Halafu ni Serikali hii ya CCM inayotuambia sisi wananchi tunaohoji kuhusu tozo tuamie bujumbura ndo watufundishe somo la uzalendo?,Labda siyo mimi kwa kweli [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] ,Serikali hii ambayo waziri anachoma hela ya walipa kodi analeta dawa ya Corona nchini na kutwambia "dawa hii kule madagascar inatolewa na Rais pekeyake" ? Serikali hii inayotuambia siku ina masaa 48? Serikali hii inayotuambia sisi ni matajiri duniani na hatutakopa? Hapana aisee
Mkuu hali ni tete sana,Magufuli alishaharibu uchumi na angeendelea kwa miaka mingine mitano,Tanzania lazima inge collapse.Ukiwasikiliza serikali wanakwambia uchumi unakuwa kwa kiwango cha 4.7% lakini ukipitia report ya IMF,tathmini yao inasema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa 1%.Meko alikopa fedha nyingi sana kwenye taasisi za kifedha za ndani na kimataifa kwa kufanya forgery kubwa za masuala ya kiuchumi na wakafanikiwa kupewa hela,sasa changamoto imebaki kwenye marejesho ya mikopo ambayo serikali lazima ilipe na hapa ndo panapowatoa jasho kweli kweli ndiyo maana wanakuja na matozo yasiyoeleweka ili kufanya marejesho ambayo hayaendani na uhalisia wa kiuchumi,kiufupi wanaumbuka.Mimi nikimwangalia huyu mama na mambo anayoyafanya naona kabisa anazungukwa na wasaidizi mizigo kabisa-Example,Hawa wakina Gwajima na Madilu system huwa wanaweza kumshauri nn cha maana zaid ya ujinga? Uchumi ambao unasinyaa hauwi-stimulated kwa kupandisha matozo yasiyoeleweka bali inahitaji maamuz smart ambayo yatamfanya mwananchi apate fedha ili uwezo wake wa kufanya manunuzi uongezeke na hivyo kukuza uchumi na mzunguko wa fedha nk.Binafsi nakuhakikishia 100% serikali haijapata hata 10B kwenye hz tozo mpya-Ni usanii tu wanaofanya,na kwa mtu mwenye uelewa na kuona mbali anajua kabisa serikali imeshaanza kupata trouble na miamala hvyo inajinasibu hvyo kwamba imefanikiwa ili ikifanya u-turn ghafla isionekane imeshindwa utekelezaji-Serikali hawana ujanja kwenye hili,lazima wapige reverse watake wasitake.Unakumbuka wakati wa Magufuli serikali kupitiaTRA ilivyokuwa inajinasibu inakusanya sana mapato kwenye vyombo vya habari,report ziliishia wapi??Uchumi haudanganyi kamwe,marejesho yanawaumbua [emoji1787] [emoji1787] .Hapa mwishoni Magufuli alikuwa ameshaanza kupiga kelele za kuomba mataifa makubwa iisamehe Tanzania madeni kwa sababu alikuwa ameshaanza kuona heat manake kushindwa kulipa madeni tunayodaiwa kuna implications zake-na zote siyo nzuri.Yanayoendelea ni recipe ya Tanzania kuelekea kwenye demokrasia-Manake CCM ni very powerless now,hawana hela wala capacity ya ku-manage nchi tena.