Michuano ya CCL hawatumii Goal line technology ambayo ingemaliza huu utata
CCL wanatumia VAR peke yake kusaidia kutoa maamuzi
Angalia Goal line technology ilivyotumika kwenye hii video fupi hapo chini
Utaona ni jinsi gani mpira unatakiwa uwe umeingia kwa asilimia 100 ili kuhesabika goli
So ukiangalia kwa haraka lile shuti lilikua ni kali sana kiasi kwamba unahitaji umakini kuchukua picha exactly pale mpira ulipo dunda na kurudi juu.
Ukichukua picha wakati mpira umekwisha dunda au kabla haujadunda ni lazima mpira utaonekana umevuka mstari kwa asilimia 100
Lakini ukichukua picha mpira unapodunda utaona uligusa mstari
Angalia picha hapo chini, moja mpira ulipodundia na nyingine ni mpira kabla au baada ya kudunda
Mwisho tujikumbushe kidogo kuhusu sheria inasemaje kuhusu mpira kuhesabika kuwa umeingia na kuwa goli.... ni lazima mpira wote uingie na sio asilimia 99.9.
Angalia picha za sheria za goli.
View attachment 2955740View attachment 2955741View attachment 2955743