Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Mzee Umekulia Masaki ,Vipi Mzee Wako Alikuachia Hata Kaplot Masaki?
Hapana mkuu kipindi hiko urban planning ilikuwa ikiheshimiwa mno maeneo mengi tayari yalikuwa yashajengwa yakilimilikiwa na serikali na taasisi zake kubwa,nyumba za mabalozi, diplomats, lazima uwe mtu flani ili kuishi huko!Baada ya serikali kuuza nyumba zake mabadiliko ndo yalianzia hapo if I'm not mistaken.
 
Ishu sio maghorofa ya makazi..
Ishu ni pamoja na maghorofa ya ofisi.....
Kingine ni ukosefu wa mipango
Ingewezekana ikawepo mitaa maalum ya high rising blocks na kwingineko kukawa nyumba za chini ...sio hapa nyumba ya chini ..jirani ghorofa la maofisi
Kama ni hivyo basi Masaki ipo sawa bcoz hata hiyo miji niliyokutajia imechanganyika na ma office vilevile.
Hata manhattan ipo hivyo...sema huko ni Apartment tu hakuna nyumba yakuishi ya chini but zimechanganyika mbona.
 
Masak naona imeanza kuwa uswazi, na mdogo mdogo inaanza kuwa ya kawaida saana, yani saana...

Bar na restaurants nyingi, na security ya premier residential inaondoka kwa kuwa na maghorofa yenye watu wengi sana, lakini zaid nyumba za ghorofa kumi kuendelea zinaongezeka sana.. soon itaanza fanana na Kariakoo.

Security kwa premier residential services ni priority... sasa hapa bungalow hapa ghorofa lenye apartments 40.

Hapo sijazungumzia frame na viduka uchwara.... hadi mama ntilie
Sitoshangaa Masaki siku zijazo ikifanana na Upanga kbs na ndiko tunakoelekea.
 
Iko hivi miji inatanuka masaki ya zamani au sinza ya zamani au kinondoni ya zamani sio ya sasa hiviipo hivi watu wanahamia na watu wanaondoka kwaiyo miaka 20 ijayo masaki itakuwa ya kawaida kama sinza ya zamani kwaiyo mji mwingine utaibuka kuwa wakishua maana siku hizi wengi wanaamia kigamboni uko kuna mijengo ya maana au bagamoyo siku hizi mjini kuna makelele sana
Boss maeneo ya kishua kbs lazima yawepo kwenye nchi yoyote inayojitambua!Usitufikirie sisi Wabongo wenzako wenye hali ya kawaida kuna diplomats, matajiri wakubwa duniani ambao wana standards zao!kwa kifupi Masaki imekuwa mixed na inazidi kuji disqualify kwenye level hizo so sorry to say that!
 
Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.

Hiyo hasa ndio ilikuwa point yako.

Lazima ujue Miji inabadilika sambamba na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, unaweza kukuta baadhi ya miji imekuwa "ghosts" na mingine imekuwa developed for better na hayo ndio maendeleo au kuporomoka kwa nchi kiujumla.
 
Hapana mkuu kipindi hiko urban planning ilikuwa ikiheshimiwa mno maeneo mengi tayari yalikuwa yashajengwa yakilimilikiwa na serikali na taasisi zake kubwa,nyumba za mabalozi, diplomats, lazima uwe mtu flani ili kuishi huko!Baada ya serikali kuuza nyumba zake mabadiliko ndo yalianzia hapo if I'm not mistaken.
Na hii ilikuwa ni maeneo ya kishua tu huko uswahilini mambo yalikuwa yakitimbanganya vibaya mno especially lile bonde la msasani!.
 
Hiyo hasa ndio ilikuwa point yako.

Lazima ujue Miji inabadilika sambamba na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, unaweza kukuta baadhi ya miji imekuwa "ghosts" na mingine imekuwa developed for better na hayo ndio maendeleo au kuporomoka kwa nchi kiujumla.
Hapana mkuu point yangu ni kuona maeneo yote yakiachwa yakiendelea kiholela hii ndo point yangu kubwa.
 
Trend ya miji ya Kibongo ni kwamba pesa ikifumuka watu wanaanzisha ka-mji ka kishua wanafunga kuta na mageti makali. Watoto wanalelewa kishua kila kitu kipo. Wazazi Wakizeeka na kuaga dunia watoto wanaishi kwenye majumba mazuri lakini ukute hawana kipato. Mwisho wa siku wanauza majumba au wanaishi humo wakiendesha biashara haramu nao wanaaga dunia nyumba zinakaliwa na wajomba na mashamgazi ndo hao mnaowaona Masaki.
Umemaliza kabisa
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;
Enzi hizo wakati naishi mimi ;

Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors .

