Mkuu unaweza nyoa tu, na haina madhara yoyote.
Binafsi nilikuwa sinyoi hata kidogo, na mara nyingi nilikuwa naogopa hasa kauli kama hizi za Wachangiaji hapa Jamvini.
Nimeanza kunyoa baada ya malalamiko ya mke wangu, alikuwa akilalamika mno na nikaona isiwe tabu kwasababu mtu pekee anayeuona utupu wangu hapendi kuniona katika hali ya kuwa na mavinyweleo mengi nimejikuta situnzi hizo nywele na kinyozi mhusika ni yeye tena sehemu zote yaani kuanzia kwapa, chini ya kitovu mbele na hiyo sehemu inayokukwaza mkuu.
Na nimejikuta hata kufuga nywele za kichwani sio mpenzi kapisa maana hata mwenza wangu si mtu wa kufuga minywele.
Haya wanayo andika wanajamvi binafsi nadhani yana akisi kile wakifanyacho ama wafanyiwacho.