Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,834
- 3,042
Asante mtumishiitakuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua kope/eye blink speed..cha haraka sana speed kubwa sana.
Kitajulikana kwa sababu itakuwa watu wawili wakiwa shambani wanalima mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa,wawili watakuwa shambani mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa.Watu wataarifiana kuhusu taarifa za kupotea kwa watu dunia mtaani,mkoa,nchi nzima na dunia kwa ujumla itarepotiwa watu kupotea na kuna watashuhudia nguo zimebaki watu hawapo au kama mlikuwa mnafanya jambo pamoja mnaona mtu anavanish chap si mnashuhudia na ukiuliza na kwingine habari zitatapakaa dunia nzima.
Then kuanzia hapo sasa NEEMA ILE NEEMA INAYOZUIA MABAYA ya wale watu wa Mungu ndio waliokuwa wanatulinda sisi kupitia maombi yao na uwepo wao na Mungu alikuwa anazuia mabaya yasiwapate kanisa lake watu wake na sisi tunanufaikamo,na mvua alikuwa anawanyeshea wema na sisi wabaya tunanufaikamo(wema na wabaya wote tunapata mvua.)
Na shetani na malaika zake walikuwa wanafungiwa kuzimu kwa ajili ya kuwalinda watu wake na sisi tunanufaikamo.
Na hiyo neema ipo mpaka sasa inatusubiri hata sisi wenye dhambi tutubu tuingie kuwa wamoja ya watoto wake kanisa lake kondoo wake tuache dhambi atusamehe.
BAADA YA UNYAKUO KUCHUKUA WATU WAKE...ile neema itaondolewa au itapungua ina maana wataobaki walioachwa duniani kuna baadhi watavumilia mateso ya miaka 7/2 nusu ya miaka 7 ilifupishwa kutoka 7,kama ingekuwa 7 hakuna angeweza vumilia,so watakaovumilia hata mauti yao bila kumkufuru Yesu na kumsujudia SHETANI watakao itetea imani yao wakivumilia mateso nao baada ya kufa Roho zao zitaingia mbinguni zikaungane na wale walionyakuliwa washerehekee kwa miaka 1000 toka ile siku ya unyakuo katika karamu ya watakatifu mbinguni washindi wateule.
Baada ya miaka 3.5 ya dhiki kuu...na miaka 1000 ya karamu ya watakatifu mbinguni wakati huo wenye dhambi wako kuzimu ya duniani wakiteseka .
Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu mara ya tatu akiwa na jeshi la watakatifu na malaika.Wema PEPONI na wenye dhambi katika ziwa la moto na shetani na mapepo majini.
BAADA YA HAPO Yesu atakuwa amemaliza kazi yake aliyotumwa na Mungu Baba,KAZI GANI hiyo 1)Alishiriki kumuumba binadamu mbinguni akishirikiana na Mungu baba na Roho Mtakatifu.2)Alikuja duniani katika umbo la binadamu akasulibiwa msalabani akateswa akafanyika kafara kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kupitia damu yake ili kila mtu kupitia yeye aokolewe kutoka dhambi atubu dhambi,amkubali Yesu..NDIO KIPINDI TULICHOPO cha hii neema ya bure inatusibiri walioko baa,lodge,wanaowanga,wezi,waasherati,wachawi,wote tunasubiriwa na hii neema ya bure...ila hii neema ina mwisho wake tusichelewe
3)UNYAKUO ..ndio huu umekaribia...neema itaondolewa.