Inakuwaje kuuza nyumba ya urithi ukawa ubogus Kila mtoto alishakuwa mtu mzima na kwa bahati mbaya mambo yao hayajawaendea vizuri wanatafuta mitaji na kuuza nyumba ni the only way ya kuwa na mtaji ambao utakuwa hauna presha ya marejesho ambapo kwa malengo baadae wanaweza kuchanga na kujenga nyumba Tena kwa ajili ya familia nzima
Wewe Baba wewe; Unasema kila mtoto alishakuwa mtu mzima ila mambo hayajawaendea vizuri eti wanatafuta mtaji kwa kukiuka Agizo la marehemu? Tena unasema huo ni Mtaji ambao hauna presha ya marejesho!!!
Na unahitimisha kwa kuweka matumaini kwamba baadaye???? wanaweza kujenga nyumba kwa kuchangishana.......
Naomba uwe makini kwani:
1. Nyumba ikiuzwa manake kiwanja(Ardhi) imeuzwa. Hiyo "baadaye" matajenga wapi? Elewa iwe iwavyo, hamtakaa kamwe (milele)muweze kupata hapo mlipopauza.i.e. eg. Kitalu Na. xy kilichopo eneo D nyumba Na. Mtapata huko kwingine ila sio hapo alipokataza marehemu.
2. Je, kama Trend ya mambo kutokuenda vizuri ikawa ni endelevu na kutamalaki kwenu mtakimbilia kurudi wapi baada ya kupigika huko mtakakokwenda kuitapanya fedha ya mgawo mliyopata?? Kuna mdau hapo juu kasema mtaishia stendi.
3. Mkiuza nyumba na kila mmoja kupata mgawo stahiki; kila mmoja wenu atashika njia yake. Mtachangishanaje wakati mmeshatawanyika kila mtu na lake? Je, itakuwaje endapo mmoja kati yenu atakuwa katangulia mbele ya haki?
4. Uzoefu unaonesha kwamba Tamko la Marehemu mara nyingi huwa ndo Fainal. Kuzembea na kutotii kauli ya mwenye mali hata kama ni marehemu kunaleta usumbufu sana na wakati mwingine madhara. Marehemu alikufa kimwili lakini kiroho yupo.(
Hiyo ni kwa wenye Imani lakini)
5. Kwa sasa hivi unasema kuuza nyumba ndo the only way ya kupata Mtaji.
Hiyo kauli mara nyingi huwa ni kihalalishio tu ili kufikia lengo la kupata fedha.
Baada ya kuzipata fedha inakuja "ponda mali kufa kwaja"