Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

Mimi naona wote ni sawa tu ila niwewe upendavyo uitwe.
 
Ninavyojua mimi neno HAYATI ni la kiarabu na maana yake ni MY LIFE au maisha yangu kwa waarabu wapendanao utasikia mshkaji anamwambia mpendwa wake YA HAYATI

Lakini huku kwetu hilo neno sijui liliingiaje na kutafsiriwa kama mfu.

Marehemu linajulikana lakini hayati kuwa sawa na marehemu?
 
Wengi wetu ni hayati watarajiwa na pia marehemu watarajiwa.

Unaweza pia ukasema Marehemu hayati fulani.

Kwa Kiswahili ni vibwagizo tu vya kujulisha kuwa unaemtaja kishatangulia akhera na au kumpa heshima aliyetangulia.

Hayati = Aliyeishi
Marehemu = Aliyerehemiwa

Maneno yote hayo mawili yanatokana na Kiarabu kama ilivyo kwa maneno mengi sana ya Kiswahili.
 
Kwa muda mrefu sana nilikua nikisikia toka kwa ndugu na watu wengine wakimuita merehemu mtu alie kufa siku nyingi zilizopita.

Hivo ilinijengea mimi pia mazoea ya kumuita marehemu, mtu alie kufa mda mrefu.

Pia nimekuwa nikisikia katika vyombo vya habari wakimuita hayati mtu ambae amekufa muda mrefu lakini akiwa na cheo fulani.

Kwa hivo katika fikra zangu zimeweza kufikiri kuwa huenda kuna makundi mawili ambalo kundi la kwanza ni la wale wasio na cheo chochote katika taifa ndio huitwa marehemu lakini pia kundi la pili ni la wale wenye vyeo katika taifa ndio huitwa hayati, sina uhakika na fikra zangu.

Kwahivo nimeona ni bora niilete huku mada ili niweze kupata uhakika wa tofauti kati ya marehemu na hayati.

JamiiForums great thinker.
 
Ni hivyo hivyo kama ulikuwa hauko serikalini na ukafa wewe ni marehemu tuu lakini kama ulikuwa na cheo fulati hata kama haukuwa serikalini lakini unajulikana wewe ni hayari
 
nimetoka kumuuliza google transilate
marehem kasema kwa kizungu ni late

kwahiyo baba wa taifa ni late JKN sijua kwanini tumuite hayati na asiitwe marehemu..

kwa neno hayati google transilate bado anatafuta majibu....
 
Ni hivyo hivyo kama ulikuwa hauko serikalini na ukafa wewe ni marehemu tuu lakini kama ulikuwa na cheo fulati hata kama haukuwa serikalini lakini unajulikana wewe ni hayari
vipi kwa kizungu neno hayati linaitwaje mkuu
 
Back
Top Bottom