Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Mzee Umekulia Masaki ,Vipi Mzee Wako Alikuachia Hata Kaplot Masaki?
Hapana mkuu kipindi hiko urban planning ilikuwa ikiheshimiwa mno maeneo mengi tayari yalikuwa yashajengwa yakilimilikiwa na serikali na taasisi zake kubwa,nyumba za mabalozi, diplomats, lazima uwe mtu flani ili kuishi huko!Baada ya serikali kuuza nyumba zake mabadiliko ndo yalianzia hapo if I'm not mistaken.
 
Kama ni hivyo basi Masaki ipo sawa bcoz hata hiyo miji niliyokutajia imechanganyika na ma office vilevile.
Hata manhattan ipo hivyo...sema huko ni Apartment tu hakuna nyumba yakuishi ya chini but zimechanganyika mbona.
 
Sitoshangaa Masaki siku zijazo ikifanana na Upanga kbs na ndiko tunakoelekea.
 
Boss maeneo ya kishua kbs lazima yawepo kwenye nchi yoyote inayojitambua!Usitufikirie sisi Wabongo wenzako wenye hali ya kawaida kuna diplomats, matajiri wakubwa duniani ambao wana standards zao!kwa kifupi Masaki imekuwa mixed na inazidi kuji disqualify kwenye level hizo so sorry to say that!
 
Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.


Hiyo hasa ndio ilikuwa point yako.

Lazima ujue Miji inabadilika sambamba na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, unaweza kukuta baadhi ya miji imekuwa "ghosts" na mingine imekuwa developed for better na hayo ndio maendeleo au kuporomoka kwa nchi kiujumla.
 
Na hii ilikuwa ni maeneo ya kishua tu huko uswahilini mambo yalikuwa yakitimbanganya vibaya mno especially lile bonde la msasani!.
 
Hapana mkuu point yangu ni kuona maeneo yote yakiachwa yakiendelea kiholela hii ndo point yangu kubwa.
 
Umemaliza kabisa
 
Haya ni matokeo ya kuuza nyumba za serikali chini ya JPM
 
Wacha mamneno mengi mura......
Masaki imejengwa juzi tu hapa tulikua tukipita Nywamwaga, unashuka kuelekea njiapanda ya kwenda Doubles Gate, kisha unakunja kulia kuelekea Boom Gate kisha Mto Tigite. Unapita Wazaza alafu unashuka pale Ng'ombe, ndipo unaelekea kulia kuitafuta Masaki.....☹️
 
Umenikumbusha mbali sana ...hapo mtaa wa Guba..toka morogoro stores unabonyea hadi oysterbay hotel...Nilipita miaka mitatu iliyopita ucku ..mtaa ulikuwa na machangu wakutosha!!

Sehemu za Mikocheni B zilikuwa mikondo ya maji..cku hizi kuna majengo mvua ikinyesha maji hadi ndani na kushakuwa uswazi kabisa
 
Unazungumzia Mikocheni A... maana kule Mikocheni B kulikuwa na mashamba tulikuwa tunaenda kulima ..mnaondoka nyumbani asubuhi mnarudi jioni. Nimeswaga Ng'ombe sana toka Obey hadi Mikocheni B
 
Masaki kuwa kawaida kama Uswazi ni ngumu, ni kweli kuna watu wengi, ofisi na majengo mengi, bado mazingira yake, uwekezaji wake na wakazi wake bado ni wa kipato cha juu kuliko mitaa mingi ya Dar.
Na daraja jipya la Tanzanite tutegemee majengo marefu yatajengwa zaidi maana Masaki ina mazingira yanayovutia kwa wanaotaka ofisi za mashirika (corporates),

Halafu kitu kingine ni mipango ya jiji, ambapo mji hauna yale ma Free ways, yanayofanya wenye uwezo wapende kuishi mbali na mjini, hiyo inafanya Masaki iwe sehemu inayoendelea kuvutia watu wengi wenye uwezo wasitamani kuishi mbali sana na mji kwa sababu ya foleni., mfano Nairobi wana ile Nairobi freeway, barabara kama ile ina encourage watu kuishi nje ya mji.

Kwahiyo pamoja na mabadiliko yake, Masaki itabaki kuwa high income area
 
Sahivi unateseka ukiwa wapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…