Kuna tetesi ligi kuu yetu wapo wachezaji wa nje wanakunja mpaka milioni 10 kila mwezi. Je, kuna mzawa yeyote anealipwa hata milioni 5 ?

Kuna tetesi ligi kuu yetu wapo wachezaji wa nje wanakunja mpaka milioni 10 kila mwezi. Je, kuna mzawa yeyote anealipwa hata milioni 5 ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwa wachezaji wa nje wa hapa bongo wapo wanaokunja hadi milioni 10 lakini kwa wazawa wetu kuna utata.

Tukija kwa wachezaji wetu wa hapa bongo, kunaweza kuwa na yeyote anaelamba walau dola elf 3 kwa mwezi takribani shilingi za kitanzanha milioni 7 kila mwezi?

Kuna tetesi zipo kwamba Feisal Salum Feitoto ndie anaelipwa zaidi kuliko wachezaji wenzake Gsm anammwagia pesa ila haijabainika makadirio ni sh ngapi, wataalam tunaombeni msaada wenu kama itakuwa alau imefikia dola elf 3.

John Boccco alikuwa anakimbiza kwenye list lakini kwa sasa nae kiwango kimeshuka huenda mshahara wake nao umeshuka tofauti na kipindi yupo Hot, kwa pale simba namna wahindi walivyo strict kwenye kupunguza matumizi ili faida iwe kubwa hata hio mikataba ya wachezaji itakuwa imejaa sana vipengere vya kuwapunguzia malipo yao viwango vikishuka, unadhani hata mchezaji akiviona hivyo vipengere ataacha?

Mikataba ya kihindi huwa inamlinda sana mhindi apunguze malipo uwezo ukishuka ili kumzuia hasara, Mhindi ni mfanyabiashara strict sana, Huenda Bocco alikuwa anakunja 12 M akiwa hot lakini kwa sasa hata 5 anaitafuta kwa tochi, Na analipwa kulingana na makubaliano ya mkataba wenye vipengere vya kuzuia hasara kwa mhindi.

Manula ni kipa mzuri ila inaonekana hafikii hizo level japo anazikaribia, mwaka huu alivunja mkataba na meneja wake Jemedari Said kwa tetesi kwamba halipwi anachostahili na meneja wake hana utaalam wa kutosha (negotiation skills) kuwashawishi wahindi wa pale simba kumlipa mshahara mnono kulingana na mchango wake kwenye timu.
 
Ayo maneno ya kwenye kahawa, hakuna mchezaji kutoka nje ya nchi apa bongo anayelipwa milioni kumi labda kocha Tena Kwa tabu sana.
mchezaji akiahirisha kwenda timu zenye uwezo wa kumlipa milioni 10, je wanakuja kwenye timu zile mbili maarufu kulipwa pungufu ?
 
Kwa wachezaji wa nje wa hapa bongo wapo wanaokunja hadi milioni 10 lakini kwa wazawa wetu kuna utata.

Tukija kwa wachezaji wetu wa japa bongo, kunawea kuwa na yeyote anaelamba walau dola elf 3 kwa mwezi takribani milioni 7 kila mwezi ?

Kuna tetesi zipo kwamba Feisal Salum Feitoto ndie anaelipwa zaidi kuliko wachezaji wenzake ila haijabainika makadirio ni sh ngapi, wataalam tunaombeni msaada wenu kama itakuwa alau imefikia dola elf 3.

John Boccco nae kiwango kimeshuka huenda mshahara wake nao umeshuka ila kipindi yupo Hot kuna uwezekano mkubwa hakuna mzawa aliekuwa anamikia kwa mshahara.

Manula ni kipa mzuri ila inaonekana hafikii hizo level, mwaka huu alivunja mkataba na meneja wake Jemedari Said kwa tetesi kwamba kachoka kulipwa mshahara wa kawaida na Meneja wake hana uwezo wa kuwashawishi wahindi wa pale simba wampe Manula mshahara anaostahili
 
Wanapata.. john bocco amekunja zaidi ya hizo toka yupo azam.. na hata alipoenda simba akawa anakunja zaidi ya hizo usd 3000
 
Wanapata.. john bocco amekunja zaidi ya hizo toka yupo azam.. na hata alipoenda simba akawa anakunja zaidi ya hizo usd 3000
John Bocco kiwango kimepungua sana kwa sasa, Nadhani hata wahindi wamepata kisingizio cha kumpunguzia,,

Hii mikataba huwa inakuwa na vipengere vingi sana hasa mlipaji akiwa ni mhindi anataka kuona anacholipia kina thamani, ataongezea vipengere kwenye mkataba kuilinda pesa yake endapo kiwango kikishuka alipe kidogo.

Pesa ya mhindi isikiage tu.
 
Hela nyingi anakula bocco 15+mil (toka aliporenew mkataba 2020)

Manula na mkude hawa wapo over 10+mil(sekeseke za kuongeza mikataba ndio zilifanya simba wajilipue)

Huyo feisal wanaemuimba kila siku monthy salary yake haifiki hata 10mil...ndio maana anapagawa na hela ya bakhresa
 
Hela nyingi anakula bocco 15+mil (toka aliporenew mkataba 2020)
Boko kwa kiwango chake cha sasa wahindi watakuwa wamempunguzia huo mshahara na si ajabu anapokea 4, ni ngumu sana muhindi kutoa pesa aisee.

Mkude nae pia kwa sasa sidhani kama kina Babra wapo tayari kumpa hizo 10, ngumu sana hio, hata ile kesi yake ya utovu wa nidhamu huenda ilimbana zaidi ama ilikuwa ni mambo ya mtonyo tu.

Kwa Manula Naweza kukubali hapo.
 
Kuna mchezaji wa Yanga alikataa offer ya uhamisho wa USD 1 Million kwenda kuupiga Sudan, hivi alikuwa analipwa ngapi?
Ngasa ni mpuuzi sana yule atakufa lofa tena atakuwa mlinzi wa magetini. Unatafutwa upewe pesa ndefu anajificha Magomeni kazi kuoa tu. Hopeless sana anayefuatia ya FeiToto asipokuwa makini atamalizia mpira wake hapo Kaunda Stadium.
 
Kwa wachezaji wa nje wa hapa bongo wapo wanaokunja hadi dola milioni 10 lakini kwa wazawa wetu kuna utata.

Tukija kwa wachezaji wetu wa japa bongo, kunawea kuwa na yeyote anaelamba walau dola elf 3 kwa mwezi takribani milioni 7 kila mwez...
Nimepiga hesabu dollar milioni 10 za aya ya kwanza ni kama bilioni 23+, je umekosea?
 
Ngasa ni mpuuzi sana yule atakufa lofa tena atakuwa mlinzi wa magetini. Unatafutwa upewe pesa ndefu anajificha Magomeni kazi kuoa tu. Hopeless sana anayefuatia ya FeiToto asipokuwa makini atamalizia mpira wake hapo Kaunda Stadium.
Na wakina manula pia ni malofa wa kutupwa alikataa dili la nje akaona sifa anazopewa bongo na maisha ya hapa amerizika
 
Back
Top Bottom