Kwa muda mrefu sana nilikua nikisikia toka kwa ndugu na watu wengine wakimuita merehemu mtu alie kufa siku nyingi zilizopita.
Hivo ilinijengea mimi pia mazoea ya kumuita marehemu, mtu alie kufa mda mrefu.
Pia nimekuwa nikisikia katika vyombo vya habari wakimuita hayati mtu ambae amekufa muda mrefu lakini akiwa na cheo fulani.
Kwa hivo katika fikra zangu zimeweza kufikiri kuwa huenda kuna makundi mawili ambalo kundi la kwanza ni la wale wasio na cheo chochote katika taifa ndio huitwa marehemu lakini pia kundi la pili ni la wale wenye vyeo katika taifa ndio huitwa hayati, sina uhakika na fikra zangu.
Kwahivo nimeona ni bora niilete huku mada ili niweze kupata uhakika wa tofauti kati ya marehemu na hayati.
JamiiForums great thinker.