Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

1736260731925.png
 
samaki wakubwa kama papa, nyangumi wana uwezo wa kummeza mtu.
Hapa hujatumia Logic, umeikwepa logic. ili utumie logic lazima ujiulize maswali na upate majibu.

Mfano, ili papa au nyangumi ammeze binadamu na asipoteze maisha, inatakiwa kinywa na tumbo lake liwe na mazingira ya aina gani?

Je Nyangumi na Papa wana kinywa na mazingira yanayowezesha kummeza binanadamu na akaishi?

Jibu ni Hapana sababu koo la nyangumi au papa kumpitisha binadamu bila kumvunja vunja kwa kemikali au meno haiwezekani.

logic ni reason. Mungu hafanyi jambo lisilo na sababu. shida ni kutaka kujua mambo ya rohoni kwa akili
Hakuna Logic bila akili mkuu.

Mfano: Mkeo akija akakwambia ana mimba na hujamwingilia miezi miwili akakwambia ni kwa uwezo wa malaika wa kiroho utatumia nini kitakachokupa logic kutatua hiyo hali bila kuhusisha akili?
 
Okay, nieleze Mungu alipomuumba Adamu, alimuumba Yeye MUNGU akiwa katika umbo Gani?

Wakati Mungu anachomoa mbavu za Adamu kumfanya Eva, MUNGU alikuwa katika umbo Gani?

Haya ni kwanini jini aweza mtokea mtu katika umbo Lolote Iwe la nyoka, Simba, Mwanamke, Mwanaume na usiamini kuwa MUNGU aweza zaliwa katika hori?

Inashangaza yule kichaa pale pwani Ya Wagerasi, Yale majini yalokuwa yamemkalia yalimtambua YESU ni nani na yakamwomba Asiyatese kabla ya wakati, yalimtambua ni nani lakini Binadamu anajiuliza maswali kumhusu.
Umeenda mbali Sana,
Twambie Mungu mwnyw kipind anaiumba dunia na vilivyomo, yeye alikua wapi.
 
Pia tujue hili,

Unyakuo utaanza kwanza Kisha maisha ya taabu na dhiki kuu yataanza rasmi duniani WATAKATIFU wakiwa mapumzikoni.

Baada ya miaka elfu , Yesu atakuja kuwachukua na kufufuka waliowake washindao mateso ya dhiki kuu.

Baada ya hapo ndipo ataihukumu Dunia na Ulimwengu kutupwa Ziwa la moto jehanum baada ya kuhukumu.
Dhiki kuu ni miaka 7 then wale tulionyakuliwa ambao itakuwa tumeshakaa mbinguni miaka 7 kwenye karamu ya mwanakondoo (wakati dhiki kuu ikiendelea duniani) tutarudi kuja kutawala miaka 1000 hapa duniani. Hizi ni nyakati nzuri sana kwa sis tuliofanya toba na kuishi maishi matakatifu maana kwa mara ya kwanza imekuwa ikiamininiwa pasipo shaka hata chembe kuwa kuna watu tena wengi sana kamwe hatutaonja mauti kwa maana tutanyakuliwa! yaani sisi tulioamuwa kutubu kumuamini bwana Yesu na kuishi maisha matakatifu.
Kuna uamsho mkubwa sana unakuja duniani ambapo watu wengi sana wataokoka then wakati uamsho huo ukiendelea ghafla unyakuo utatokea.
 
Pengine wewe bado mtoto mdogo wa 2000, ila sie wazee wako tulishaahidiwa na manabii wa kizazi kipya kuwa mwisho wa dunia ulikuwa mwaka 1978, wakachemka tena na kusema mwaka 1982 mara 1999......cha kushangaza mpaka leo bado tunapeta tu na kugawana dhambi according to dini za kuletewa.
Mwisho wa Dunia hauji kabla ya Unyakuo wa WATAKATIFU.

Majira tuliyopo ni karibu kunyakuliwa Kanisa.

Get prepared
 
Mwaka 82 kuna jamaa aliuza kila kitu...akawa analewa ...akisema PONDA MALI KUFA KWAJA>>>>>>>>>> akawa lofa na kufa hakufa na mwisho wa dunia hakuna.....🙂🙂🙂🙂
Hizi dini za kuletewa zipigwe tu ban hapa Afrika, zinafanya wananchi wetu kuwa wajinga sana.
 
Badala ya kunukuu alichokisema Yesu mwenyewe kuhusiana na mwisho wa dunia na kurudi kwake mara ya pili mlikuwa mnasubiri mdanganywe na wahuni?. Hakukuwa na Biblia?
Nani aliyedanganywa sasa? Mimi si mtu wa kudanganyika na mwanadamu mwenzangu haswa linapokuja suala la kuamini dini za kuletewa na watu wa nje, hutonipata hata iweje....nitakusomesha na kukufungua macho mpaka utajiua mwenyewe au kujipiga vidole huku unalia.
 
Hizi dini za kuletewa zipigwe tu ban hapa Afrika, zinafanya wananchi wetu kuwa wajinga sana.

swali kama Dini zinafanya wananchi kuwa wajinga, je, kabla ya Ukristo walikuwa werevu? hao wananchi waliishije? Usisahau kabla ya Ukristo kuingia (miaka kama 150 tu iliyopita) tanzagiza au hii sehemu tunaishi leo hii waliojua kusoma na kuandika walikuwa <1% ukiondoa waliojua kukariri kuran tu kiarabu tena ukanda wa pwani tu, leo hii tanzagiza wanaojua kusoma na kuandika ni >95% halafu unasema Ukristo unafanya watu wajinga?
 
Acha kujidanganya mkuu, Yesu hawez kurudi.

Tena Kwa wayahudi tulionao sahivi, watampiga Yesu makombora mpk achakae.

Bora kina Pilato walimhurumia wakamgonga misumari nchi 6 mikonini na miguuni Ila wakauacha mwili wake angalau unatambulika ukiutizama

Ila Kina Netanyau hawacheki na kima, wataulipua,kuuchakaza na kuufukia na vifusi vya Gaza.
Kunywa bia mkuu nakuja kulipa 🤣🤣🤣🤣
 
unafahamu malimbuko? (first fruits)
tabia za kanisa la filadelfia ni kanisa ambalo halitapitia kwenye dhiki. kuna unyakua wa zaidi ya mara mbili:
1. Malimbuko (kanisa la wazaliwa wa kwanza)
2. Mazao (Hawa ni wengi) Yohana aliulizwa: na Hawa? akaambiwa hawa ni wale wanaotoka katika Ile dhiki
3. Mabaki
Totally confused 😕 😕
 
swali kama Dini zinafanya wananchi kuwa wajinga, je, kabla ya Ukristo walikuwa werevu? hao wananchi waliishije? Usisahau kabla ya Ukristo kuingia (miaka kama 150 tu iliyopita) tanzagiza au hii sehemu tunaishi leo hii waliojua kusoma na kuandika walikuwa <1% ukiondoa waliojua kukariri kuran tu kiarabu tena ukanda wa pwani tu, leo hii tanzagiza wanaojua kusoma na kuandika ni >95% halafu unasema Ukristo unafanya watu wajinga?
Wananchi wetu walikuwa werevu na waliishi kwa amani, only dini za kuletewa ndizo zilikuja na kuharibu mambo kiasi kwamba kwa sasa Mkristo kuoa Muislam japo wote ni Watanzania na pengine wa kabila moja inakuwa shida lakini zamani tulioana tu na tuliishi kwa amani. Kwa akili yako kusoma na kuandika ni Ukristo kweli au werevu? Jibu halafu nitakujibu tena kutokana na uelewa wako, niko hapa nakuangalia tu unavyojikanyaga taratibu na kujitoa kafara.
 
Mkuu ila naamini unyakuo itakuwa kimya wala haitajulikana ila sasa baada ya kukaa huko mbinguni na kisha kurudi ndio watamwona au mimi nimetafsir vibaya.
itakuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua kope/eye blink speed..cha haraka sana speed kubwa sana.

