Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Nachukia sana mwenge. Natamani aje atokee mwamba anaemuamini Mungu kikweli kweli atengue hilo tambiko. People have been praying over and over lakini wapii. Kuna tambiko lingine lilifanyika Zanzibar, ni baya zaidi kuliko haya yanayofahamika sana. Mungu atusaidie tu la sivyo hatutatoka hapa.
Hili la zenj muhusika pia ni JK Nyerere????

Au Maalim seif?
 
Hebu funguka zaidi kuhusu tambiko la nchi la Zanzibar mkuu
Lilifanywa na Nyerere pamoja na karume na kuna makubaliano ya kwenda kufanya renewal ya makubaliano yao kila inapoingia awamu mpya ya uongozi. Wanapeleka ajenda wanazotaka na wao kupewa masharti ama matakwa na wahusika wa ulimwengu huo mwingine. Kiongozi wa hayo matambiko huwa anatakiwa kuwa binti bikra wa umri usiozidi miaka 16.

Unakumbuka ajali ya MV spice islander ya September 2011? Ile ilikuwa moja ya demand za makubaliano yao 2010.

Kuna mzee mmoja nilikutana nae Morogoro 2014 alikuwa anaandaa kitabu kabisa cha matambiko yote makubwa yaliyofanyika nchini; kusini, Dodoma na Zanzibar. Too bad sijui aliishia wapi, sikupata kumsikia tena. Nchi ilikabidhiwa kwa shetani, Mungu aturehemu tu aisee.
 
Thus awataki katiba mpya na uraia pacha hivi vinafungua code.
Uraia pacha na katiba mpya ni sawa na dawa ya panya na panya.
Hivi viwili ndio code ya kuisambaratisha ccm.Ccm ikifa nchi itafunguka na maendeleo yataanza kuja.
Maana tunakupandia ukale na ujinga saa nyingine hata sio uchawi ni uoga wa changes za kijamii
 
Nyie waongo watupu. Lindi sio mkoa masikini kuliko yote TZ. Yaani hata darasa la 7 anapata hilo swali. Wewe inaonekana ndio wale wale unafaulu kwa madesa.

sababu za mikoa mingi ya pwani kuwa masikini ndio utakuwa hujui kabisa
Mikoa masikini ni ya kanda ya ziwa has geita na Mwanza
 
Mshana Jr nashawishika kusema kuwa kuna marekebisho kidogo pale ulipoandika UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU, usahihi ni kwamba UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU.

Lakini maudhui ya andiko yanabaki kuwa taifa lipo katika hali isiyoelezeka.
[emoji1545][emoji1545][emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1548]
 
Lilifanywa na Nyerere pamoja na karume na kuna makubaliano ya kwenda kufanya renewal ya makubaliano yao kila inapoingia awamu mpya ya uongozi. Wanapeleka ajenda wanazotaka na wao kupewa masharti ama matakwa na wahusika wa ulimwengu huo mwingine. Kiongozi wa hayo matambiko huwa anatakiwa kuwa binti bikra wa umri usiozidi miaka 16.

Unakumbuka ajali ya MV spice islander ya September 2011? Ile ilikuwa moja ya demand za makubaliano yao 2010.

Kuna mzee mmoja nilikutana nae Morogoro 2014 alikuwa anaandaa kitabu kabisa cha matambiko yote makubwa yaliyofanyika nchini; kusini, Dodoma na Zanzibar. Too bad sijui aliishia wapi, sikupata kumsikia tena. Nchi ilikabidhiwa kwa shetani, Mungu aturehemu tu aisee.
Mkuu huyu binti anapatikana kwa njia zipi ?

Na je huwa anatolewa kafara au hubaki hai ?
 
Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.
Hapa bila shaka unamaanisha ushirikina. Kama una maanisha Ushirikina kauli hii si ya kweli bali ina uongo mwingi. Yapo mataifa mengi yamesimama pasi na chembe ya hayo uliyoyasema,bali mengi yalianguka kutokana na hayo uliyo yasema. Mataifa yote ambayo yalikuwa chini ya mitume haua yalisimama pasi na chembe ya kafara wala matambiko bali wala kwa vyama vya mashetani,rejea ufalme wa nabii Suleyman,rejea taifa la Saudia kwa zama zetu hizi,sasa unaposema hivi sijui uliwaza nini ?
 
Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.

Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.

Tanzania nj taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk

Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana.. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana.. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi

Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?

Kafara la Bagamoyo ni la moto..na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho

"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"

Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?

Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani...sasa hapa ndio penye shida...ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa

Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda

Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake
Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi
Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao

Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana

Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega

Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?
Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
Umeupiga mwingi sana kaka
 
Moshi huo kitu kidogo Mshana Jr anazungumzia wachawi wote wa nchi walivyozunguka nchi yote na kwenda Lindi vijijini ambapo MOHAMMED ABOUBAKAR LUSINDAMBA alienda kikao Cha wachawi Cha kidunia Cha Abu Dhabi akaja na maazimio ya zindiko hilo la pili la Lindi la 1990.
Tambiko la Lindi kilufanyika siku chache kabla ya 9)12/1961, Ardhi ilipasuka, ikameza watu zaidi ya 50, ikajifukia.
Kabla ya hapo Lindi haukua mkoa, na tafsiri ya neno/jina Lindi ni shimo
 
Jamaa aliyeshiriki matambiko yote kaeleza vyema na nini kifanyike Ili kuikomboa nchi dhidi ya maagano ya kishetani.
Huyu alikuwa ni mwenyekiti wa wachawi tanzania kwa sasa ameokoka ameyaacha yote ana muhubiri Kristo.Huyu jamaa ni masta kwenye mambo ya ulimwengu wa roho.
Ana clip nyingi Sana anafundisha anaitwa Shehe Omari Mnyeshani amesoma elimu zote uchawi na uganga kufundishwa na wa darasani na pia amewahi kuwa mkuu wa chuo cha uchawi na uganga nchini.
Kwanini asifanye yeye? Anaogopa nini mkuu

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom