Kuna Tofauti kubwa ya wadau wa upinzani wa Kaskazini na sehemu nyingine

Kwa hiyo ulitaka tanzanite iendelee kutoroshwa?
 
Mbeya ipi unayoiongelea? Mchango wa Mbeya kwenye pato la Taifa ni mkubwa kuliko Arusha.

Mbeya kulikuwa na shule kibao, bila mashule mengi Mbeya wengine huenda tusingegusa kabisa huko, tungekuwa tu kwetu huko Nyambitilwa nacheza ngoma ya mbina na kina Ng'wana Ituli
 
Hakuna anaetaka kupendelewa na serikali
 
Hizo lami kwenye migomba umejenga wewe?

Kilimanjaro airport na Arusha airport is just walking distance ulishasikia mtu analalamikia hilo?

 
Siku raia wengi wakizinduka na kufahamu ni wajibu wa msingi wa serikali kujenga barabara, vituo vya afya, masoko na kupeleka maji tutakuwa taifa la watu wanaojielewa.
 
Fuatilia data, same Ina shule nyingi na zinafanya vizuri
 
Si kweli mkuu maendeleo mengi kaskazini wamejiletea wenyewe ,hawakusubiri serkali iwaletee.

Hivyo huwezi kugawa keki ya taifa ambayo kila mtu kaitolea jasho halafu uniambie nisubiri. Kwani huko kwingine walikuwa wapi wakati wa kaskazini wanajibidiisha? Unakuta kabila zingine mfano Mzaramo ana ardhi ekari 2 au zaidi lkn amelima tuta mbili za tembele,miti mitano au 2 ya muhogo na kisamvu.Hapo anajiona mkulima hasa.

Ndiyo maana mchaga hazikwi porini tofauti na kabila zingine ukifa wanazika hukohuko. Watu wanadhani wachaga Ni wajinga au ushamba lkn iko siri ktk hilo. Km hutukuzi kwenu umepotea. Leo kila mchaga anajitahidi kuwa na makazi bora kijijini ili hata akiwa na tukio basi asije onekana hakuendeleza kwake. Ni aibu unaishi mjini umejenga vzr halafu ulikozaliwa kuko duni.
 
jamani angalieni hapa mjifunze kuhusu Kilimanjaro. Kungekuwa na maendeleo yanayosema Mbunge asingedhalilika namna hii kuomba fedha za maendeleo. Kilimanjaro ni zaidi ya mnavyoisikia.


cc MkamaP, Kamundu
Unaongea hisia zako, unaifahamu knjaro au basi unaongea ili na ww uonekane umepost

Unafikiri wabunge wa knjaro wataacha kulia kuomba fedha za maendeleo kwasababu knjaro inasemwa ina hali nzuri. Mwenye nacho anahitaji kuongezewa kila siku ili asonge mbele zaidi na zaidi..

Kusema knjaro kuna maendeleo siyo kwamba ni stori bali dunia nzima inajua hivyo na serkali inajua kwamba Ni mkoa ambao uko hatua nyingi mbele. Hata takwimu za serkali ktk nyanja kmbalimbali zinaonyesha hivyo.

Niseme wazi:Mimi Ni mchaga. Kwetu kuna umeme tangu mwaka 1985.

Sijawahi kubeba ndoo kwenda kutafuta maji ktk utoto wangu. Hatujawahi kunywa maji ya mtoni au chemchemi nyumbani kuna Bomba la maji tangu zamani hizo, na kulikuwa na mtandao wa maji bomba ya jumuiya kwa wasiokua na bomba majumbani.

Kwetu kwasasa karibu nyumba za udongo zinatoweka km ipo ni km kumbukumbu ya historia tu.

Shuleni wanafunzi wengi tulitembea chini ya nusu kilomita kuifuata shule na hiyo ni miaka ya 80.kijiji chetu kulikuwa na shule 4.Madarasa ya kisasa yenye vioo.

Leo utasikia huko mikoani shule ina mwalimu mmoja au wawili, darasa la fito vitu ambavyo knjaro walisahau miaka ya 70 au 80 mwanzoni.

