Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Mkuu nilipitia hizo hali kidogo nife.

Nilifanya hivi...

Nunua limao 3 zikatekate Kama chips bila kutoa mbegu zake wala maganda.

Katakaa vitunguu maji vinne...


Weka vitunguu swaumu viwili.


Weka tangawizi 2 ( twanga)


Halafu chemsha kwa pamoja Hadi ichemke... Subiri ipoe halafu chuja glass moja unywe asubuhi na usiku ( ni chungu Sana Sana Sana).... Mimi nilipiga hiyo kwa siku kadhaa.


Kingine piga zoez , Mimi nilianza mazoez ya push up

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu nitajaribu kuzingatia ushauri wako
 
Nipo Songea Ruvuma mkuu kwa sahiv natumia mchanganyiko wa juice ya limao,Tangawizi na vitunguu swaumu vinanipa nafuu

ila changamoto ipo kwenye Kupumua Kuna muda nakosa hewa hadi naivuta mwenyewe kwa force...Usiku naogopa kulala maana nahisi nitakufa usingizini
mzee hata mimi ilikuwa hivo unawezaje kulala wakati unaona malaika mtoa roho anakusogelea, nilisema ni bora nife nikiwa naona kuliko nikiwa usingizini
 
Simulia sana ila omba yasikukute...Hapa nilipo sina uwezo wa kusikia harufu yoyote wala kuhisi radha ya chakula chochote

Viungo vya mwili ndio usiseme vinavouma...Pua zimeziba hii inaelekea siku ya 7 au 8 na hamna dawa ya mafua iliyonipa nafuu

Covid ni hatarii naamin nitapona tu inshaallah...
Utapona tu mkuu na kikubwa zingatia tangawizi na limau. Ivyo viungo vya mwili vinavyouma ni mateso makubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Songea Ruvuma mkuu kwa sahiv natumia mchanganyiko wa juice ya limao,Tangawizi na vitunguu swaumu vinanipa nafuu

ila changamoto ipo kwenye Kupumua Kuna muda nakosa hewa hadi naivuta mwenyewe kwa force...Usiku naogopa kulala maana nahisi nitakufa usingizini
Huwez kulala kwa iyo hali na mimi nilikaa siku 4 bila kupata usingizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzee hata mimi ilikuwa hivo unawezaje kulala wakati unaona malaika mtoa roho anakusogelea, nilisema ni bora nife nikiwa naona kuliko nikiwa usingizini
Kuna sehemu nilisoma/kuona wanashauri ukiumwa huu ugonjwa usilalie mgongo wako wanashauri ulalie tumbo au kiubavu ubavu
 
Nipo Songea Ruvuma mkuu kwa sahiv natumia mchanganyiko wa juice ya limao,Tangawizi na vitunguu swaumu vinanipa nafuu

ila changamoto ipo kwenye Kupumua Kuna muda nakosa hewa hadi naivuta mwenyewe kwa force...Usiku naogopa kulala maana nahisi nitakufa usingizini
Pole sana, kazania hiyo huduma uliyoianza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huamini Mungu yupo basi anza kusali leo kuna majanga ukipitia unatamani usali kwa lugha zote za ulimwengu huu, unamuona kabisa Israel mtoa roho anakukaribia Ule ugonjwa ulifanya niombe kila aina ya sala wakati kanisani nina miaka sijawahi kugusa, mafua makali, kizunguzungu na kuishiwa nguvu mara chache nikawa napumua kwa kuhema na kwa tabu sana haikuwa homa wala mafua ya kawaida niliyoyazoea

Siamini mpaka sasa niko hai japo sikupima lakini naamini ile ni hii new cases, zile wiki karibia 4 kasoro zilikuwa za mtihani mkubwa sana kwangu.

Naanza kwenda kanisani rasmi naamini ni mungu tu aliyeniponya
Hongera kwa kuijua kweli na kweli itakuweka huru
Mungu ni KWELI.
Na Mungu wangu akubariki sana.

Hii Ni nadhiri uliyomuwekea Mungu (kusali)
Hakikisha unaitimiza maana usipotimiza kuna gharama utailipia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom