desayi
JF-Expert Member
- Aug 27, 2017
- 3,593
- 5,848
Vipi baba wa mtoto hakumegei appleSiku ninawajulisha ndugu zangu kuwa namwoa dada x ambaye amezaa, mamangu aliapa viapo vyote na kulia kikamilifu. Walioniunga mkono ni wadogo zangu wawili wa kiume tu.
Ila leo katika familia nzima, msaada wa haraka na wa dhati ambao mama huutegemea ll the time huwa ni huyu mke wangu. Sijui huwa anajisikiaje wakati alimkataa.
Ninamshukuru Mungu kwa kunipa huyu mwanamke. Ninampenda na ananipenda.
Sent using Jamii Forums mobile app