Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Mabibo hostel ilianza1998 kama sikosei,Ila ujue ubungo mi kubwa Sana,kibangu,maziwa,kibo,msewe,shekilango NHC,urafiki,mabibo hostel imeafect sehemu ndogo ya ubungo
Mabibo hostel haijaanza 1998,mpaka 2001 ilikua haijaanza tumika na kituo Cha daladala kilikua pale bakwata
 
Iko hivi miji inatanuka masaki ya zamani au sinza ya zamani au kinondoni ya zamani sio ya sasa hiviipo hivi watu wanahamia na watu wanaondoka kwaiyo miaka 20 ijayo masaki itakuwa ya kawaida kama sinza ya zamani kwaiyo mji mwingine utaibuka kuwa wakishua maana siku hizi wengi wanaamia kigamboni uko kuna mijengo ya maana au bagamoyo siku hizi mjini kuna makelele sana
Ndio akiliza zako zilipo ishia? Kuna miji haibadiliki miaka 100 kama ni eneo.la.makazi ni la makazi na pia kuna aina za nyumba zinatakiwa kujengwa, hapo, Ukweli mipango miji kwa Tanzania ni shida sana
 
Watu wanapokuwa na uchumi na kipato kizuri hujenga mijengo ya maana kipato kikipungua au kustaafu wanashindwa hata kuifanyia maintanance mijengo yao wakifa ndo kabisa mdogomdogo kauswahili fulani kanaanza

Nimeanza kuona hii kitu hata pale Mbezi Beach hata huko Mbweni itaenda mwisho wa siku vipato vikipungua itabaki historia

Haya ndio yanayotokea baadhi ya maeneo ya Masaki.
Roho ya kichawi
 
Mabadiliko haya yanatokana na kukua kwa mji pamoja na ongezeko la watu mjini. Nakubaliana na wote kuwa Masaki imebadilika sana lakini si Masaki peke yake hata maeneo mengine nayo yamebadilika kutokana na kukua kwa mji

Sinza leo badala ya makazi imegeuka kuwa sehemu ya biashara kama Kariakoo. Maeneo ya Kimara ambako kulikuwa ni nje ya mji watu walikuwa wanaenda kule kujenga makazi na ufugaji leo hii ni makazi tena overpopulated. Mji umesogea mpaka mkoa wa Pwani Bagamoyo na Kibaha imeungana na DSM
Ongezeko la watu
Ukuaji wa technolojia
Ongezeko la Waliosoma
Kuongezeka biashara

Haya yanasababisha sana watu wajitanue.
Kosa kubwa ni serikali ilishindwa pima viwanja na kupangilia matumizi mapema
 
Mkuu umekulia masaki ushuani.. siku hizi unateseka ukiwa wapi?
Baada ya kutoka Masaki tulihamia Oysterbay baada ya hapo nikaanza kujitegemea mwenyewe from msasani mafleti krb na ubalozi wa Marekani to Mbezi Makonde then Mikocheni B kwa sasa naishi Kinyerezi na ni kwa sababu ya kazi mimi si mpenzi wa kuendesha distance ndefu kwa kifupi nafanya kazi Julius Nyerere International Airport.Na siteseki, I live my life to the fullest.
 
Unazungumzia Mikocheni A... maana kule Mikocheni B kulikuwa na mashamba tulikuwa tunaenda kulima ..mnaondoka nyumbani asubuhi mnarudi jioni. Nimeswaga Ng'ombe sana toka Obey hadi Mikocheni B

Siyo Mikocheni ya Opposite na MayFair Plaza maana Kule ni full matola....Hata Obay ya Maandazi road /Macho nayo chaka.
 
Mabadiliko haya yanatokana na kukua kwa mji pamoja na ongezeko la watu mjini. Nakubaliana na wote kuwa Masaki imebadilika sana lakini si Masaki peke yake hata maeneo mengine nayo yamebadilika kutokana na kukua kwa mji

Sinza leo badala ya makazi imegeuka kuwa sehemu ya biashara kama Kariakoo. Maeneo ya Kimara ambako kulikuwa ni nje ya mji watu walikuwa wanaenda kule kujenga makazi na ufugaji leo hii ni makazi tena overpopulated. Mji umesogea mpaka mkoa wa Pwani Bagamoyo na Kibaha imeungana na DSM

Serikali inabidi itekeleze sheria zake ,watu huko dar wana ekari kibao wameziacha wala hawaziendelezi ,ndiyo wanafuga mapori ,ilitakiwa kama hawajaendeleza ndani ya miaka mitatu wanyanganywe wapime viwanja.
 
Back
Top Bottom