jamani angalieni hapa mjifunze kuhusu Kilimanjaro. Kungekuwa na maendeleo yanayosema Mbunge asingedhalilika namna hii kuomba fedha za maendeleo. Kilimanjaro ni zaidi ya mnavyoisikia.
cc
MkamaP,
Kamundu
Unaongea hisia zako, unaifahamu knjaro au basi unaongea ili na ww uonekane umepost
Unafikiri wabunge wa knjaro wataacha kulia kuomba fedha za maendeleo kwasababu knjaro inasemwa ina hali nzuri. Mwenye nacho anahitaji kuongezewa kila siku ili asonge mbele zaidi na zaidi..
Kusema knjaro kuna maendeleo siyo kwamba ni stori bali dunia nzima inajua hivyo na serkali inajua kwamba Ni mkoa ambao uko hatua nyingi mbele. Hata takwimu za serkali ktk nyanja kmbalimbali zinaonyesha hivyo.
Niseme wazi:Mimi Ni mchaga. Kwetu kuna umeme tangu mwaka 1985.
Sijawahi kubeba ndoo kwenda kutafuta maji ktk utoto wangu. Hatujawahi kunywa maji ya mtoni au chemchemi nyumbani kuna Bomba la maji tangu zamani hizo, na kulikuwa na mtandao wa maji bomba ya jumuiya kwa wasiokua na bomba majumbani.
Kwetu kwasasa karibu nyumba za udongo zinatoweka km ipo ni km kumbukumbu ya historia tu.
Shuleni wanafunzi wengi tulitembea chini ya nusu kilomita kuifuata shule na hiyo ni miaka ya 80.kijiji chetu kulikuwa na shule 4.Madarasa ya kisasa yenye vioo.
Leo utasikia huko mikoani shule ina mwalimu mmoja au wawili, darasa la fito vitu ambavyo knjaro walisahau miaka ya 70 au 80 mwanzoni.
Leo utakuta kata moja Ina sekondari 4
Isipokua kutoka same mjini kwenda mlimani huko na Ni kutokana na jiografia ya hiyo wilaya lkn moshi mjini imeunganishwa na lami na Wilaya nyingine zote. Na barabara zote za vijiji za vumbi zile kubwa na za halmashauri kila mwaka zinalimwa na zinapitika mda wote.
Nimeongea vitu vya kawaida sana ambavyo ni basic tu. Kimsingi Kilimanjaro siyo kwamba hakuna changamoto, zipo lkn siyo kwa viwango vikubwa km kwa baadhi ya maeneo mengine ya nchi.
Mfano changamoto ya maji ya uhakika ipo bado na Ila Ni kwa baadhi ya maeneo machache.
Juzi wakat wa ziara ya MH Rais Samia pale Moshi wabunge wengi waliomba barabara,ambazo ni km 5 au 6 unakuta Ni za kuunganisha tarafa na tarafa au maeneo fulani ndani ya Jimbo.Kiukweli jibu walilopewa wenyewe watakubali walichemka Sana kuomba lami.
Chasaka umenielewa.