Leo utakuta kata moja Ina sekondari 4

Isipokua kutoka same mjini kwenda mlimani huko na Ni kutokana na jiografia ya hiyo wilaya lkn moshi mjini imeunganishwa na lami na Wilaya nyingine zote. Na barabara zote za vijiji za vumbi zile kubwa na za halmashauri kila mwaka zinalimwa na zinapitika mda wote.

Nimeongea vitu vya kawaida sana ambavyo ni basic tu. Kimsingi Kilimanjaro siyo kwamba hakuna changamoto, zipo lkn siyo kwa viwango vikubwa km kwa baadhi ya maeneo mengine ya nchi.
Mfano changamoto ya maji ya uhakika ipo bado na Ila Ni kwa baadhi ya maeneo machache.

Juzi wakat wa ziara ya MH Rais Samia pale Moshi wabunge wengi waliomba barabara,ambazo ni km 5 au 6 unakuta Ni za kuunganisha tarafa na tarafa au maeneo fulani ndani ya Jimbo.Kiukweli jibu walilopewa wenyewe watakubali walichemka Sana kuomba lami.

Chasaka umenielewa.
 
Nyie ni sehemu ya tanzania hamuwezi kuendesha biashara bila kufuata sheria na taratibu za nchi.
 
Halafu pia utagundua kwamba kwa suala la barabara same ndiyo shida Ni kubwa na jiografia yake Ni milima. Lkn barabara wanazoomba Ni kutoka same mjini kwenda huko vijijini.

-Lkn Kuna lami toka moshi mjini hadi same mjini
-kuna lami kutoka nwanga mjini kwenda Milimani huko Usangi
-kuna lami toka moshi Hadi ROMBO (tarakea,Rongai hadi Kamwanga)
-kuna lami moshi-himo-marangu-kilema
- Kuna lami Moshi-kawawa road- kirua vunjo (mlimani huko)
-kuna lami Moshi-kiboriloni-Old Moshi(mlimani huko)
Kuna lami Moshi -machame(machame ya kina Mbowe)
-kuna lami Moshi-kwa sadala-machame
Kuna lami Moshi - kibosho(kibosho umbwe,kirima mweka)

HAKUNA MKOA MWINGINE ULIOUNGANISHWA HIVI.

Same Wana shida ya kipekee.

Na ukimsikia mbunge wa knjaro anaomba lami Ni ya kuunganisha kata, vijiji au tarafa kwasababu wilaya zilishaunganishwa tayari.au barabara fulani korofi ndani ya jimbo lake.

Mlio nje ya huu mkoa mkisikia mnahemka tu na hizo clip za You Tube lkn hamjui wabunge wanapigania nini.
 
This is...

Wewe unazungumzia wilaya na majimbo ya uchagani. Na mimi siwezi kubisha kuhusu maendeleo yaliyoko huko. Hoja niliyoweka mezani ni kwamba wilaya ya Same ambayo ni 40% ya mkoa mzima wa Kilimanjaro imetengwa na serikali na kuachwa nyuma kimaendeleo.

Kuhusu barabara ni kweli barabara toka Dsm kwenda Arusha inapita upande wa magharibi wa wilaya Same ambako ndiko uliko mji wa Same. Lakini eneo la magharibi la wilaya ya Same lina watu wachache kuliko eneo la mashariki. Pia eneo la mashariki lina biashara kubwa ya mazao kama mpunga, tangawizi, n.k, lakini lina barabara kuu pekee ktk mkoa wa Kilimanjaro ambayo haina lami. Barabara hiyo inapita Mkomazi--Bendera--Kihurio--Ndugu--Gonja--Kisiwani--Same.

Ukiacha barabara kongwe Mkomazi--Gonja--Same, barabara nyingi za kwenda milimani zina hali mbaya sana, haswa kipindi cha mvua. Kwa msingi huo mbunge wa Same anapoomba barabara ni tofauti kabisa na mbunge wa Vunjo, Marangu, Hai, anapoomba barabara. Mazingira yao hayafanani.

cc residentura , Kamundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…