Kitajulikana kwa sababu itakuwa watu wawili wakiwa shambani wanalima mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa,wawili watakuwa shambani mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa.Watu wataarifiana kuhusu taarifa za kupotea kwa watu dunia mtaani,mkoa,nchi nzima na dunia kwa ujumla itarepotiwa watu kupotea na kuna watashuhudia nguo zimebaki watu hawapo au kama mlikuwa mnafanya jambo pamoja mnaona mtu anavanish chap si mnashuhudia na ukiuliza na kwingine habari zitatapakaa dunia nzima.
Then kuanzia hapo sasa NEEMA ILE NEEMA INAYOZUIA MABAYA ya wale watu wa Mungu ndio waliokuwa wanatulinda sisi kupitia maombi yao na uwepo wao na Mungu alikuwa anazuia mabaya yasiwapate kanisa lake watu wake na sisi tunanufaikamo,na mvua alikuwa anawanyeshea wema na sisi wabaya tunanufaikamo(wema na wabaya wote tunapata mvua.)
Na shetani na malaika zake walikuwa wanafungiwa kuzimu kwa ajili ya kuwalinda watu wake na sisi tunanufaikamo.
Na hiyo neema ipo mpaka sasa inatusubiri hata sisi wenye dhambi tutubu tuingie kuwa wamoja ya watoto wake kanisa lake kondoo wake tuache dhambi atusamehe.
BAADA YA UNYAKUO KUCHUKUA WATU WAKE...ile neema itaondolewa au itapungua ina maana wataobaki walioachwa duniani kuna baadhi watavumilia mateso ya miaka 7/2 nusu ya miaka 7 ilifupishwa kutoka 7,kama ingekuwa 7 hakuna angeweza vumilia,so watakaovumilia hata mauti yao bila kumkufuru Yesu na kumsujudia SHETANI watakao itetea imani yao wakivumilia mateso nao baada ya kufa Roho zao zitaingia mbinguni zikaungane na wale walionyakuliwa washerehekee kwa miaka 1000 toka ile siku ya unyakuo katika karamu ya watakatifu mbinguni washindi wateule.

Baada ya miaka 3.5 ya dhiki kuu...na miaka 1000 ya karamu ya watakatifu mbinguni wakati huo wenye dhambi wako kuzimu ya duniani wakiteseka .

Yesu atarudi kuhukumu ulimwengu mara ya tatu akiwa na jeshi la watakatifu na malaika.Wema PEPONI na wenye dhambi katika ziwa la moto na shetani na mapepo majini.

BAADA YA HAPO Yesu atakuwa amemaliza kazi yake aliyotumwa na Mungu Baba,KAZI GANI hiyo 1)Alishiriki kumuumba binadamu mbinguni akishirikiana na Mungu baba na Roho Mtakatifu.2)Alikuja duniani katika umbo la binadamu akasulibiwa msalabani akateswa akafanyika kafara kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kupitia damu yake ili kila mtu kupitia yeye aokolewe kutoka dhambi atubu dhambi,amkubali Yesu..NDIO KIPINDI TULICHOPO cha hii neema ya bure inatusibiri walioko baa,lodge,wanaowanga,wezi,waasherati,wachawi,wote tunasubiriwa na hii neema ya bure...ila hii neema ina mwisho wake tusichelewe
3)UNYAKUO ..ndio huu umekaribia...neema itaondolewa.
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Sio Trump anarudi tena kweli.
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Picha please
 
Pia tujue hili,

Unyakuo utaanza kwanza Kisha maisha ya taabu na dhiki kuu yataanza rasmi duniani WATAKATIFU wakiwa mapumzikoni.

Baada ya miaka elfu , Yesu atakuja kuwachukua na kufufuka waliowake washindao mateso ya dhiki kuu.

Baada ya hapo ndipo ataihukumu Dunia na Ulimwengu kutupwa Ziwa la moto jehanum baada ya kuhukumu.
We Gwajima hebu acha ujinga wako

Cc: Lamomy Labella Extrovert Nyani Ngabu
 
Wananchi wetu walikuwa werevu na waliishi kwa amani, only dini za kuletewa ndizo zilikuja na kuharibu mambo kiasi kwamba kwa sasa Mkristo kuoa Muislam japo wote ni Watanzania na pengine wa kabila moja inakuwa shida lakini zamani tulioana tu na tuliishi kwa amani. Kwa akili yako kusoma na kuandika ni Ukristo kweli au werevu? Jibu halafu nitakujibu tena kutokana na uelewa wako, niko hapa nakuangalia tu unavyojikanyaga taratibu na kujitoa kafara.

tumejua kusoma na kuandika baada ya Ukristo kuja, na sababu ilikuwa tulifundishwa kusoma na kuandika ili tuweze kusoma na kuelewa Biblia takatifu, kabla ya Ukristo hakuna aliyejua kusoma wala kuandika ukiondoa waislamu wa pwani waliojua kukariri kurani tu kwa kiarabu tena.

kabla ya Ukristo kuingia hakukuwa hata na Shule moja kama tuijuavyo Shule leo hii, hakukuwa na nchi kama tuijuavyo leo hii, hata civilisation tu ya kuishi kwenye Cities haikuwepo, kwani hatukujenga miji kama tuijuavyo leo hii …
 
Back
Top Bottom