Kuna tofauti kati ya VAR na Goal Line Technology

Mkuu anaetoa maamuzi kutokana na review za VAR ni maafisa wa VAR au refa
Watu wa VAR hawahusiki katika kutoa maamuzi , anayehusika ni REFA PEKE YAKE. Watu wa VAR wanajukumu la kumsaidia refa kuliona tukio katika angle na position tofauti Ili mwisho wa siku AKAAMUE MWENYEWE .
Refa mara nyingi ana review video kwenye matukio ambayo aliyatolea maanuzi na VAR ikaonyesha tofauti hivyo anaitwa kwenda kujiridhisha
Au kama kuna tukio hakuliona lakini limepita na VAR ikalibaini .
Hapa uko sahihi. Sasa tukio la Jana lilikuwa na utata Kwa Nini hakwemda kufanya REVIEW Refa mwenyewe Ili aje kufanya MAAMUZI kama alivyokwenda kwenye tukio la Lomarisa?
Kuna matukio yakitokea wachezaji wakalalamika anaweza kwenda kuangalia au maafisa wa VAR wakaangalia na kumpa matokeo
Narudia Tena Maafisa wa VAR hawana mamlaka ya mwisho kumpa REFA KUAMUA MATOKEO YA TUKIO.
Game ya jana baada ya lile shuti refa aliwaailiana na maafisa VAR na baada ya review wakamwambia HAKUNA GOLI.
UAMUZI WA MWISHO uwanjani unafanywa na Refa wa kati sio watu wa VAR.
Mwenye mamlaka ya kusema HAKUNA GOLI ni refa wa kati . Sasa refa wewe ndo mwamuzi wa mwisho unaletewa malalamiko na wachezaji kuwa hili ni goli hutaki kwenda kujiridhisha unawaambia watu wa VAR waliangalie na KUAMUA Sasa hapo kazi Yako Nini?
Lakini wangeweza pia kumwambia akajiridhishe iwapo wangeona kuna ulazima huo
Kwani refa umeletewa malalamiko na wachezaji uwanjani unashindwa vipi kuwaambia watu wa VAR nipeni review ya tukio lililotokea dakika hii na sekunde hii then wewe Kwa MACHO Yako ukaenda kujionea? . Yaani refa unasubiri Hadi watu wa VAR wakwambie kaangalie tukio furani et kama Kuna ULAZIMA ?🤣🤣
 
Mbona unajichanganya sasa
 

Wewe ulikuwa na hiyo "goal line technology" au fikra zako tu?
 


Goal line technology inamsaidia refa wa kati kati ya uwanja kugundua kama ni goli limeingia kwa saa yake kuvibrate

Var inamsaidia refa wa kati kwa kumuonesha kwa video ili afanye maamuzi yake.

Refa wa kati ndie muamuzi wa mwisho

Review za VAR na Goal line technology huwa zinaoneshwa katika screen. kama Highlights za review zote kwenye mechi ya yanga zimeonesha mpira haujavuka mstari, je izo walizo review wao wakakataa goli mbona hawakuzionyesha? watu wote tuzione wazi wazi, kwa nini wameficha ficha
 
Kule wana review matukio mkuu

Goal line technology inatoa matokeo yenyewe automatic
Review za VAR na GLT zinaoneshwa katika screen. Highlights za review zote zimeonesha mpira umevuka mstari izo walizo review wao wakakataa goli mbona hawakuzionyesha?
 
Who is suppose to interpret
 
Who is suppose to interpret
Wanao tafsiri review ni refa au VAR officials
Anayekamilisha maamuzi ni refa

Kuna review refa anawasiliana na officials na wanampa majibu bila kwenda kuangali video
Na kuna review refa anaambiwa akaangalie ajiridhishe
 
Review za VAR na GLT zinaoneshwa katika screen. Highlights za review zote zimeonesha mpira umevuka mstari izo walizo review wao wakakataa goli mbona hawakuzionyesha?
Hebu weka hapa hiyo review inayoonyesha mpira umevuka mstari 100%

Acha mihemko angalia kwa utuo mpira ulipodundia kisha screenshot uje utuonyeshe umevuka 100%
 
Kwahiyo wewe hujaiona review inayoonyesha mpira unapiga besela na kudunda chini kisha ukarudi uwanjani?

