Masaki kuwa kawaida kama Uswazi ni ngumu, ni kweli kuna watu wengi, ofisi na majengo mengi, bado mazingira yake, uwekezaji wake na wakazi wake bado ni wa kipato cha juu kuliko mitaa mingi ya Dar.
Na daraja jipya la Tanzanite tutegemee majengo marefu yatajengwa zaidi maana Masaki ina mazingira yanayovutia kwa wanaotaka ofisi za mashirika (corporates),
Halafu kitu kingine ni mipango ya jiji, ambapo mji hauna yale ma Free ways, yanayofanya wenye uwezo wapende kuishi mbali na mjini, hiyo inafanya Masaki iwe sehemu inayoendelea kuvutia watu wengi wenye uwezo wasitamani kuishi mbali sana na mji kwa sababu ya foleni., mfano Nairobi wana ile Nairobi freeway, barabara kama ile ina encourage watu kuishi nje ya mji.
Kwahiyo pamoja na mabadiliko yake, Masaki itabaki kuwa high income area