Wale wanaobaki avic town ,hawana mchongo huo?
 
Umeeleweka vzr sana,tuliwahi kuhoji hili sehemu flani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…