Kuna tatizo gani Nigeria ? Kutoka Naira 1 = Shilingi 5 za kitanzania mpaka shilingi 1.8 na bado inazidi kuporomoka.

Wanachimba mafuta na wa auza buku kwa lita, tatizo nchi imemezwa na ukabila na udini,
 
Kuchimba mafuta bajeti yake si mchezo bora wazungu watusaidie huku tukiendelea kujipanga
 
Wanaija wanamiliki magari yenye engine zenye cc kubwa, Sasa wanaanza kuona ugumu kuyamiliki mana mafuta yamepanda tofauti na walilvyozoea kununua kwa bei rahisi.
 
Upigaji na viongozi wetu
 
Mamaeee naangalia kwenye vyombo vya habari ,hii ni kiama mzee ,halafu si mafuta tu ,ni hadi. Chakula ,chakula chako kikuu Mihogo ,viazi na mchele ,nyama ,bei hazishikiki
Hii inflation inayowakuta Nigeria sio mchezo
 
Madeni ya nje, wananchi wana wasiwasi wananunua dola kwa wingi kujilinda
Hio ni kweli kabisa nchi ikiwa ina madeni pesa yake inashuka, kinachosaidia pesa kuwa strong ni Political and economic stability and the demand for a country's goods and services are also prime factors in currency valuation.
 
Hao wanajua utapeli tu
 
Rahisi.
Uongozi mbaya, rushwa, ufisadi, wizi, tamaa....
 
Unaweza kufanikiwa kuchimba mwenyewe jamaa wakayawekea vikwazo mafuta yako usiuze sababu hufuati haki za binadamu unauwa raia hovyo.
Unakuta raia wenyewe ni Boko Haram ambao sasa wanaitwa maghaidi na hao hao waweka vikwazo.
Kwani umesahau yaliyo tokea au yanayo endelea kutokea Syria?
 
Mkuu unawalsumu Nigeria wakati sisi ni copy and paste ya wao tuna vitu vingapi vinatushinda hapa mpaka mwendokasi tu tupo hovyo ndio huko kwenye kuchimba mafuta au madini..
 
Vijana Nigeria wakiomba Passport asubuhi on-line jioni anapata wanashangaa sisi tunavyobaniwa kupata passport miezi kadhaa mtu anafatilia mkwaju.
 
Kama sisi hapa almost contract zote za ujenzi wanachukua wachina, in trillions of money.

Sasa sijui kwanini tusiweke watu wetu huko wawe wanajifunza jamaa wanachokifanya mwisho wa siku tufanye wenyewe.

Ndivyo mataifa huwa yanakuwa na nguvu za kiuchumi, kwa kujenga uwezo wa ndani. Sio kutegemea wageni tu.
 
Mamaeee naangalia kwenye vyombo vya habari ,hii ni kiama mzee ,halafu si mafuta tu ,ni hadi. Chakula ,chakula chako kikuu Mihogo ,viazi na mchele ,nyama ,bei hazishikiki
Sio poa mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…