Kama umeiona tuambie au screenshot utuonyeshe hapa mpira umeingia 100%
 
Hebu weka hapa hiyo review inayoonyesha mpira umevuka mstari 100%

Acha mihemko angalia kwa utuo mpira ulipodundia kisha screenshot uje utuonyeshe umevuka 100%
Tatizo wewe ni shabiki wa simba hatuwezi kuelewana hapa. Izo screenshot, review alitakiwa kuleta mleta mada kusupport hoja yake
 
Kwahiyo wewe hujaiona review inayoonyesha mpira unapiga besela na kudunda chini kisha ukarudi uwanjani?

Kama umeiona tuambie au screenshot utuonyeshe hapa mpira umeingia 100%

Sijaona review ya VAR. Maana haikuoneshwa.

Sisi tumeona marudio tu ya broadcaster wa mechi yaani azam tv. Ila hatujayaona ya VAR

Media hazina jukumu wala mamlaka kuonesha review ya VAR kwa kujitungia wenyewe.

Watu wa VAR huwa wanawapa media taarifa wakati wanafanya review zao na wote tunakuwa tunaona kwenye TV var inavyofanya kazi yake
 
Mkuu kuna matukio yana hitaji “opinion” ili ufanye maamuzi na kuna matukio hayahitaji opinion bali FACT

Mpira wa miguu ni mchezo wa kutumia nguvu na kugusana hivyo basi kuna kiwango cha nguvu na namna unavyo mgusa mwezako kunaweza kutafsiriwa kama ni rafu au sio rafu..... hapa refarii mara nyingi anakwenda kuangalia kwenye slow motion review ili kutafsiri

Lakini kuna matukio haya hitaji opinion ya refa kama offside, mpira kutoka, mpira kuingia golini
Mpira ukitoka au ukivuka goli VAR officials wanamaliza kwa ku review na kumpa majibu refa
 
Tatizo wewe ni shabiki wa simba hatuwezi kuelewana hapa. Izo screenshot, review alitakiwa kuleta mleta mada kusupport hoja yake
Mbona nimeziweka hapo juu hizo screenshot
 
Mbona nimeziweka hapo juu hizo screenshot
LIle shuti lilikua na kasi kubwa sana sio rahisi kupata screenshot ya exactly point ambayo mpira ulitua ila angle waliyochukua kwenye zile review video wakati tunaangalia mechi zilionesha mpira ulidondokea ndani ya mstari sasa kama walitumia review nyingine kutoa maamuzi kwamba sio goli mbona hatukuoneshwa highlights za izo reviews mbadala walizotumia. Inawezekana likawa goli au sio goli lakini jinsi walivyoli-handle ili suala inaleta utata hasa ukizingatia mmiliki wa sundowns ndio uyo uyo rais wa CAF. Haki kutendeka tu haitoshi inatakiwa ionekane kweli imetendeka.
 
Mleta mada ameanza vizuri ila hajatoa msimamo wake,

Swali ni je kama mpira unatakiwa uingie wote 100% ukiangalia mpira kabla haujadunda chini ulivyokuwa una move ulikuwa ndani , ila wakati una dunda ulikuwa haupo ndani 100%? Hili swala naliona refa atabebeshwa mzigo wa ban Yanga wakikaza. Kibaya kwa refa ni kukataa ku review tukio hapo ndipo watu wanaona amepanga matokeo
 
Mkuu nahakika ulisoma fiziksi sekondari

Unaweza kuelezeaje kifizikia jinsi lile lishuti lilivotoka kutoka kwenye besela na kuingia ndani kisha kutoka kukata kona ukadunda kwenye line

Zingatia kwamba besela na mstari vipo sambamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…