Nashangaa mpaka leo bado CCM na viongozi wa Serikali hawajajua tofauti ya wapinzani wa kaskazini na wa sehemu nyingine kama Kigoma au Mbeya
Huku Arusha, Kilimanjaro na Tanga tatizo kubwa sio barabara au madarasa ya shule. Ni sehemu ambayo ilikuwa na barabara nyingi za lami na shule nyingi ukilinganisha na sehemu nyingine lakini kulikuwa na wapinzani wengi.
Hivyo Rais Samia anavyoringia barabara na kujidanganya kwamba watu wamebadilika sio kweli watu wako vilevile.
Jamii ya huku Kaskazini tatizo lao na Serikali ni kwamba Serikali imekuwa kikwazo kikubwa kwa biashara. Serikali imeingilia biashara za madini kuwa na mpangilio, tozo biashara za utalii na hoteli. Lakini hii mikoa ya mipakana haipendi kusumbuliwa kwenye biashra za mpakani kama kuuza mahindi, vitunguu na kupita kwa magari.
Kwa ufupi watu wa Kaskazini wanataka Serikali ambayo ni pro-business na yenye mazingira mazuri ya biashara.
Wengi wa Kaskazini wanaamini vitu vingi wanaweza kufanya bila serikali lakini wanataka serikali isiwe vikwazo.
Upinzani wa sehemu nyingine kama Kigoma ni kutokana na serikali kuwasahau na kuona kama vile wenyewe hawapewi maendeleo kama barabara, reli, mazao yao, na ziwa Tanganyika. Lakini Mbeya nayo ni hivyo hivyo ni maendeleo ya barabara na maji ndiyo tatizo.
Hivyo Rais Samia kwenda Arusha na kuongea kuhusu maji kuliko biashara ni kutokujua jamii ya Kaskazini
Ili kutoa ukabila nijitambulishe mimi mwenyewe. Mimi nimekulia Arusha na Baba Mpare na Mama Mchagga hivyo nimechanganya kama wengine wengi