Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Unajua kuna kupenda na kutamani,kama ni kupenda hata maandiko matakatifu yametutaka tupendane na amri iliyokuu ni upendo na kutamani ni dhambi isiyo kuwa na mjadala na utakuwa umekiuka moja wapo ya amri kumi ZA MWENYEZI MUNGU MUUMBAJI,soma kuanzia KUTOKA 20:1-..........
 
Uko nondo!
 
Lakini kumbuka Mungu alichukia sana alichokifanya Daudi kwa sababu kwa tamaa zake aliamuru pia Uria awekwe mstari wa mbele wa vita ili afie vitani amchukue jumla
Lakini kumbuka Daudi alimlilia sana Mungu amsamehe dhambi ile akiahidi atamchukua kama mkewe hiyo ndio ilikuwa salama yake daudi
Mungu hapa alimwacha kabisa Daudi kwa kuwa kuna amri mbili alizivunja Usizini, na usimtamani mwanamke asiye mkeo
Na kwa mujibu wa bible Daudi alitumia miaka 5 akimlilia Mungu amsamehe dhambi yake
We unaweza
 
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
MIT. 6:32‭-‬33‭, ‬35 SUV
MIT. 6:32-35; # Ayu 31:12; Ebr 13:4 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;Wala fedheha yake haitafutika. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu;Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi. Hatakubali ukombozi uwao wote;Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
 
siku 1 mkulu aipiga simu 360clouds akasema anataman azifaham familia za watangazajwa 360! siku waiyokuja mume wa baby alikua amevaa suti kuubwa sana sana !sasa jana walikua wanamsema maalimu sief kuvaa suti oversize nikawa nashangaa
Lengo la kuzifahamu familia zao ilikuwa ni nini? (nje ya mada, samahani)
 

Natamani ungempenda wangu, ningefurahi sana, maana mimi sijui.
 

Kwenye diwani ya CHUNGU TAMU kilichoandikwa na T. Mvungi kuna SHAIRI linaitwa FIKRA ZA WAUNGWANA moja ya beti za shari hilo unasema hivi:

Mume wangu nakupenda, Josefu amenikuna,
Nimekula naye tunda, nampendelea sana,
Ila usifanye inda, mimi ni wako kimwana,
Nitaishi kwa mpango, kwako na kwake Josefu.

Ukweli ni kwamba watu na hasa wanaume na wanawake hawapendi mali au vitu bali mapenzi tena yenye kuleta tija katika mahusiano. Wanaume huongozwa na tamaa ya macho na wakinogewa hukaa kabisa na manjonjo yakipungua hutafuta msaada kwenye tuta (nyumba ndogo/mchepuko).
 
Shetani mzima mzima ndo tunataka kumjadili. Daudi kumpenda mke wa alisababisha kupigwa sana na MUNGU,hata Taifa la Israeli lote pia lilipigwa. Wewe unaechangia angalia jinsi unavyochangia yasije kukukuta kutoka Mbinguni. Ni tahadhari tu.
 
Mie mke wangu anapendwa sana na wanaume niwaachia. Nimegundua hakuna mwanamke wa peke yako hivyo bora uishi bila mke wewe kuwa naye yeyote hata ukioa ni wa wote. Ila wanaume wengi wanajifariji kuwa mie mke wangu hana mme wa nje na hawapendi kujua ukweli ndo maana ndoa zao zinadumu lakini ukitaka kujua lazima ivunjike. Hakuna mwanamke wa pekee yako!! Nasisitiza hayupo!!!
 
Huu mfano wa Daudi mbona umetuingiza chaka mkuu??.

Mtoto wa Daudi alifariki kutokana na dhambi ya uzinzi aliyofanya baba yake, hiyo si baraka ni laana ya kizazi, Halleluyaa!!!.


_haya muda wa sadaka sasa [emoji23][emoji23]_
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…