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.
Haya ni matokeo ya kuuza nyumba za serikali chini ya JPM
 
Wacha mamneno mengi mura......
Masaki imejengwa juzi tu hapa tulikua tukipita Nywamwaga, unashuka kuelekea njiapanda ya kwenda Doubles Gate, kisha unakunja kulia kuelekea Boom Gate kisha Mto Tigite. Unapita Wazaza alafu unashuka pale Ng'ombe, ndipo unaelekea kulia kuitafuta Masaki.....☹️
 
Enzi hizo masaki ikiitwa, kichangachui ilikuwa ukitaka kufanya shopping kuanzia oysterbay kule ubalozi wa marekani hadi kichangachui ( masaki) unaenda Morogoro store unapata mahitaji yako yote hapo plus huduma za posta. Petrol station ( sheli) ikiwa kando yake, yatch club ikiwa pale msasani peninsular na Oysterbay hotel kule coco beach kwa ajili ya starehe Mitaa yote ilikuwa tulivu kabisa nyumba zimetengana kwa michongoma tu Enzi hizo mbawala wakikamatwa kichangachui.

Kweli enzi hazirudi
Umenikumbusha mbali sana ...hapo mtaa wa Guba..toka morogoro stores unabonyea hadi oysterbay hotel...Nilipita miaka mitatu iliyopita ucku ..mtaa ulikuwa na machangu wakutosha!!

Sehemu za Mikocheni B zilikuwa mikondo ya maji..cku hizi kuna majengo mvua ikinyesha maji hadi ndani na kushakuwa uswazi kabisa
 
Hata Prof jay 99 alitoa wimbo wa chemsha bongo na moja ya mstari wake aliimba "Tulikuwa tukihama hama leo Obey kesho Mikocheni" - Miaka hiyo Obay,mikocheni,masaki,upanga ilikuwa full wa kishua.

Ni kweli mkuu mjumba mengi wanakaa walinzi,shamba boys ,beki tatu.

Mbweni (plots za kupimwa) kule ni hatari prime areas sana ,kule ndiyo USHUANI.

Kule Mbweni kwa Samia plots nadhani si chini ya milioni 300.
Unazungumzia Mikocheni A... maana kule Mikocheni B kulikuwa na mashamba tulikuwa tunaenda kulima ..mnaondoka nyumbani asubuhi mnarudi jioni. Nimeswaga Ng'ombe sana toka Obey hadi Mikocheni B
 
Masak naona imeanza kuwa uswazi, na mdogo mdogo inaanza kuwa ya kawaida saana, yani saana...

Bar na restaurants nyingi, na security ya premier residential inaondoka kwa kuwa na maghorofa yenye watu wengi sana, lakini zaid nyumba za ghorofa kumi kuendelea zinaongezeka sana.. soon itaanza fanana na Kariakoo.

Security kwa premier residential services ni priority... sasa hapa bungalow hapa ghorofa lenye apartments 40.

Hapo sijazungumzia frame na viduka uchwara.... hadi mama ntilie
Masaki kuwa kawaida kama Uswazi ni ngumu, ni kweli kuna watu wengi, ofisi na majengo mengi, bado mazingira yake, uwekezaji wake na wakazi wake bado ni wa kipato cha juu kuliko mitaa mingi ya Dar.
Na daraja jipya la Tanzanite tutegemee majengo marefu yatajengwa zaidi maana Masaki ina mazingira yanayovutia kwa wanaotaka ofisi za mashirika (corporates),

Halafu kitu kingine ni mipango ya jiji, ambapo mji hauna yale ma Free ways, yanayofanya wenye uwezo wapende kuishi mbali na mjini, hiyo inafanya Masaki iwe sehemu inayoendelea kuvutia watu wengi wenye uwezo wasitamani kuishi mbali sana na mji kwa sababu ya foleni., mfano Nairobi wana ile Nairobi freeway, barabara kama ile ina encourage watu kuishi nje ya mji.

Kwahiyo pamoja na mabadiliko yake, Masaki itabaki kuwa high income area
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;
Enzi hizo wakati naishi mimi ;

Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors .

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.
Sahivi unateseka ukiwa wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom