Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Ss Mungu alivyi waajabu..wanatoka aalama hawaumwi mimi kipindi najihis nna malaria kumbe sio..mwanangu anakuja ananibusu mara nilishe namlisha ..nalala nae etc..baadar nilivyoanza kuona sinusi nikasema hili goma jipya hili limenikumba..nikaanza mwazia mwanangu but suprisingly mwezi ss tangu nipone walaa hajaguswa....so pray for them wako salama hao malaika lkn walinde usirelax

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo ulithibitisha kuwa ni gonjwa hili lililofungisha watu shule na vyuo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni hofu ndiyo inanipeleksha puta,,nahisi hili gonjwa litaleta ugonjwa wa msongo wa mawazo (depression) kwa watu wengi sana. Koo linakereketa kiasi na vichomi vya kishkaji vimeanza leo kwa pafu la kushoto. Sijui ndo corona hii make nimekunywa tu dawa za maumivu nikiombea nilale na kuamka salama.

Nine Google dalili za Corona naona zote sina isipokua kifua kubana kwa mbali ila hiyo hofu sasa ni balaa [emoji29][emoji29][emoji29] ,siwezi kujifungia ndani lazima nikasake hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Songea Ruvuma mkuu kwa sahiv natumia mchanganyiko wa juice ya limao,Tangawizi na vitunguu swaumu vinanipa nafuu

ila changamoto ipo kwenye Kupumua Kuna muda nakosa hewa hadi naivuta mwenyewe kwa force...Usiku naogopa kulala maana nahisi nitakufa usingizini

Poleni sana wana JF, inashauriwa kulalia tumbo usiku inasaidia pia zaidi
 
Mimi nimeugua na wadogo zangu nyumbani. Mdogo wangu mmoja imemchukua kama week mwingine kama siku 8 mimi siku 10 lakini tumepona tuko ngangari kinoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni hofu ndiyo inanipeleksha puta,,nahisi hili gonjwa litaleta ugonjwa wa msongo wa mawazo (depression) kwa watu wengi sana. Koo linakereketa kiasi na vichomi vya kishkaji vimeanza leo kwa pafu la kushoto. Sijui ndo corona hii make nimekunywa tu dawa za maumivu nikiombea nilale na kuamka salama.

Nine Google dalili za Corona naona zote sina isipokua kifua kubana kwa mbali ila hiyo hofu sasa ni balaa [emoji29][emoji29][emoji29] ,siwezi kujifungia ndani lazima nikasake hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu punguza mawazo fanya mazoezi hapo home hata kuruka ruka ili mradi utoke jasho ...

Mimi nilishikwa na huo ugonjwa naamini ni Mungu TU kanifikisha leo ... Nilikuwa najisikia na kuona ndoto za kufa , kichwa kuuma , vichomi, mbavu kubana , joto la mwili Kama lote.

Sema nilijikubali na nilisema hii ni corona na afe beki afe kipa nitapambana nayo ... Nilipiga juice za limao na panador ... Nikawa poa Hadi leo .... Ukiwa na mawazo utapata shida saaana sio kwa corona tu hata malaria.



Kingine tafuta Vidonge vya vitamini D na Zinc utakuwa poa kabla issue haijawa serious ukaanza kushindwa kupumua .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huamini Mungu yupo basi anza kusali leo kuna majanga ukipitia unatamani usali kwa lugha zote za ulimwengu huu, unamuona kabisa Israel mtoa roho anakukaribia Ule ugonjwa ulifanya niombe kila aina ya sala wakati kanisani nina miaka sijawahi kugusa, mafua makali, kizunguzungu na kuishiwa nguvu mara chache nikawa napumua kwa kuhema na kwa tabu sana haikuwa homa wala mafua ya kawaida niliyoyazoea

Siamini mpaka sasa niko hai japo sikupima lakini naamini ile ni hii new cases, zile wiki karibia 4 kasoro zilikuwa za mtihani mkubwa sana kwangu.

Naanza kwenda kanisani rasmi naamini ni mungu tu aliyeniponya
Mkuu ukiona mtu anakebehi uwepo wa Mungu jua ni ujeuri tu mambo hayajawakuta. Kuna maprof flan walienda Russia kusoma wakarudi bado ni vijana na PhD zao huku wamejaa ukomunist wakiwa wanasema live hakuna Mungu. Walivyoanza kuzeeka, huku magonjwa yamepamba moto, wengine wakarudi kimya kimya kwenye nyumba za ibada, wengine wakaenda mbali zaidi kuwa wanakwaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii kitu ilinipiga ..nikawa kila nikikaa nasikia ule wimbo wa niagieni ..niagieni...pua zote zikaziba...koo linakereketa...tumbo linasokota...ngozi inacharara...akili ikarudi kwenye 2G...nikawa nakula mlo kama nakula makapi...kusema kweli niliumwa mnoo..nauhakika asilimia 199.95% ilikuwa ni ile kitu...nilkuwa nikilala naota majeneza tu..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimejikuta nacheka aisee, hasa hapo pa niagieni niagieni[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimejikuta nacheka aisee, hasa hapo pa niagieni niagieni[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
haya mambo sikia kwa mwenzio tu...nilikuwa nawaza sana...nikiwaza madhambi niliyofanya hapa duniani naona kabisa nipo back bencher jehanamu
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
Back
Top Bottom